UDSM yapandisha ADA 100% kwa Masters 2013

Brother Kaka

Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
90
Reaction score
55
Wadau inasikitisha sana kwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)kupandisha ada ghafla kwa masters 2013. Mpaka watu wanatuma maombi ada iliyotangazwa ilikuwa Tsh 3,700,000/-kwa College of Arts and Social Sciences (CASS). Mabadiliko yanaonekana katika Admission letter ambapo ADA imepanda hadi Tsh 6,375,000/-

Note:
Mabadiliko haya ya ADA yameonekana tu katika admission letter.Mchakato wa kutagaza nafasi walionesha ADA za awali
 
Sasa tufanyaje wacha wa pandishe tu ccm kidumu wote tuseme oyee
 
Sasa tufanyaje wacha wa pandishe tu ccm kidumu wote tuseme oyee
 
Nakushauri uende pale chuoni directorate of postgraduate studies utapewa brochure ya fee structure. Acha kulalamika bila kuwa na uhakika. Mimi nilipita kwenye banda lao sabasaba hakuna chuo chenye ada nafuu hapa tanzania kama UDSM. Kozi ghali zaidi ni Masters of International Trade na Masters International Business.

Nashauri tuache kufikiria kisiasa, tuache kufikirishwa. Nashangaa eti CCM inatajwa kwenye swala la ada vyuoni, sijui inahusikaje! Au chama chake ndiyo kitakua na uwezo wa kupangia vyuo ada! Mhhhh kweli hiki chama kibovu kinapotosha umma. Nathani ni bora mjitahidi muingie madarakani ili elimu iwe bure hadi vyuo vikiuu.
 

Mabulangati
Nazungumza kitu nikiwa na ushahidi kwa 100% baada ya kuona admission letter kwa mtu aliyeomba MPA mwaka huu 2013.Mabadiliko haya yamejitokeza ktk barua hizo lakini mchakato wa kutoa matangazo mpaka watu kuomba walionesha ADA za zamani.Tafuta mtu aliyepata admission utaona haya mabadiliko mkuu
 
Last edited by a moderator:

International business na International Trade fee zake ni kiasu gani?
 
UDBS, kwa MBA hiyo ada ya 6m imekaa kwa muda mrefu sana na wanafikiria kuipandisha. Ni muda muafaka na huko CASS ipandishwe. BTW milion sita kwa Masterz ni hela ndogo sana. Watoto wetu primary tunawalipia hiyo 6m na zaidi, kwanini kwa masters ishindikane?
 
Mtu aliyezoea kusoma bure utawajua tu. Iyo mbona bei rahisi sana kwa watu ambao tulionyimwa mkopo. Tunasoma kwa kuunga ni bei simpo kama ukijimeki ila me nilienada kwenye banda lao pale sabasaba nikapewa maelezo mazuri tu juu ya uliipaji wa ada kwa watu wa master na form nikanunua sh elf hamsini kama unaona gharam nenda open bei rahis sh mil 3.5. Kwa miez 18 aumiaka 2
 
Hii ada mpya hata kwa wanafunzi wa master wanaoendelea?
 

Mabulangati ni kweli ada imepanda mdau,unaongelea habar za kwenye banda wakat mwenzio anaongelea admission letter,binafsi nimepewa barua ya admission ikiwa na mchanganuo wa ada mpya,ni kweli ada ni Tsh 6,375,000/= kwa CASS,CoET,CoNAS,CoICT,IDS,IMS,IRA,UDSoL na UDBS,
Ila SJMC ni tsh 5,250,000 na UDSE pamoja na IKS wao ni 4,875,000/= na hiyo ada ni kwa kozi za miez 18 tu,miez 24 wana ada yao pia.
 
Last edited by a moderator:
Hii ada mpya hata kwa wanafunzi wa master wanaoendelea?

hapana,udsm huwa wana utaratibu mzuri,kama ulishaanza kwa dada fulani,basi inapopanda huwa haikuhusu wewe,inawahusu wanaoanza,
ingawa ada wameongeza si kubwa sana ila ndo hali za kiuchumi tulizonazo,ada ya mil 6 si nyingi kwakweli,maana ada hiyo ndo mtoto wa feza analipa,tatizo linakuja hali za maisha tu,maana ulaya kusoma ni zaid ya milion 10
 

TARIMO WA ROMBO ada imepanda kweli,tofauti na hiyo uloambiwa kwenye banda lao,na application form ni elf 20 na si elf 50,binafsi naona udsm ndo chuo kinachotoza bei ya chini ya form ya maombi ya kujiunga,,,na pia ukiwapiga sound unaanza hata kwa 1.5 mil,
hope umenipata mzee wa MASHATI ROMBO
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…