Uenyekiti CCM: Jakaya Kikwete imetosha!

Status
Not open for further replies.
CCM sio chama cha kifalme kuwa mtoto Nyerere haimaniishi wewe ni kiongozi wa CCM
Utoto wa Nyerere umeuleta wewe hapa, jamaa hajasema lolote kuhusu utoto wa Nyerere wala kwamba yeye ni kiongozi wa CCM kwa vile eti ni mtoto wa Nyerere , acha kubabaikia pedigree ya mleta hoja, nobody is talking about utoto wa Nyerere hapa, get a grip!

Mtu akitoa nasaha zake kwamba Kikwete apumzike hapo zimevunjwa taratibu gani za chama?

Kikwete ameshindwa kuongoza chama, kila siku ni minyukano ya wenyewe kwa wenyewe kwenye press conferences zisizoisha. Mwenyekiti anaambiwa chama kinaelekea pabaya anajibu kwa mipasho, "kwa wale wanaosema chama kinakufa watakufa wao itabaki CCM..." anajibu mipasho utadhani sio Rais. Kwani Nyerere alivyokua anaasa kuhusu mustakabali wa CCM alimaanisha hatakufa kabla hayo anayoasa hayajatokea? Kuna mtu hafi maisha haya? JK please! Shameful irresponsible leader, worst chairman CCM has seen since its founding in 1929.
 
Utoto wa Nyerere umeuleta wewe hapa, jamaa hajasema lolote kuhusu utoto wa Nyerere wala kwamba yeye ni kiongozi wa CCM kwa vile eti ni mtoto wa Nyerere , acha kubabaikia pedigree ya mleta hoja, nobody is talking about utoto wa Nyerere hapa, get a grip!

Mtu akitoa nasaha zake kwamba Kikwete apumzike hapo zimevunjwa taratibu gani za chama?

Kikwete ameshindwa kuongoza chama, kila siku ni minyukano ya wenyewe kwa wenyewe kwenye press conferences zisizoisha. Mwenyekiti anaambiwa chama kinaelekea pabaya anajibu kwa mipasho, "kwa wale wanaosema chama kinakufa watakufa wao itabaki CCM..." anajibu mipasho utadhani sio Rais. Kwani Nyerere alivyokua anaasa kuhusu mustakabali wa CCM alimaanisha hatakufa kabla hayo anayoasa hayajatokea? Kuna mtu hafi maisha haya? JK please! Shameful irresponsible leader, worst chairman CCM has seen since its founding in 1929.

Kamanda haya ya CCM tuachieni wenyewe hayawahusu wewe ni bibi yake Andrew mpaka umjibie?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Habari za siku mkuu wangu MWM

Naona unaniwekea maneno mdomoni.....Sijasema kwamba CHADEMA ni kioo cha kujitazamia cha CCM, nimejaribu tu kumtaka Lole Gwakisa anijibu maswali hayo ambayo nadhani majibu yakeo yataonesha ni nini kilichopo nyuma ya pazia la siasa za vyama ndani ya Tanzania kuhusiana na kitu kinachoitwa Demokrasia....

CHADEMA kama chama mbadala katika siasa za Tanzania wanapaswa kuja na mambo mapya, wajitofautishe na CCM hasa katika namna ya kuwapata viongozi wao wa kitaifa.......


Btw......Kama wakifanya tofauti na CCM haitakuwa kitu cha ajabu kwa wao konekana ni kioo cha kujitazamia cha CCM...

Kuna member mmoja humu JF anaitwa Belo......Yeye kwenye signature yake kasema 'Kitu pekee ambacho mwanasiasa anaweza kukisemea ukweli ni Jina lake'............ Vingine vyote ni wizi mtupu


Nzuri mkuu,

Nimekupata vizuri nadhani..ila huwa natatizika na tabia za baadhi ya wana ccm kushindwa kutolea majibu ya matatizo ya chama chao badala yake huwa wana sema mbona na CDM wako hivyohivyo!!!
Hii huwa inanitia kichefuchefu mno!!

Sasa angalia hapa, Andrew kasema Kikwete apumzike uenyekiti wa CCM kwani kapwaya....tumebadili mada!! tuisaidia nchi kweli?
 
Boss wa Obama ni nani? Mkuu Aweda

Representative Debbie Wasserman Schultz ndie bosi wa Obama. Ndie mwenyekiti wa sasa wa Democratic National Committee (DNC). DNC ndiyo mwangalizi mkuu wa chama.
 
Mkuu usikonde huo ndio uhuru wa mawazo si lazima tukubaliane; inaonekana hujamsoma Andrew ndio sababu umejikita kwenye uzushi

Chama
Gongo la mboto DSM

Haya mkuu!!

Lkn wewe ndiye ulieanza kukataa kutokubaliana na wenzio!! ukawaita wanajifanya watoto wa mfalme!!
 
Hivi Freeman Mbowe alishindana na nani katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA?.....

Nakumbuka Zitto alichukua fomu za kugombea, wazee wakamshauri ajitoe......

Sijui tatizo lilikuwa ni nini hasa....

Two wrongs don't make it right.
Chifu, mfumo wetu wa siasa ni wa hovyo mno.
Pengine katiba mpya italeta unafuu.
 
Last edited by a moderator:
Two wrongs don't make it right.
Chifu, mfumo wetu wa siasa ni wa hovyo mno.
Pengine katiba mpya italeta unafuu.
Uko sahihi mkuu.........Tatizo ni mfumo

Na mbaya zaidi ni kwamba karibu vyama vyote vinafuata mfumo uleule wa CCM, kuanzia structure ya uongozi mpaka Katiba zao......Mpaka aina ya upataji viongozi....Kila kitu ni kilekile.

Bado tuna SAFARI ndefu sana chief........
 
Mkuu akili yako safi? Jina langu Chama unataka nitumie jina gani za hilo? Mpaka leo hujajua JF ni kiwanda cha uzushi? Andrew ana uhuru wa kutoa mawazo si lazima nikubaliane naye; manayekubaliana naye ni nyie mashabiki wa siasa za uzushi; Andrew kama yeye ni mwanaccm anatakiwa ajue taratibu za chama; kama ana maoni ya kubadilisha utaratibu wa kupata mwenyekiti anatakiwa atumie vikao halali vya chama kupitisha mawazo yake sio kuja kupiga porojo JF. Nina wasiwasi kama kweli Andrew ni mwanachama wa CCM; wanachama tunafahamu utaratibu wa chama chetu.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mama kapita bila kupingwa, mtoto kapita bila kupingwa...baba naye apite bila kupingwa!!

Ila on a serious note CHAMA, ninadiriki kusema naamini UNAFIKIRI kwa TUMBO na sio AKILI.
 
Inafaa Ndugu Kikwete apumzike sasa. Amelitumika Taifa kiasi cha kutosha. Kazi aliyofanya ni nzuri, lakini there is nothing to be gained kwa yeye kuendelea kuwa CCM Chairman. Kikwete ni spent force.

Nawasilisha hoja.
hoja yako inajengwa zaidi na hisia na pengine chuki dhidi ya Kikwete kwa sasa ndani ya CCM hakuna kiongozi mwenye busara na hekima kama yeye, na si kwa maslahi ya chama kwa sasa kuweka mwenyekiti mwengine wakati chama kikielekea uchaguzi 2015,
haya ni makelele ya wapinzani kujaribu ku influence maamuzi ndani ya CCM, kama njia ya kuidhofisha CCM lakini nadhani wenyewe watangamua.
Kikwete ana hitajiwa sasa hivi ambapo ndani ya chama kuna makundi kila moja yanataka kundi lake litoe mgombea urais.Ni kikwete pekee ambae anaweza kuliongoza jahazi la ccm kupata mgombea makini.
wat
asema lakini kikwete ni kiongozi aliekaa ndani ya chama tangu ngazi ya chini kabisa kwa muda mrefu na amefanya kazi na wenyeviti wote wa ccm , ana uzoefu mkumbwa wauongozi katika ngazi za chama na katika kuongoza chama.
wana chama wamekua walikosoa mara kwa mara shughuli za chama na yeye amekua mvumilivu wa hali ya juu
hakuna mwenyekiti yoyote aliyemtangulia ambaye ameruhusu kukosoa CCM, ILA Alifukuzwa ama alinyimwa nafasi za ubunge kama nja za kuwakomoa na kunyamazisha..lakini haya si wakati wa kikwete CCM imekua na democracy ya hali ya juu, wabunge wake wamekua wazi bila ya kuingiliwa na chama kuhoji serikali yao
haya ndugu yangu hayakustahamiliwa na wenyeviti walopita..wote walikua wabaabe na maamuzi yao yalikua ya nguvu zaidi
kikwete ndie nguzo muhimu kisha wa ccm sasa hivi...ila mara baada ya uchaguzi anaweza kuit
isha mkutano mwengine wa dharura kumpatia rais ajae uenyekiti wa chama
hakuna kama yeye
 
Mwenyekiti JK anaanza kuzungumza, lakini yupo ktk tansion kubwa. Nadhani leo atalipua mambo makali sana.
 
Uko sahihi mkuu.........Tatizo ni mfumo

Na mbaya zaidi ni kwamba karibu vyama vyote vinafuata mfumo uleule wa CCM, kuanzia structure ya uongozi mpaka Katiba zao......Mpaka aina ya upataji viongozi....Kila kitu ni kilekile.

Bado tuna SAFARI ndefu sana chief........

Safari bado ni ndefu haswaa.

Lakini on a serious note chifu, safari inakuwa ndefu zaidi ni uwepo wa CCM madarakani.
Nimesikitishwa sana na ufujaji wa mali za dola kwa manufaa ya chama. Hili suala limekuwa kama ni jambo la kawaida kabisa.

Juzi Nape kasema wapinzani wajifunze kutoka uchaguzi wa Marekani. Ila anasahau kwamba kule, huwezi kuona wala kusikia Obama, Hillary au wana Dems wowote walio serikalini, wakitumia mali za dola kwenye shughuli za chama!!!
 
CCM is still being judged by its outer colour by many of our people, I can see. rangi yake ya kijani na manjano kwaya za kina Komba, maigizo ya kina Masnja, mikwara yake, propaganda.. Uzuri wa mkakasi...
 
Kamanda haya ya CCM tuachieni wenyewe hayawahusu wewe ni bibi yake Andrew mpaka ujiibie
wewe ndio uliyechangia kama unataka kuolewa na jamaa, watu wanajadili hoja husika wewe unaleta za utoto wa Nyerere, nani alikuwa anajadili utoto wa Nyerere hapa? Acha kuchemka we zealot unaezinguka na pedigree za watu, utapelekwa pwani wewe.
 
Mkuu usikonde huo ndio uhuru wa mawazo si lazima tukubaliane; inaonekana hujamsoma Andrew ndio sababu umejikita kwenye uzushi

Chama
Gongo la mboto DSM
Wacha siasa za maji taka wewe, unaonekana ni mchumia tumbo tu, ndio maana unaogopa changamoto za Andrew!
Sio siri, huu mfumo wa Rais kuwa Mwenyekiti wa Chama ni hovyo kabisa! Raisi anakosa mahala pa kuwajibika, anavurunda kotekote.
 
Kwa demokrasia ya Afrika sio?!
Kwa demokrasia ya wenye nayo, hilo linawezekana na mambo yakaenda mswano. Mfano mzuri ni hapo Marekani tu, sidhani hata kama unafahamu viongozi wa Dems na GOP ni kina nani!!

Nipe darasa mkuu
 
Ndugu mwenyekiti, nimefarijika sana kwa maneno yako ya busara. Nimefurahi kusikia kwamba wewe mwenyekiti umegundua kwamba kuna nyoka ndani ya jumba letu. Sasa tujiulize huyu nyoka amengiaje kwenye jumba letu na tunawezaje kumuondoa? Ndugu mwenyekiti, huyu nyoka, tulimgundua mwaka na zaidi uliopita. Tuliamua kumuangamiza, lakini matokeo yake tukamuonea huruma na kumuacha na gamba lake. Huyu nyoka matokeo yake kazaa, na watoto aliowazaa ni hatari zaidi. Hata tukimuua, haitatusaidia,, kama ni kumuua, itabidi tumuue yeye pamoja na watoto wake ambao wamekuwa ni hatari zaidi ya mama yao. Huyu nyoka yukoje?



  1. Nyoka tuliyetaka kumvua gamba alikuwa ni ufisadi. Ufisadi umeshamiri ndani ya chama chetu. Mwagwiji wa Ufisadi tumewaonea huruma na aibu huku wakiwa wanajipanga. Hawa nyoka wa ufisadi wameshazaa na nguvu zao zinatisha. Wamezaa watoto wao ambao ni hatazi yaidi ya mama yao. Mh. Mwenyekiti, huyu nyoka hatuwezi kumvua gamba. Tukijaribu au wewe mwenyewe ukijaribu, watakumaliza. Watakung’ata
  2. Nyoka wetu mwenye gamba amemzaaBernad Membe;- aliyekuchonganisha na Lowassa akihofia mustakabali wake ktk nafasi ya uraisi. Alilamba mabilioni ya Ghadafi, mpaka na leo hajanyoosha maelezo. Alikunanga pindi makamanda wa M4C walipotia nanga Jimbo kwake, ikumbukwe alidai hajawahii ona raisi kilaza kama JK. Huyu Nyoka mwenye gamba amemzaa Fisafi Hatari Nyalandu;- Mwizi wa nyara za taifa, kumbuka dili la meno ya tembo, mbakaji, kumbuka scandal yake iliyotokea USA, hana uzalendo kumbuka alivyowasaidia vijana wa kitanzania kuingia marekani kwa gia ya Summer camp, huku akijua wazi analinyima taifa nguvu kazi yake. Mtoa rushwa mahiri, kumbuka UVCCM Dodoma
  3. Huyu nyoka mwenye gamba amemzaa Ridhiwani Kikwete, kiongozi wa Majungu na makundi. Anavuruga kila kitu. Ameleta mnyukano mkubwa sana ndani na nje ya chama. Ameiingilia hadi vilabu vya mipira. Ridhiwani ni hatari kwa kueneza Rushwa. Bila kukuficha, huyu nyoka ridhiwani ni hatari kuliko kila nyoka mwingine ndani ya Chama Chetu. Ridhiwani ni hatari siyo tu kw auongozi wako, bali kwa taifa zima. Makundi ndani ya Chama au tofauti kubwa zinazoonekana waziwazi, zimeasisiwa na Mwanao Ridhiwani.
  4. Ndugu Mwenyekiti, nadhani mara nyingi kutafuta chimbuko la tatizo ni vizuri zaidi kuliko kujaribu kutatua tatizo kwa juu juu. Mzizi wa fitina, majungu, rushwa, mgawanyiko, makundi, ufisadi, uongozi dhaifu, UDINI, ukabila ni wewe. Kumbuka umekuwa ukitoa nafasi za kazi kwa upendeleo. Kumbuka umefumbia mambo mambo ya kifisadi. Kumbuka umekuwa ukimtumia Zitto, Membe na Ridhiwani kuleta mafarakano ndani na nje ya chama chetu kutumia udini na ukabila. Haya tunayajua kwa sababu baadhi ya vikao tumehudhuria
  5. Ukimya wako kukemea rushwa, kutokumkema mwanao Ridhiwani kuwa kinara wa kugawa rushwa na kuchafua kampeni kumewanyima vijana uwezo nafasi za uongozi ndani ya chama. Mh. Mwenyekiti, nyoka anayekumaliza ni Yule nyoka uliyemlea January Makamba ambaye anajua siri zako nyingi. Sisi kama wandani ndani ya Chama, tunajua jinsi huyu nyoka anavyokutafuna kisiri. Ili kukiokoa Chama ni vyema tukaanza na kuungoa Mzizi. Na mzizi ni wewe Ndugu mwenyekiti. Kwa kipindi kirefu, huyu nyoka mtoto alikuwa ikulu kikazi Zaidi. Usichezee Chama fanya Ustaarabu ukiokoe Chama. Uongozi nikupokezana vijiti. Yule Nyoka mwenye Gamba ameshazaa na watoto wake ni wakali zaidi unavyofikiria
  6. Ukiwa na nia njema na chama, basi ng'atuka. vinginevyo utatolewa kwa aibu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom