UDSM website | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDSM website

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Belo, Jan 25, 2009.

 1. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,262
  Likes Received: 4,236
  Trophy Points: 280
  Nimeona UDSM hatimaye wamesikia kilio chetu na sasa wamefanya mabadiliko makubwa kwenye website yao
  visit
  UDSM - Home
   
 2. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tangia Juzi wamebadilisha lakini jinsi display ya matangazo (announcement) mimi sijaipenda maana unatakiwa usubili zaidi ili matangazo yote yapite, namanisha kwamba kama unataka tangazo waliloweka tarehe x iliyopita then unatakiwa tarehe a, b ,c, ....w zipite (one after another) ndio upate hilo tangazo x. Timw consuming
  All in all, nawapa big-up kwa mabadiliko. Tunasubiri Mkwawa, DUCE tayari
   
 3. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hiyo ya awali ilikuwa na tatizo gani? Nataka nijue tu, maybe kuna vitu vyenye manufaa nitajifunza.
   
 4. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Website haiko current. Bado official statements zinafagilia DARUSO wakati wameshaifuta!

  Halafu list ya "Batch of Re-admitted Students" imekusanywakusanywa kiholela, hakuna cha alphabetical order au cha numerical order ya student number, kwa maana kwamba kama imebandikwa ukutani ukitafuta jina la mtu inabidi usome listi yote jina moja moja. Hivi Microsoft Excell huwezi kuiambia ikupangie listi ya majina alphabetically?

  Kwenye photo gallery kuna album ina picha moja ya May, 2006. Toka mwaka 2006 ki-social event kimoja cha kuogelea!

  Halafu sehemu muhimu kuliko zote katika tovuti ya chuo chochote kile - prospective students/admissions - ina link ambayo inafungua blank page!
   
 5. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  heheh,Ila jamani tumekuwa watu wa kukosoa sana,kama wewe unajiamini kaa chini toka na Sample yako the uwapelekee mlimani uone kama wataikataa,nimewahi kufanya hivi kwenye website moja tena ni nyeti katika Database yao wakaniappreciate.
  Nini napenda kusema ni kuwa tuwe tunatoa kasoro pamoja na kuja na suluhisho kwani sisi Watanzania ni watu wa kuongea mno,maneno matupu hayajengi wakuu,By the way sisi katika IT huwa tunaongea kwa vitendo,Yangu machache.
   
 6. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kilongwe, suluhisho la yaliyosemwa hapo juu yamo humo humo, na wala hayahitaji dissertational mapendekezo kuyang'amua.

  Nimesema link ya "prospective students" iko blank. Pendekezo haliko wazi hapo?: fill the blank pages! Weka information za qualifications na jinsi ya ku apply. Simple as that!

  Nikasema tovuti bado ina official statements zinafagilia DARUSO wakati wameshaifuta. Pendekezo: acha kufagilio DARUSO wakati mmeshaifuta!!! What is so conceptually hard hapo? Chombo cha wanafunzi kimefutwa in a high profile, controversial, circus. Halafu bado unapotosha jamii kana kwamba bado kipo?

  Li-website limerundika majina ya re-admitted students bila hata kuyaorodhesha katika namna ambayo itakuwa rahisi mtu kutafuta jina lake kama yakiwa yamebandikwa ukutani. Hapa napo huhitaji thesis ya mapendekezo, lakini kama yanahitajika nilishasema cha kufanya: panga majina na Microsoft Excell!!!!!

  Maana I am guessing bado wana mchezo wa kubandika majina ukutani. Hawana nia ya kumtumia kila mtu barua au hata e-mail ndio maana wanawabandika kwenye mu-website. Hakuna cha privacy kwenye jamii yetu. Yale yale ya darasa la saba kubandika matokeo ukutani, kila mtu mjini anaona listi...Kuhani kafeli! Duu! Halafu wanakijiji wanakuja kukupoza eti hukufeli ila tu hukuchaguliwa. Hukuchaguliwa my foot, kwani tulichezeshwa sandakalawe huko Baraza la Mitihani?
   
 7. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,262
  Likes Received: 4,236
  Trophy Points: 280
  Kuna kasoro nyingi lakini tovuti yenyewe hata wiki haijafikisha naamini bado wanaendelea kuweka information nyingine
   
Loading...