Uelewa wa baadhi ya wabunge kuhusu utawala wa sheria unatia shaka

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Mtu akizifanyia tathmini hoja ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali, zinazotetea uhalali wa ulipaji posho za vikao kwa wabunge, inaonekana wazi ama watu hao ni wanafiki wa kupindukia au ni bumbumbu wa utawala wa sheria.

Nasema hivyo kwasababu hii hoja yao ya kusema kwamba posho hizo zinalipwa kwa mujibu wa sheria na kanuni haina mshiko; kwani kama kuna sheria yeyote inayo halalisha wizi, sheria hiyo ni batili.

Ni kweli katika miaka ya hivi karibuni nchi yetu imeshuhudia vitendo vingi vya matumizi mabaya ya madaraka ambapo viongozi waliopewa dhamana ya kulinda rasilimali za taifa kula njama za kujigawia wao wenyewe hizo rasilimali walizokabidhiwa kuzihifadhi.

Hii ndiyo iliyotokea kwa nyumba za serikali na kiwanda cha Kiwira, ingawaje uporaji huo umenyika chini ya mgongo wa sheria bado ukweli unabakia pale pale ya kuwa ni wizi. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa hii posho ya vikao wanayolipwa wabunge, kwakuwa inasababisha mbunge alipwe mara mbili kwa kazi ile ile.
 
Back
Top Bottom