Uenyekiti CCM: Jakaya Kikwete imetosha!

Status
Not open for further replies.
Unamwambia hivyo fisadi? Basi subiri km ndoto yako inaweza kutimia....siku hizi chama ni cha familia, sasa ukimuondoa kwenye uenyekiti alafu akina riziwani na salma wapo kwenye jumuiya umesaidia nini....this is a family pary na urais ni mradi wa familia
 
Ushauri wangu;

Wakati umefika wa kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti wa chama kwa sababu zifuatazo;

-utawala wa JK umekumbwa na madhaifu mengi ya kiuongozi na kiutendaji na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi.
Kwa kiasi kikubwa udhaifu huu umetokana Na kuchanganya maslahi ya chama na maslahi ya taifa

-Mheshimiwa JK ameshindwa kufanya maamuzi magumu yenye maslahi ya nchi kwa sababu yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho serikalini na ndani ya chama. Hivyo kukosa msukumo nje ya taasisi yake ya urais

-Mheshimiwa amekuwa na majukumu ya kiserikali na kichama na hivyo kumzidia kiasi kwamba mambo mengi hayafanyiwi maamuzi na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa utendaji wa serikali.

-akiwa Kama rais na mwemyekiti wa chama tawala kama hatafanya maamuzi sahihi hakuna wa kumkosoa au kumshauri. Hii inapelekea nchi kuongozwa kiimla (ki-dictator)

-chama kinapokuwa kwenye migogoro kama ilivyo sasa, rais anajikuta akishughulikia kutatua migogoro ndani ya chama zaidi badala ya kushughulikia Masuala ya kitaifa.

-Hii ya kubaki na kofia moja ya urais vile vile itamfanya rais ajione kuwa anawajibika zaidi kwa watanzania wote na si kwa ajili ya kupendezesha wana CCM

-rais huyo huyo hawezi kujisimamia katika kutekeleza ilani ya chama. Mwemyekiti atamkumbusha rais endapo rais atasahau au kupuuzia kutekeleza yaliyokubalika kwenye ilani

-chama kikiyumba lawama atabebeshwa mwemyekiti wa chama na si rais kama ilivyo sasa.
Kwa kuwa na kofia mbili rais anabebeshwa lawama za chama na lawama za makosa yanayosababishwa na serikali na hivyo kusababisha stress kubwa ( msongo wa mawazo) kwa kiongozi wa nchi.
Hiki kitu si kizuri kiafya na kinapunguza kwa kiasi kikubwa performance (utendaji) ya rais

Ingawa mi si mwanachama wa CCM Nimeona nitoe Ushauri huu kwani kama utazingatiwa na Kufuatwa ili kumpunguzia rais majukumu na rais akatenda majukumu yake bila udhaifu basi watanzania wote tutafaidika na Maendeleo bila kujali itikadi zetu

kutenganisha hizi kofia ni kumpunguzia majukumu ya chama ili ashughulikie maslahi ya taifa zaidi.

Hiki si kitu kigeni na wala hakipingani Na katiba ya CCM.

Mwalimu Nyerere alipong'atuka urais na kumwachia Mh mwinyi, aliendelea na uenyekiti wa chama kwa muda hadi hapo mwl alipoamua kuachia na uenyekiti. Hakuna mgogoro uliojitokeza kwa hili kama wanachama wengi wa CCM wanavyoogopa.

CCM fanyeni maamuzi magumu, msiogope mabadiliko, tenganisheni hizo kofia ili kumpa rais muda zaidi wa kushughulikia Maendeleo ya nchi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Inafaa Ndugu Kikwete apumzike sasa. Amelitumika Taifa kiasi cha kutosha. Kazi aliyofanya ni nzuri, lakini there is nothing to be gained kwa yeye kuendelea kuwa CCM Chairman. Kikwete ni spent force.

Nawasilisha hoja.
Wewe ni mwana CCM kweli?
Maoni yako hayawezi kuwa ya dhati.
Tungependa kufahamu maoni hayo hayo juu ya Mzee Mtei na Mwenyekiti Mbowe wa CDM.
 
Wewe hukuiona heading niliyoiweka katika hii posting,''Nataka kwenda Dodoma kumgaragaza Jakaya Kikwete'',lakini mod. katika 'hekima' yake ameibadili,imekuwa ''Jakaya imetosha.'' It is what they call 'censoring' of The Press.[I call it the Jewish Conspiracy]

Andrew Nyerere
CCM sio kikundi cha wahuni tuna utaratibu wetu maamuzi hayafanywi na mjomba wala baba mkwe; wewe kama unataka kuingia kwenye kiminyano hujakatazwa fuata taratibu zinazohusika; inashangaza mtu mzima na wenye hekima kama wewe umejiingiza kwenye siasa za uzushi zinazofanywa JF; wewe kama umeona Jakaya ametosha bado kuna wanaccm wengi tu wanahitaji uongozi wake. CCM hivi sasa ipo njiani kuua siasa za makundi inakuwaje wewe unataka kuturudisha kwenye makundi? CCM sio chama cha kifalme kuwa mtoto Nyerere haimaniishi wewe ni kiongozi wa CCM; usijivunjie heshima yako; kama unataka kujiingiza kwenye siasa za CCM gombea kwa kufuata taratibu; hiyo ndiyo demokrasia tuliyofundishwa na Mwl, Nyerere (R.I.P). Mpaka sasa hivi CCM ndio chama tegemeo la watanzania; hivi vya ruzuku kama Chadema watanzania wameshavishtukia.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Sijawahi kuona mtu wa hovyo kama wewe!!
Kama ndiyo ubora wa wanaCCM huo basi chama chenu kimekufa kabisa!! ndio maana hata mwenyekiti akiwa na akili kama mbuzi kabisa nyie mnaona mzuri tu!!!

Nani kakwambia JF kuna siasa za uzushi! ndivyo mnavyo danganyana!! Wewe umeficha jina lako lkn Andrew yuko wazi na anauhuru kutoa maoni yake kama mtanzania yeyote yule na wala hajawalazimisha mahali popote kufuata maoni yake.

Jibu hoja.... mwenyekiti wenu dhaifu mno...acha kukimbilia kutukana Mtu ili ajisikie vibaya!! Hivi unaweza kumfananisha mtoto gani wa Nyerere na wa Kikwete kwa kiherehere na kujaa tuhuma za ufisadi?

Acha kuendekeza uchumia tumbo! Think!
 
Inafaa Ndugu Kikwete apumzike sasa. Amelitumika Taifa kiasi cha kutosha. Kazi aliyofanya ni nzuri, lakini there is nothing to be gained kwa yeye kuendelea kuwa CCM Chairman. Kikwete ni spent force.

Nawasilisha hoja.

ccm safi aliondoka nayo baba yako.iliyopo ni ccm ya vigogo na watoto wao.ushauri uliotoa ni mzuri lakini usitegemee jambo kama hilo kutokea.
 
Sijawahi kuona mtu wa hovyo kama wewe!!
Kama ndiyo ubora wa wanaCCM huo basi chama chenu kimekufa kabisa!! ndio maana hata mwenyekiti akiwa na akili kama mbuzi kabisa nyie mnaona mzuri tu!!!

Nani kakwambia JF kuna siasa za uzushi! ndivyo mnavyo danganyana!! Wewe umeficha jina lako lkn Andrew yuko wazi na anauhuru kutoa maoni yake kama mtanzania yeyote yule na wala hajawalazimisha mahali popote kufuata maoni yake.

Jibu hoja.... mwenyekiti wenu dhaifu mno...acha kukimbilia kutukana Mtu ili ajisikie vibaya!! Hivi unaweza kumfananisha mtoto gani wa Nyerere na wa Kikwete kwa kiherehere na kujaa tuhuma za ufisadi?

Acha kuendekeza uchumia tumbo! Think!

Mkuu akili yako safi? Jina langu Chama unataka nitumie jina gani za hilo? Mpaka leo hujajua JF ni kiwanda cha uzushi? Andrew ana uhuru wa kutoa mawazo si lazima nikubaliane naye; manayekubaliana naye ni nyie mashabiki wa siasa za uzushi; Andrew kama yeye ni mwanaccm anatakiwa ajue taratibu za chama; kama ana maoni ya kubadilisha utaratibu wa kupata mwenyekiti anatakiwa atumie vikao halali vya chama kupitisha mawazo yake sio kuja kupiga porojo JF. Nina wasiwasi kama kweli Andrew ni mwanachama wa CCM; wanachama tunafahamu utaratibu wa chama chetu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wewe ni mwana CCM kweli?
Maoni yako hayawezi kuwa ya dhati.
Tungependa kufahamu maoni hayo hayo juu ya Mzee Mtei na Mwenyekiti Mbowe wa CDM.
Hivi Freeman Mbowe alishindana na nani katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA?.....

Nakumbuka Zitto alichukua fomu za kugombea, wazee wakamshauri ajitoe......

Sijui tatizo lilikuwa ni nini hasa....
 
Last edited by a moderator:
Mkuu akili yako safi? Jina langu Chama unataka nitumie jina gani za hilo? Mpaka leo hujajua JF ni kiwanda cha uzushi? Andrew ana uhuru wa kutoa mawazo si lazima nikubaliane naye; manayekubaliana naye ni nyie mashabiki wa siasa za uzushi; Andrew kama yeye ni mwanaccm anatakiwa ajue taratibu za chama; kama ana maoni ya kubadilisha utaratibu wa kupata mwenyekiti anatakiwa atumie vikao halali vya chama kupitisha mawazo yake sio kuja kupiga porojo JF. Nina wasiwasi kama kweli Andrew ni mwanachama wa CCM; wanachama tunafahamu utaratibu wa chama chetu.

Chama
Gongo la mboto DSM

Bado unatokwa jasho tu! lkn husemi wapi Andrew kasema anayaongea hayo kwakuwa yeye ni mwana CCM!? au kwakuwa ni toto wa Nyerere?
Pole sana, lkn ndiyo nchi ilipofikia hakuna ushabiki bila kufikiri, ukiongea pumba watu tutajua tu..na wewe utaishia kusema tunaongea uzushi!!

Think chama, kuwa huru bwana!!
 
Kumbe CDM chama cha upinzani, ambacha hakijawahi kuongoza nchi ndiyo kioo cha kujitizamia cha CCM!!!!
 
Mkuu usikonde huo ndio uhuru wa mawazo si lazima tukubaliane; inaonekana hujamsoma Andrew ndio sababu umejikita kwenye uzushi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
na ushabiki wako huwa unatoka wapi sasa zinapowasilishwa hoja za chama kingine na wewe kushabikia against wakati watambua kuwa hayo pia ni maswala ya vikao kwa chama husika. je hiyo kwako ndio siasa safi na ya Andrew inakuwa ya hovyo?
Mkuu akili yako safi? Jina langu Chama unataka nitumie jina gani za hilo? Mpaka leo hujajua JF ni kiwanda cha uzushi? Andrew ana uhuru wa kutoa mawazo si lazima nikubaliane naye; manayekubaliana naye ni nyie mashabiki wa siasa za uzushi; Andrew kama yeye ni mwanaccm anatakiwa ajue taratibu za chama; kama ana maoni ya kubadilisha utaratibu wa kupata mwenyekiti anatakiwa atumie vikao halali vya chama kupitisha mawazo yake sio kuja kupiga porojo JF. Nina wasiwasi kama kweli Andrew ni mwanachama wa CCM; wanachama tunafahamu utaratibu wa chama chetu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
na ushabiki wako huwa unatoka wapi sasa zinapowasilishwa hoja za chama kingine na wewe kushabikia against wakati watambua kuwa hayo pia ni maswala ya vikao kwa chama husika. je hiyo kwako ndio siasa safi na ya Andrew inakuwa ya hovyo?

Mkuu anza siku kwa kumuomba Mungu; pata kifungua kinywa ndio uingie JF

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kumbe CDM chama cha upinzani, ambacha hakijawahi kuongoza nchi ndiyo kioo cha kujitizamia cha CCM!!!!
Habari za siku mkuu wangu MWM

Naona unaniwekea maneno mdomoni.....Sijasema kwamba CHADEMA ni kioo cha kujitazamia cha CCM, nimejaribu tu kumtaka Lole Gwakisa anijibu maswali hayo ambayo nadhani majibu yakeo yataonesha ni nini kilichopo nyuma ya pazia la siasa za vyama ndani ya Tanzania kuhusiana na kitu kinachoitwa Demokrasia....

CHADEMA kama chama mbadala katika siasa za Tanzania wanapaswa kuja na mambo mapya, wajitofautishe na CCM hasa katika namna ya kuwapata viongozi wao wa kitaifa.......

Btw......Kama wakifanya tofauti na CCM haitakuwa kitu cha ajabu kwa wao konekana ni kioo cha kujitazamia cha CCM...

Kuna member mmoja humu JF anaitwa Belo......Yeye kwenye signature yake kasema 'Kitu pekee ambacho mwanasiasa anaweza kukisemea ukweli ni Jina lake'............ Vingine vyote ni wizi mtupu
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kuwa rais kama siyo kiongozi wa chama. Kiongozi wa chama atakuendesha kama gari bovu

Kwa demokrasia ya Afrika sio?!
Kwa demokrasia ya wenye nayo, hilo linawezekana na mambo yakaenda mswano. Mfano mzuri ni hapo Marekani tu, sidhani hata kama unafahamu viongozi wa Dems na GOP ni kina nani!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom