Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Status
Not open for further replies.
Leo hii asubuhi katika pita pita zangu za huku na kule, nilicho shuhudia ni kwamba watu wengi wanaamini Zitto ni msariti na wengi waowamekua wakimkandia kwa zile tuhuma ambazo CDM imekua ikizitoa dhidi ya Zitto.

CDM kama taasisi ikae ikijua kama tuhuma walizo elekeza kwa Zitto ni za kubuni na ni uzushi ikae ijkujua itafikia tamati, maana uongo auna uhai wa mda mrefu kama ukweli. Na hapo hawa wanao mkandia Zitto ndio watakua adui zao wakubwa na matokeo yake chama kitakufa.

Na kama tuhuma ni za kweli basi Zitto inampasa kukili madhaifu na ajisafishe, maana hakuna binadamu mkamilifu. Nae endapo hato fanya hivyo atakua na hali mbaya kisisiasa.

Zitto, wananchi wenye imani na wewe bado tupo wengi kutokana na utendaji wako, chukua fursa hii kuweka mambo sawa.

:dance:Kwani kuna shida gani? Hata ccm wamewahi mara chungu mzima kuondoa wanachama uoongozini tena wa ngazi ya juu na chama kikaendelea na kinaendelea. Haiwezekani watu wasio waaminifu na wasaliti waendelee kubaki kwenye uongozi na pengine hata chamani. Hata hivyo maudhui yaliyo kwenye waraka uliomfukuza Zitto na wenzake una hoja nzito na kama ni kweli ni lazima upande mwingine wa shilling uangaliwe. Hayo mapunguvu yaliyoko katika uongozi wa juu wa chama ni sharti yarekebishwe haraka. Kwa kuwa Chadema ni chama kikubwa na chenye wanachama wengi nchi nzima na ambacho ni tegemeo kubwa kwa wananchi wote bila itikadi, inabidi sasa mkutano mkuu uitwe haraka ili kasoro hizo zirekebishwe na chama kisonge mbele. Ni upuuzi wanachama kusema watakiacha chama chao kutokana na maamuzi ya kumwondolea Zitto madaraka. Kwa upande mwingine pande zote mbili ni za kulaumu. Upande wa Uongozi wa juu wa chadema, na Upande wa zitto. Ni uvumilivu tu umekosekana. Ni miaka miwili tu imebaki ambapo hicho chama wanachosema wao kimeletwa na Mungu ama kingeshika dola au kula sahani maja na ccm kwa maana kuwa na idadi ya wabunge wa kukaribiana sana. Hilo litawezekana tu kama kasoro zilizoelezwa kwenye waraka zitarekebishwa kwa spidi ya haraka ili chama kiongozwe kidemokrasia zaidi.
 
lazima tujifunze kuwajibika,kuleama ni sera ya ccm.heri chama kitetereke kuliko kulea dumilakuwili
 
Watu wengi sana wamepongeza uamuzi wa Kamati kuu , tunampongeza sana Zitto kwa kukiri usaliti , huo ndiyo uungwana , bila shaka video za tukio hilo muhimu zitawekwa ili kulinda ushahidi usipotee .
 
wewe haujawahi kufanya kosa na ukasemehewa?

Kosa husamehewa pale mkosaji anapokili kosa,nakuomba msamaha.Sasa ni lini ulimsikia Zitto kafanya hivyo!?Sanasana utamsikia akisema "yeye ndiyo ameifikisha CHADEMA hapo ilipo,hivyo hakuna wa kumtisha",sasa basi,kama ana nguvu kubwa hivyo na akaanzishe chama chake akikuze,atuachie Chadema yetu na ujinga wetu.
 
Wadau
Anachosahau Zitto ni kwamba hajui kuwa sifa haidumu sana kama mhusika anakosa adabu, wakati nasoma UDSM tulikuwa na watu wanaojiita TO (Tanzania one) yaani mtu aliyeongoza form six mwaka huo, vijana wale walikuwa wanalewa sifa kweli kweli mwaka 2008/2009 kuna moja alikuwa anasoma COET (BSc Telecom Engineering) alidisco mwaka wa pili si kwamba hakuwa na akili la hasha bali alijiona sana na mwisho wa siku hata discusion na wenzake hataki vile vile lecture kwake zilikuwa si muhimu.
Baada ya yule kijana kudisco wenzake (aliowamini kuwa ni vilaza) waliendelea na shule na wakapata Degree zao.

Zitto kabwe ni mlevi wa sifa: Taarifa za CDM zinaonyesha kuwa mahudhurio ya Zitto kabwe katika vikao na shughuli za chama ni approximate to 20%. sasa kama anaamini taasisi ya CDM ni nzuri ila watu wawili ndo shida kwanini asishirki ktk kuimarisha chama then afanya namna ya kutoa ushauri formally baadala ya WARAKA wa mabidiliko.
Zitto anaamini kuwa yeye ni zaidi ya Chama, yeye anajiona tu kama ameibuka na si kwamba amelelewa,
kwa wale wadau wa football mpira ni team work mkiwa na goalkeeper mzuri nanma gani kama beki si nzuri lazima team yenu ifungwe. lakini pia kama Beki ni nzuri na kipa pia yuko safi forward ikiwa butu mpira haitakaa mbele badala yake kila wakati mtakuwa golini na mwishowe mtafungwa.
kilichopo mbele na lazima kitimie ni kwamba Zitto atakuwa kama huyo kija wa mlimani aliyejiona kuwa ni Superstar, kwanini ZItto asijiulize maswali kwanini leo Mwingulu nchemba anamsifia wakati aliwahi kuchana Budget aliyoindaa yeye Bungeni?
Zitto unalewa sifa , lakini kuna methali nyingi sana na mifano hai za kukufunza, waangalie akina Hamad Rashid na Umaarufu wao ( walikimbilia Mahakama), Rafiki yako Kafulila aliliya mchana kweupe na mwisho wa siku alipiga magoti na sasa amesamehewa.
NB
; ZZK sifa ni Mbaya kama utalewa na CCM wanatumia watu kama mpira wa kiume (mtafute shonza, Lamwai na kabouru)
Haya ni sehemu ya maoni na ushauri wangu kwa ZZK &Co






 
Kupatikana kwa laptop ya Mwigamba Kweli kumezaaaa

Mkuu dont get distracted watu hawa document vitu vya hatari... Wanavifanya kwa verbal face to face communication ila kujilinda documentation inafanywa ku distract the second party kutumia luga ya third party kama ilivyo hiyo document!

Ukiona watu wana document strategies za hatari uelewe tu hao siyo smart maana risks ni very high kufanya hivyo! Siyo the kind ya hao they should be smarter than this! Wakifanya hivyo hata a secondary school student atawacheka!
 
Chadema mmeshindwa kuwa retain wanachama wenye hisia za CDM kuongozwa kwa misingi ya mfumo kristo na ukaskazini, badala yake mnajifanya nyie ndio kila kitu, majibu ya haya mnayofanya sasa mtayapata 2015, maana kila mtu anayewakosoa kwenu ninyi ni adui na mnadhani ni CCM, kwa sasa Muislam mwenye akili timamu wala mtu asiye wa kaskazini hawezi kuwapigia kura kama mnabisha mtaona 2015 kura zenu zitapungua sana.
 
hakuna watu wafupi wajeuri sana..nahasa awe mfupi halafu muislam..anakuwa hatari zaidi.....
 
Tukiendekeza marumbano, hatutofika tunapo taka kwenda.. Nchi yetu ni ya kutafuta solution na sio ku create matatizo.

Kosa husamehewa pale mkosaji anapokili kosa,nakuomba msamaha.Sasa ni lini ulimsikia Zitto kafanya hivyo!?Sanasana utamsikia akisema "yeye ndiyo ameifikisha CHADEMA hapo ilipo,hivyo hakuna wa kumtisha",sasa basi,kama ana nguvu kubwa hivyo na akaanzishe chama chake akikuze,atuachie Chadema yetu na ujinga wetu.
 
ukiyumbishwa kidogo nawe unayumba fanya maamuzi usikubali kutumiwa na kufuata mkumb
 
Mpuuzi wakufikiria wewe ,nyie ndio mtakaoadhibiwa .haya mambo ya udini unayoanzisha hayaana uhusiano na kinachotokea mvivu wa kuwaza idiote unataka kuharibu nchi yetu kwa kutugawa na issue zako za dini suwaini .useless!!!!!!!
 
wewe haujawahi kufanya kosa na ukasemehewa?

Msamaha unakuwepo pale unapokiri na kujutia kosa lako. Lakini huwezi kukosea kisha hutaki kutambua kosa lako halafu ulazimishe msamaha eti kwa vile wewe ni binadamu na binadamu hukosea.
Tuhuma za Zito zimeanza siku nyingi na yeye kaonyesha dharau sana. Kumbuka hizi harakati zimepoteza maisha ya watu,mali zao na wengine kuwa vilema. Sasa hilo sio jambo la mchezo kiasi cha kuliacha bora liende ili kulinda sifa ya mtu mmoja.
Wakati wa harakati za ukombozi South Africa kuna viongozi wa Wapiganaji wa ANC waliuawa na wenzao kwa sababu ya usaliti wa kuuza habari zao kwa makaburu, walichoka kupoteza maisha yao huku wengine wakiwauza kujinufaisha. USALITI NI HATARI SIO SIFA.
 
...hatupo kwaajili ya madaraka bali kusimamia ukweli haki na maslahi ya msingi/lengo la kuanzishwa kwa chama. So tunafahamu maana ya maamuzi magumu na tumejiandaa kwaajili ya watu wenye mtazamo kama wako...
 
Hiv mtu kuanza mikakati ya kuchukua madaraka ndan ya chama ni USALITI? Mbona mnawavsha watu ----- nyiee?watu mnaongea usaliti paspo kuupitia walaka unaodaiwa kuwa wa ZZK,somen kwanza mjue n kip kipo kwenye zle pge 13 ndo muanze kumlaumu mkigoma yule,he z clean
 
ZITTO angefanya utafiti wa reaction ya jamii juu ya ili suala angejua ni jinsi gani wananchi wanavyounga mkono kuondolewa kwake,hata Kigoma wengi wanadia ZITTO ni msaliti na hawajafurahishwa na haya maandalizi ya political prostitution kwani bila shaka siku si nyingi atatangaza kuhamia chama kingine.
 
hata mwenye mtindio wa ubongo anajua hila Zitto kuwa ni msaliti

Hata yeye mwenyewe anajua hilo maana aliomba kujiuzulu baada ya waraka wao wa siri , wao wakiuita waraka wa ushindi kukamatwa. WALIOMBA KUJIUZULU KABLA KAMATI KUU HAIJAKAA ili waonekane heros, ikanuma.
 
Leo hii asubuhi katika pita pita zangu za huku na kule, nilicho shuhudia ni kwamba watu wengi wanaamini Zitto ni msariti na wengi waowamekua wakimkandia kwa zile tuhuma ambazo CDM imekua ikizitoa dhidi ya Zitto.


CDM kama taasisi ikae ikijua kama tuhuma walizo elekeza kwa Zitto ni za kubuni na ni uzushi ikae ijkujua itafikia tamati, maana uongo auna uhai wa mda mrefu kama ukweli. Na hapo hawa wanao mkandia Zitto ndio watakua adui zao wakubwa na matokeo yake chama kitakufa.

Na kama tuhuma ni za kweli basi Zitto inampasa kukili madhaifu na ajisafishe, maana hakuna binadamu mkamilifu. Nae endapo hato fanya hivyo atakua na hali mbaya kisisiasa.

Zitto, wananchi wenye imani na wewe bado tupo wengi kutokana na utendaji wako, chukua fursa hii kuweka mambo sawa.


du tanesco rudisheni umeme akili za watu zimedumaaa....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom