Ufafanuzi kuhusu Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Mkurugenzi wa Manispaa Musoma

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,633
2,297
Kulingana na maelezo ya Jasnira humu JamiiForum alidokeza kwa kusema "alisoma chuo kikuu Huria cha CommonWealth cha Uingereza alipohitimu shahada ya Uzamivu (PhD) in management akahitimu mwaka 2012".

Kama ni hivyo, ukweli kuhusu hicho chuo huu hapa :-

i) Kiuhalisia hakuna chuo kama hicho - Ukitembelea website ya commonweath open University, utagundua kuwa imekuwa registered British Virgin Islands lakini jengo lao halipo.

ii) Kuonyesha kuwa ni feki, wamejaribu kutoa simu yao, ila hizo zote na fax number pamoja na address ni za Spain ambazo ni :- commonweath open University, P.o Box 124,Austurias Spain, Tel:(34) 985274241

iii) Pia commonweath open University imekuwa registered kama kampuni lakini haina learning institution yeyote (matata, 2006).

iv) This is unaccredited entity, so their degrees are not recognized and US won't be accepted by civil service

v) Katika kitabu cha CommonWealth association members, hiki chuo hakijaorodheshwa

vi) Kiufupi ni kwamba, hicho chuo hakipo na hao jamaa wanaotoa hizo shahada ni matapeli.

Tamisemi mmekaa kimya, upo wapi uhalali wa huyu mtu kuendelea kusaini kwenye documents za serikali kama Dr (PhD holder)?
 
Hatujamkomalia Kaka, ndo facts zenyewe hizo. Maana watanzania pale unaposema maneno yenyewe bila kuweka details hawachelewi kusema ni majungu hayo. Mara, tumenyimwa tenda. Sasa huo ukweli na kunyimwa tender wapi na wapi.
 
Maelezo ya bwana "Janko" yanasomeka hivi "The University is not state approved /lincensed,and their website is attractively presented but I couldn't find any real authorization to grant degrees" Mwisho wa kunukuu. Alimaanisha hicho chuo cha CommonWealth Open University.
 
Kwa hivyo baada ya upelelezi wako kwa huyu jamaa na ukagundua ana vyeki feki unapendekeza aachishwe kazi sawa? Muone Mungu ndg yangu.Baya gani kubwa alilokufanyia huyu bwana hadi kumchimba kiasi hicho. Vibaya ufanyavyo!
 
Kwa hivyo baada ya upelelezi wako kwa huyu jamaa na ukagundua ana vyeki feki unapendekeza aachishwe kazi sawa? Muone Mungu ndg yangu.Baya gani kubwa alilokufanyia huyu bwana hadi kumchimba kiasi hicho. Vibaya ufanyavyo!
watu wako na original PHD wakowako tu huyu jamaa jipu.

swissme
 
Kwa hivyo baada ya upelelezi wako kwa huyu jamaa na ukagundua ana vyeki feki unapendekeza aachishwe kazi sawa? Muone Mungu ndg yangu.Baya gani kubwa alilokufanyia huyu bwana hadi kumchimba kiasi hicho. Vibaya ufanyavyo!
Elimu na iheshimiwe na watu wote.
 
Ndo maana ile slogan ya UKAWA ya elimu elimu elimu, kiujumla ilikuwa nzuri. Maana haiwezekani mtu mkubwa kama huyu serikalini awe na cheo hicho na serikali bado imemfumbia macho
 
Tunaiomba serikali kupitia wizara ya elimu, utumishi mjue kuwa hakuna chuo kama hicho. Kama kingekuwa chuo ofisi zao zingeonekana UK. Maana wana claims kuwa ofisi zao zipo (palm chambers, Virginia islands).
 
Serikali inabidi iwe macho ili kukomesha ununuaji wa vyeti feki hasa kwa watawala (viongozi) wetu. Atakae taka details zaidi, aseme nimpe kuhusu hiki chuo.
 
Baada ya uhakiki wa wafanyakazi hewa kumalizika ufuate uhakiki wa wenye vyeti bandia ili shule ipate heshima yake stahili! PhD halali inapatikana kwa mtu kusoma chuo kikuu kwa muda wa miaka 3+ halafu wengine wanaipata kwa sekunde 3 tu tena kwa kutumia fedha walizotuibia wananchi, hii haikubaliki! Eti Dr, labda wa Mafenesi!
 
Baada ya uhakiki wa wafanyakazi hewa kumalizika ufuate uhakiki wa wenye vyeti bandia ili shule ipate heshima yake stahili! PhD halali inapatikana kwa mtu kusoma chuo kikuu kwa muda wa miaka 3+ halafu wengine wanaipata kwa sekunde 3 tu tena kwa kutumia fedha walizotuibia wananchi, hii haikubaliki! Eti Dr, labda wa Mafenesi!
Aisee utafanya watu wafe kwa pressure.
 
Dada jasnira, umesoma huu uzi vizuri kweli? Mi nashangaa sana watanzania, eti mtu akisema ukweli baadhi wanasema oh ni kupakana matope. Sasa muulize, eti mkuu vyeti vyako ni kutoka chuo kipi?
 
Kama kimbunga cha vyeti bandia kitatokea, basi kitaondoka na wengi, wapo waheshimiwa sana wengi tu walio jificha kwenye mwamvuli huu.
 
Ni kweli gwakipanga. Hivi serikali inaogopa nini? Ndo maana kuna sehemu zingine maamuzi watendaji wengi wanakurupuka. Maana hawajiamini ktk kazi zao.
 
About Commonwealth Open University
COU provides adult continuing education. It was developed to meet the needs of adults by offering non-resident degree and other programs on an international basis. The programs have been organized and developed using as a starting point the "off-campus" external degree concept tried and tested by the various "universities without walls".

There are no entry requirements for undergraduate courses. You decide how long you will take to complete your course work. While you are studying, a teacher will be available to offer help, answer questions, and guide you through the learning process, but students are free to choose their own study pace.

As an institution of distance learning, COU has been able to assemble a faculty of recognized experts from throughout the global marketplace. Our faculty consists of university professors, business executives, consultants, and other specialists. Though these instructors vary in subject matter expertise, they share important attributes. All of them are actively practicing what they teach, and they are skilled in imparting their knowledge through distance learning channels and technology.

COU is committed to providing equal opportunities for study. We welcome applications from English and Spanish speaking people of all nationalities and from any background, regardless of race, gender, sexual orientation, age, occupation, marital status, sensory or physical disability, religious or other beliefs.

Commonwealth Open University is an international institution registered and established in the British Virgin Islands (U.K.), which has many students all over the world. COU educational programs are acknowledged as the foremost, with an excellent academic reputation. COU staff and lecturers are very committed to quality in services.

Our graduates have had remarkable success in having their degrees accepted. We will gladly supply information to potential or current employers or institutions.

Accreditation and recognition is an extremely complex issue, given that there are hundreds of accreditation bodies around the world, and no course is ever going to be accredited or recognized everywhere. The important thing is that you choose education that is going to be meaningful for what you need. The best indicators of our credibility are the quality of our staff and the testimonials from our students. COU is accredited by the accrediting commission of Wiener School for Advanced Studies on Global Education and Distance Learning. Accreditation is an assurance and a guarantee that the learning offered is of uniform and sound quality. COU has been assessed, examined, and verified by WSAS


PhD anaweza kuwa nayo lakini alipopatia ndio issue, kama nchi haina culture ya kupima quality za vyeti vinavyopatikana ktk vyuo na inaangalia una Masters, degree au PhD huna jinsi
 
Back
Top Bottom