UDSM yatengeneza nyungu ya kidijitali, fukiza bila majani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
1594202642149.png

CHUO kikuu cha Dar es Salaam chatengeneza dawa ya kujifukiza (Nyungu) ambayo imetengenezwa kwa mfumo wa kisasa zaidi ambapo hutumii majani ya miti lakini unatumia mafuta tete.

Akizungumza na Michuzi Blog Meneja mradi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Stephan Nyandoro amesema kuwa dawa ya kujifukiza ijulikanayo kama Fukiza 'Udanol' imetengenezwa kwa miti mbalimbali yenye kutoa mafuta ambayo yanasaidia kuzibua mfumo wa upumuaji ulioziba.

Akizungumza katika banda la chuo kikuu cha Dar es Salaam lililopo katika Maonesho ya Saba saba jijini Dar es Salaam amesema kuwa watanzania wawe na imani na dawa zinazotengenezwa kwa miti shamba hapa nchini kwani zinatibu.

"Dawa hii imetoka na mimea ambayo jamii yetu imekuwa ikitumia kwa kujifukiza kwaajili ya kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yanayoshambulia mfumo wa upumuaji, sasa sisi tumeona watu wanatumia majani na magome kwaajili ya kujifukiza sasa chuo chetu tukaona tutafute mbadala ambao utasaidia kupambana na ugonjwa huu wa Corona."

"Tumetengeneza ikiwa nisehemu ya mchanganyiko wa mafuta tete, ambayo ni mepesi na hayana uzito wa mafuta ya kupikia, mafuta haya yanapeperushwa kwenye hewa na ukichemsha maji yanaondoka kiurahisi.

Amesema kuwa unapoyatumia kwa kujifukiza kwa kutumia mimea mafuta tete yanayosaidia katika kutibu maradhi mbalimbali.

Amesema mafuta hayo ukitaka kutumia unachemsha maji lita moja na kuweka matone mawili au matatu tuu ndipo unaanza kujifukiza.

Licha ya hivyo Nyandoro amesema kuwa unaweza kujifukiza kwa dakika tano hadi 10. Pia amesema mbadaka wa dawa hiyo ya kujifukiza unaweza kutumia kwenye chai kwa kuweka tone moja la dawa hiyo ya Udanol.

Chanzo: MICHUZI BLOG
 
Ukiwauliza working mechanism au pharmacology, watakwambia huthamini vumbuzi za nyumbani. Watafiti wabobezi wananyofolewa kila kukicha, wanapelekwa likizo kwenye nafasi za kisiasa, ambazo ukimpa ndugu yangu Msukuma na darasa lake la 7 au Munde na darasa lake la 6 watazifanya.
Utafiti mmefanyia wapi na lini?
 
Wanapoanza kufanya tafiti zao na wanapomaliza huwa ni lazima wakujulishe?
Sio lazima wanijulishe lakini kama wanajinadi na kujinasibu kuwa wasomi isn't it obvious waseme kuhusu utafiti wao?

Swali la msingi labda pengine ulitakiwa uulize kama TBS wame-approve
TDMA does, TBS does not. Lakini kupata tu muhuri wa TDMA is irrelevant IMO, based nilichoongea hapo juu!
 
Huo ni utafiti ama ugunduzi?
Kwa elimu yangu ndogo ninaelewa kuwa utafiti (research) ina methodology ndefu kidogo sasa hiyo imekuwa vipi kwa muda huu mfupi tayari imeshatoa results na kujua aina ya matumizi, nani inamfaa na nani haimfai kutumia, muda wa matumizi, dosage, efficiency and effectiveness n.k.
 
CHUO kikuu cha Dar es Salaam chatengeneza dawa ya kujifukiza (Nyungu) ambayo imetengenezwa kwa mfumo wa kisasa zaidi ambapo hutumii majani ya miti lakini unatumia mafuta tete.

Akizungumza na Michuzi Blog Meneja mradi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Stephan Nyandoro amesema kuwa dawa ya kujifukiza ijulikanayo kama Fukiza 'Udanol' imetengenezwa kwa miti mbalimbali yenye kutoa mafuta ambayo yanasaidia kuzibua mfumo wa upumuaji ulioziba.

Akizungumza katika banda la chuo kikuu cha Dar es Salaam lililopo katika Maonesho ya Saba saba jijini Dar es Salaam amesema kuwa watanzania wawe na imani na dawa zinazotengenezwa kwa miti shamba hapa nchini kwani zinatibu.

"Dawa hii imetoka na mimea ambayo jamii yetu imekuwa ikitumia kwa kujifukiza kwaajili ya kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yanayoshambulia mfumo wa upumuaji, sasa sisi tumeona watu wanatumia majani na magome kwaajili ya kujifukiza sasa chuo chetu tukaona tutafute mbadala ambao utasaidia kupambana na ugonjwa huu wa Corona."

"Tumetengeneza ikiwa nisehemu ya mchanganyiko wa mafuta tete, ambayo ni mepesi na hayana uzito wa mafuta ya kupikia, mafuta haya yanapeperushwa kwenye hewa na ukichemsha maji yanaondoka kiurahisi.

Amesema kuwa unapoyatumia kwa kujifukiza kwa kutumia mimea mafuta tete yanayosaidia katika kutibu maradhi mbalimbali.

Amesema mafuta hayo ukitaka kutumia unachemsha maji lita moja na kuweka matone mawili au matatu tuu ndipo unaanza kujifukiza.

Licha ya hivyo Nyandoro amesema kuwa unaweza kujifukiza kwa dakika tano hadi 10. Pia amesema mbadaka wa dawa hiyo ya kujifukiza unaweza kutumia kwenye chai kwa kuweka tone moja la dawa hiyo ya Udanol.

Chanzo: MICHUZI BLOG
Sawa tutazitumia,tunahitaji tupone, na kwa hili gonjwa wacha tu tupambane kivyetu...
 
Huu sio uvumbuzi. Hii ni kucopy na kupaste maana hii dwa ilikuwepo hata kabla ya corona.
 
Wanastahili pongezi maana miti shamba ndiyo inataengeneza madawa lakini tuekuwa hatutumia elimu zetu kutengeneza madawa kwa kutumia miti shamba yetu ambayo imajaa kila mahala
 
Back
Top Bottom