Udom kuna mambo, ndio maana wanaosema Ukipata first class UDOM ujue UDSM ungedisco mwaka wa pili hawajakosea. Hebu angalia mambo yaliyopo UDOM:-
Usipofanya Assignment au Test, Lecturer anahaha kukutafuta ili ufanye tena mtihani au akuandikie zero na siyo Incomplete. Yaani sheria ya incomplete UDOM ni kama kivuli tu hakuna lecturer anayejiamini kumwandikia mwanafunzi INC.
Mkifanya Assignment au Test mkafeli wengi, basi lecturer anafuta matokeo yote na kuwapa maksi 10 kila mtu za bure.
Kuna masomo yanafundishwa na walimu vilaza sijapata kuona katika historia ya vyuo vikuu mpaka najiuliza hivi interview za walimu wa UDOM zinafanywa na nani? au ni secretarieti ya ajira? maana kama zinahusisha na maakademishani hakyamungu huwezi ukawa na walimu wa sample za UDOM, Sio wote ila ni baadhi na wengi wao ni wa Dini ile inayolalamikiwa sana kuwa ndiyo kigezo cha kuajiriwa UDOM. Anyway bado nipo kwenye utafiti wa hili swala ila nikimaliza nitawataja kwa majina ili mwenye taarifa zao atusaidie.
Kuna wanafunzi wanamaliza UDOM ukiangalia uwezo wao unashindwa hata kuelewa walipitaje semester ya I kuingia ya II, ni mambulumundu squared. Jamani uongozi wa UDOM habu kuweni serious, mtatuharibia na wengine ambao tuna uwezo wetu binafsi. Vyeti vyetu vitawekwa kapuni kwa kuhisiwa ni walewale.