Uenyekiti CUF: Nani atamrithi Prof. Lipumba?

Uenyekiti CUF: Nani atamrithi Prof. Lipumba?

Toosweet

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2012
Posts
2,140
Reaction score
1,983
Salaam Wanajamvi.

Nimejaribu kutazama siasa za ndani za CUF hasa bara na kubaini kuwa hawana utaratibu wa kukuza na kuandaa vijana wanaharakati ili iwe hazina ya chama kama wenzao CHADEMA ambao wana vijana tele wenye uwezo wa kuitisha mikutano na kuhutubia.

Nani wata 'Takeover' wakongwe wakiondoka?

Tujadili.
 
Lipumba na mbowe hawana tofauti ni wenyeviti wa kudumu
 
Lipumba na mbowe hawana tofauti ni wenyeviti wa kudumu

Hao ni viongozi wa milele,toka mwanzo wa vyama vyao hadi leo hawaachii ngazi ya uenyeviti. Ndo huwa natathmini kuwa hizi ni NGOs na si vyama vya siasa kwani hakuna utofauti ni taasisi ya mama Kijo bisimba alokaa pale toka 1974
 
ni wakati wa CUF kuwaandaa sasa, mtatiro ndiye aliyetakiwa kuongoza kwa sasa.
 
Hao ni viongozi wa milele,toka mwanzo wa vyama vyao hadi leo hawaachii ngazi ya uenyeviti. Ndo huwa natathmini kuwa hizi ni NGOs na si vyama vya siasa kwani hakuna utofauti ni taasisi ya mama Kijo bisimba alokaa pale toka 1974
kama vitu hujui bora ukae kimya tu......hapo kwenye mwaka 1974 LHRC Haikuwepo ....lhrc imeanzishwa katikati ya miaka ya 1990....halafu LIPUMBA siyo mwenyekiti wa kwanza wa CUF.......Wala Mbowe si mwenyekiti wa kwanza cdm....ni Mwenyekiti watatu wa chadema toka mwaka 1992....ccm toka mwaka 1977 (1954?...1960' (TANU) Wamepita wenyeviti wanne tu..........
 
Usiwe na mashaka wakti ukifika atapatika mwenyekiti makini kabiisa.
Tena msomi alieandaliwa . Sio kama mbowe au magufuli.
 
mbowe anapenda umaalufu,akiachia kiti atazimika mazima.
 
Usiwe na mashaka wakti ukifika atapatika mwenyekiti makini kabiisa.
Tena msomi alieandaliwa . Sio kama mbowe au magufuli.

Magufuli ni mwenyekiti wa wapi KANYENYE?
 
Kunani huko CUF?

Yaani CUF ni Trick mnafanya ama tatizo ni nini? Wakati CCM wanajipanga CUF ndo mnapanga mambo ya BARAZA kuu, tena late kabisa? Kuna tatizo gani kuwaita hao wajumbe wa Baraza kuu hata kesho?

UKAWA, wananchi wana shauku ya kujua mgombea, Tatizo ni nini?

Eti Baraza kuu, wakati mnampitisha Lipumba awe mgombea mbona hamkungoja baraza kuu.

CUF acheni kuchezea Watanzania, iteni Baraza kuu hata Kesho.

UCF mkija kutusaliti, oohoo shauri yenu...
 
kama vitu hujui bora ukae kimya tu......hapo kwenye mwaka 1974 LHRC Haikuwepo ....lhrc imeanzishwa katikati ya miaka ya 1990....halafu LIPUMBA siyo mwenyekiti wa kwanza wa CUF.......Wala Mbowe si mwenyekiti wa kwanza cdm....ni Mwenyekiti watatu wa chadema toka mwaka 1992....ccm toka mwaka 1977 (1954?...1960' (TANU) Wamepita wenyeviti wanne tu..........

Hakuna Mwenyekiti asiye na ukomo CCM, ukomo wa kila Mwenyekiti unajulikana. Mfano Mh. Kikwete ukomo wake ni 2016, anayefuata ni Magufuli ambaye naye ukomo wake ni 2026.
 
Back
Top Bottom