Kwa kuwa source yako ni Biblia acha nikusaidie kidogo, kama ni wa kusaidika na sio sikio la kufa. Nimesoma andiko lako ila inaonekana hata hujui unachokisema, umenakili mahali au umekurupuka toka mahali kuandika au tu umeamua kupotosha kwa makusudi yako.
Vyovyote iwavyo vile, acha nijaribu kukusaidia, kama ni msaidika!
Sura ya 13 ya Kitabu ulichonukuu inaongelea juu ya wanyama wawili. Kwa kuwa unamuongelea wa kwanza (mpinga Kristo) acha nibakie hapo. Kwa mwenye akili timamu, na anayetafuta kujua, sifa za huyu mnyama zipo kuanzia mstari wa kwanza kabisa:
Ufunuo 13
1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. 2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. 4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? 5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. 7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. 8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
9 Mtu akiwa na sikio na asikie.
Sasa kama una sikio nadhani umesikia. Mtu ambaye kichwa kimejaa makufuru, anapewa uwezo na shetani, anasimamia enzi ya shetani, dunia nzima inamsujudia kana kwamba ni mungu, anamtukana Mungu na kuua watu wa Mungu, huyo sio mtu muovu, ila ni taswira iliyojengwa blah, blah? Kama una sikio la kusikia basi naamini umesikia!
Ufunuo 20
11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. 15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. 16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.
Mnyama na Jeshi lake Washindwa
17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu; 18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.
19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake. 20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; 21na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.
Hii sura ni mwisho wa wanyama hawa wawili. Kristo original anapokuja, kwenye vita kuu kule Meggido, mpinga kristo anaongoza vita dhidi ya Kristo. Kwa mujibu wa Biblia, ambayo ndio chanzo chako, Masihi ndio starring. Hapa jamaa wanatupwa kwenye ziwa la moto, kabla hata ya shetani. That's how bad this dictator is going to be. Shetani atawa join miaka 1,000 baadaye.
Pasipo na shaka, huyu mpinga Kristo kwa mujibu wa Biblia ambacho ndio chanzo chako, ni mtu muovu sana. Na ameelezewa vizuri sana tabia zake na atakayoyafanya. Na kwa sababu hiyo, bandiko lako ni la uongo.
Nimesoma sehemu iliyobakia ya andiko lako, umejichanganya tu. Inawezekana kabisa hata hiyo Biblia sio msomaji. Maana si kwa kupuyanga huko!