Ufafanuzi: Majina ya watahiniwa wa darasa la saba yanayodhaniwa kuwa feki

kunena

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
506
711
Ufafanuzi wa majina ya watahiniwa wa Darasa la VII yanayodhaniwa kuwa feki kwenye mtandao wa Jamii forums

Kati ya shule zilizotajwa ni shule za Serikali zipo Arusha DC Loovikunyi (Usajili EM.5789, Kituo NECTA PS0101038) na Shule ya Msingi Lesiraa (Usajili EM.4578 Kituo NECTA PS0101036)

Majina yanayoonekana kwenye mtandao huu wa Jamii Forums sio majina halisi ya wanafunzi waliohitimu katika shule hizi. Mzalishaji wa uzi huo amefanya hivyo kwa malengo yasiyo mema ya kupotosha umma kwa kujaribu kuwaaminisha wafuatiliaji wengine wa uzi wake huo kuwa hayo ni majina feki. Ukweli ni kuwa orodha hiyo ni ya kujitengenezea kwa kutumia namba halisi za watahiniwa zikiambatanishwa na majina bandia kwa lengo la kuleta upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii.

Tunaomba umma ufahamu kuwa, matokeo rasmi ya watahiniwa wa mitihani ya Kitaifa inayosimamiwa na NECTA, inapatikana katika kurasa rasmi za mtandao wa NECTA (*www.necta.go.tz*)

Ukurasa huo wa Jamii Forums upuuzwe na pia ili kuwashinda wahalifu hawa, wanajamii wajenge utamaduni wa kutembelea kurasa za taasisi zinazohusika na utoaji wa taarifa rasmi kabla ya kuamini walichokiona kwenye kurasa za wapotoshaji wa mitandaoni.

Orodha sahihi toka chanzo sahihi kwa shule tajwa ni


 
Back
Top Bottom