Ufafanuzi kuhusu shares za Utuexchange

Mtade_Halisi

Member
Feb 23, 2008
28
0
Ndugu wadau wa JF naomba ufafanuzi wa yafuatayo kuhusu utuexchange

  • Ninanuaje hisa?
  • Ninauzaje hisa
  • Hisa moja ina thamani gani?
  • Nitapataje malipo yangu?
  • Nitanunuaje kama nataka hisa kwa fedha taslimu
UFAFANUZI TAFADHALI KWA WAHUSIKA...
 
Ndugu wadau wa JF naomba ufafanuzi wa yafuatayo kuhusu utuexchange

  • Ninanuaje hisa?
  • Ninauzaje hisa
  • Hisa moja ina thamani gani?
  • Nitapataje malipo yangu?
  • Nitanunuaje kama nataka hisa kwa fedha taslimu
UFAFANUZI TAFADHALI KWA WAHUSIKA...

Ni nini hii utuexchange? Bring us up to speed.
 
Maswali mazuri mkuu.

Kwa kifupi mkuu, UtuExchange ni mchezo unaoendeshwa kwa mtindo wa masoko ya mitaji. Lakini badala ya kufanyia biashara hisa za makampuni tunafanyia biashara hisa za matukio ya baadaye kwa lengo la kubashiri matukio yajayo kwa pamoja.

Aina hii ya michezo inaitwa "Prediction Markets" ( http://en.wikipedia.org/wiki/Prediction_market ). Inaitwa michezo lakini si kwa dhana ya mzaha, na imeonekana kuwa na uwezo mzuri wa kubashiri yajayo kuliko wataalamu wa eneo husika. Tafadhali pia check "Wisdom of the Crowds" ( http://en.wikipedia.org/wiki/The_Wisdom_of_Crowds ) .

Unaweza ukazichukulia kama kamari, lakini tofauti yake ni kwamba lengo kuu sio tu kucheza kamari na kushinda. Lengo kuu ni kujaribu kukusanya maoni ya watu kuhusu the future.

Kwa upande wa mfumo, zipo za mifumo tofauti, na UtuExchange inatumia mfumo wa masoko ya mitaji.

Kwa upande wa currency, Zipo prediction Markets zinazotumia fedha halisi, e.g. intrade.com, na zipo ambazo hazitumii fedha halisi. Na zimeonekana kutokuwa na tofauti kubwa sana katika usahihi wa bashiri zake.

Sasa UtuExchange hatutumii fedha halisi pia. Fedha yetu pale inaitwa U.

Kila mshiriki akishajiunga anapewa 25,000U kama mtaji ambao anaweza kuutumia kuanza kununulia hisa. Baada ya kutengeneza faida, faida yako itakuwa inakua, na utaweza kutumia faida zako kununulia hisa pia.

Sasa baada ya hayo naomba nikujibu maswali yako kama ifuatavyo.

1. Ninanunuaje Hisa?
Kununua hisa unapenda kwenye ukurasa wa dai unalotaka kununua hisa. Sehemu rahisi ya kuona madai ni katika ukurasa wa mbele.

Baada ya kuwa katika ukurasa wa dai, inategemea dai hilo lipo katika hatua gani:

IPO:
Kwenye hatua ya IPO, hisa zinatolewa kwa mara ya kwanza. Na utaratibu unaotumiwa hapa unafanana kidogo na utaratibu mpya unaoitwa "Open IPO" ambao kwa mfano google waliutumia.

Hisa zinapigwa mnada na kila mshiriki anayetaka hisa anaweka dau lake (namba ya hisa anazotaka, na kiasi ambacho yupo tayari kulipia). IPO ikifungwa, hisa zitauzwa kwa nusu ya washiriki wa mnada huo ambao wame-bid bei za juu zaidi. Ila bei watakayouziwa ni bei ya yule aliyeweka bei ya chini kabisa kati yao. (Kwa hiyo unaweza kupata hisa kwa bei ya chini ya bei uliyoombea, lakini si kwa bei ya juu zaidi ya uliyoombea).

Kushiriki kwenye IPO ndio njia rahisi na cheap zaidi ya kupata hisa.

Active
Kenye hatua hii watu ndio wanauziana hisa.

Kwenye stock market za kweli kununua hisa, unapeleka order yako ya kununua kwa broker wako, ukimwambia kisasi cha hisa unazotaka na bei ambayo upo tayari kununulia. Kama kuna mshika dau ambaye amepeleka na yeye order yake ya kuuza hisa zake katika bei ile unayotaka wewe au chini, basi biashara inafanyika kati yako na yeye. Kama hayupo, basi broker wako atasubiri mpaka mtu huyo atokee, ama mpka utakapoamua kuifuta hiyo order.

Vivyo hivyo ndani ya UtuExchange, unaweka order yako ya kununua hisa. Unaweza ukaona kama kuna wengine wanauza hisa zao na bei wanazouzia kabla hujaamua kuweka order yako.

Baada ya hapo, kama kuna mshikadau anayeuza kwa bei hiyo uliyotaka, basi biashara itafanyika, la sivyo system itasubiri mpaya atokee, au wewe uamue kuifuta hiyo order.

Kumbuka tu kwamba huwezi kununua hisa kutoka hewani. Inabidi kuwe na mtu ambaye ana hisa, na yupo tayari kuuza katika bei unayotaka wewe. Kama watu hawataki kukuuzia, pengine ni kwa sababu bei uliyo-offer ni ndogo. Jaribu kuiongeza na pengine mtu atashawishika kuuza.

2. Ninauzaje Hisa?

Unauza hisa ambazo umezipata kwenye IPO, au umeuziwa na mshika dau mwingine.

Kuuza hisa inafanana na kununua hisa. Unaweka order ya kuuuza hisa, na kama kuna mtu amweka order ya kununua katika bei hiyo au kubwa zaidi, basi biashara inafanyika. La sivyo order yako itasubiri mpaka huyo mtu atokee, au ufute hiyo order yako.

Kama watu hawanunui hisa zako, pengine umeweka bei ya juu zaidi ya ambayo wapo tayari kulipia. Kwa hiyo, pengine jaribu kushusha bei kiaina.

Short Selling
Kwa wanaofuatilia masoko ya mitaji, kuna kitu kinaitwa short selling. Kwa lunga rahisi pengine tunaweza kusema kwamba short selling ni kuuza hisa ambazo huna ukitegemea kwamba bei ya hisa itashuka. Bei ya hisa ikishuka kweli baadaye basi unaweza kutengeneza faida. La sivyo ikipanda imekula kwako.

Ndani ya UtuExchange ni ruksa kuuza hisa hata kama huna.
Maelezo mazuri yapo hapa:
http://www.utuexchange.com/community/node/2

3. Hisa moja ina thamani gani?
Kwa ujumla thamani ya hisa yoyote ndani ya UtuExchange ni kati ya 0U na 100U.

Kabla ya dai kufungwa
Thamani ya hisa inategemea na supply na demand, i.e. wewe na washiriki wengine ndio mna-influence thamani ya hisa. Kwa ujumla, matukio ambayo yanauwezekano mkubwa wa kutokea bei zake zitakuwa juu kwa sababu kila mtu atataka apate hisa zake. Matukio ambayo yana uwezekano mdogo wa kutokea, bei yake itakuwa ya chini kwa sababu walionazo watatamani kuziuza lakini wengine watakuwa hawapo tayari kuzinunua.

Wakati wa IPO, hisa zinapigwa mnada, na bei ya hisa itakuwa bei ndogo kabisa kati yabei ambazo walioshinda mnada huo wali-offer. Kumbuka walioshinda mnada wa IPO ni nusu ya washiriki wa mnada huo walio-offer bei ya juu.

Wakati dai linafanyiwa biashara, anayenunua ananunua kwa bei anayotaka, na anayeuza anauza kwa bei anayotaka. Biashara inafanyika pale bei ya muuzaji na ya mnunuaji ziko sawa.

Bottom line, supply na demand. Hakuna mtu anayepanga bei.

Baada ya dai kufungwa
Ila sasa baada ya dai kufungwa bei ya hisa itakruka kwenda 100U kama tukio hilo limetokea, na itaporomoka kwenda 0U kama tukio hilo halijatokea.

Na kama limetokea kila mwenye hisa katika dai hilo atapewa 100U. Kwa hiyo kama ulinunua hisa hizo kwa 60U utakuwa umetengeneza faida ya 40U.

Kama halijatokea kila mwenye hisa katika dai hilo hapati kitu. Kwa hiyo kama ulinunua hisa hizo kwa 60U utakuwa umepata hasara ya 60U.

Na kwa kuwa unawekeza kwenye madai amabayo unadhani yatakuja kuwa kwelie, basi ukibashiri sawasawa ndio unatengeneza faida. Unapata hasara ukibashiri visivyo.

4. Nitapataje malipo yangu?
Kama nilivyokwisha sema, ndani ya UtuExchange hatutumii fedha halisi.

Kama umetengeneza faida nyingi zaidi kuliko wengine wengi, njia pekee kwa sasa ya kufaidika na faida zako za U ni kujinyakulia tuzo.

Tuzo zinatolewa kwa mnada. Kwa hiyo anayetengeneza faida nyingi zaidi ndio yupo katika nafasi nzuri ya kujinyakulia zawadi. Kwa hiyo jinsi ambavyo unabashiri vizuri zaidi ndio jinsi unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kujinyakulia zawadi.

Baadaye kutakuwa na tuzo kwa waliotengeneza faida nyingi ndani ya mwezi, etc.

Lengo la kuwa na Tuzo hizi ni kuwazawadia wanaotengeneza faida nyingi, kwa sababu hawa ndio wanaotusaidia kubashiri sawasawa.

5. Nitanunuaje kama nataka hisa kwa fedha taslim?

Ndani ya UtuExchange hatutumii fedha halisi kwa hiyo hutaweza kufanya hivyo.

Ni bure kabisa kujiunga na kushiriki. Na hupotenzi kitu, bali unashinda tu kama unaweza kubashiri yajayo vizuri zaidi kuliko wengine.

Maelezo zaidi ...

Maelezo mengi yametolewa kwenye thread hii ya JF:
https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/19345-karibu-utuexchange.html

Na pia kuna maelezo mazuri hapa:
http://www.utuexchange.com/community/node/5

Na hapa kuna tutorials amabzo zinaweza kukupa mwanzo mzuri:
http://www.utuexchange.com/community/forum/3

Natumaini nimesaidia.
Karibu sana UtuExchange.
 
Pia pengine naweza kuzema kuwa UtuExchange ni seheme nzuri ya kufanyia mazoezi trading skills zako kabla hujaenda kwenye masoko ya kweli ya mitaji kama DSE.

UtuExchange inakupa platform nzuri ya kuelewa masoko ya mitaji yanavyofanya kazi, na kufanya mazoezi bila kujiumiza.

Kwa hiyo, kama wewe ni mpya kwa masoko ya mitaji, pengine ni vizuri ukaanza at http://www.utuexchange.com/ kabla hujamtafuta broker wako. Utajifunza kwamba kwenye masoko ya mitaji kuna hasara na faida pia na ni jisni gani inabidi u-weigh risks ili ku-minimize hasara na ku-maximize faida.
 
^^ Shukrani kwa maelezo mazuri, natumai wengi watajiunga huko ili kupanua wigo wao katika biashara
 
Back
Top Bottom