wewe sisi watu wa UD tuko active sana humu JF.
sema tu shida hatujiandiki kuwa ni watu wa ud
Ninapenda kupitia hapa niweze kuzungumzia mtafaruku uliopo Chuo kikuu cha DSM. Mkuu wa chuo Prof Mkandara aliwasimamisha wanafunzi 25 hapo chuo akiwemwo waziri mkuu na mpaka sasa wanafunzi wote wapo kimya na hakuna kinachoendelea kudai kurudishwa kwa wanafunzi wenzao... NINI SASA sio kwamba wanafunzi wako kimya bali ni hila na jinsi mkuu alivyoamua kutumia UBABE NA NDIKTETA kuzuia any movement ambayo inaweza kuwarudisha pale chuo.
Ikumbukwe kwamba mkuu huyo yupo pale kisiasa na siyo kivingine na anapoaana matakwa ya chama chake hayafanikiwi anatumia njia mbadala za kuumiza umma wa chuo.
KWANINI NATUMIA JF: nia makusudi yangu kwamba tukitoa sauti ya nguvu kuwasaidia wanafunzi waliosimamishwa chuo eti kwa kuhatarisha amani ya chuo wanaweza kurudi.
Wanafunzi hapa leo walitaka kuanzia mgomo lakini kuna kina hali yawao kushindwa kwa maana kila mtu anayeonekana kuleta move anaitwa na Mgaya(PRof) anampiga biti na kumtukana tena kumwambia atamfunga.
Inaniuma sana pia nikifikiria Uongozi wa chuo unahaonga hata waandishi wahabari ili wasitoe sauti yao
Tupo Chuo kujifunza jinsi ya kutetetea maisha ya watanzania ambao wengi ni masikini tunaomba mtuunge mkono kwani bila msaada wenu hatutaweza...
Mwnakijiji, Invisible na wote wale nyie ni wanaharakati na mnajua nini maana ya haya yote tupeni sapoti ili tuweza kukikomboa chuo chetu then kiweze kuitetea nchi.
Tunamkumbuka Chachage ambaye alikuwa mtetezi wa wanafunzi Siyo hawa kina SHIVJi wanaomuenzi Nyerere bila kufuata yale yote aliyoyataka.
REVOLUTION FOR CHANGES
Kwa hakika hakuna anayejua haswa Tatizo kuu ni nini haswa lakini kuanzia saa 4 asubuhi yaleo wakati wanafunzi hawa walipoanza tena maandamano yao kutokea UDASA wakapitia Yombo na kwenda utawala wameonekana wanabeba mabango ya kumtaka Mkuu wa Chuo ajiuzuri ndio bango la mbele kabisa lilikuwa linasema hivyo .
Upande mwingine ni kuhusu kile kilichotokea jana ambapo inasemekana bomu la machozi lilirushwa katika Mgahawa wa chakula kukatokea kifo cha mwanamama mmoja aliyekuwa mjazito pamoja na mtoto wake tumboni , pia kuna mwanafunzi mwingine naye alifariki katika vurugu hizo hiyo jana .
Kwahiyo leo asubuhi watu wameamka na mengine haswa kuhusu vifo vya watu hao , ila idadi kubwa ya wanafunzi haitoi ushirikiano kwa kikundi hicho cha wanafunzi wanaoendesha huo mgomo katika maeneo kadhaa nilipopita wanafunzi wengi wanaoongea na vyombo vya habari nao wanawashangaa wenzao tazama Channel Ten leo usiku utaona maoni ya wanafunzi waliohojiwa pale Hall 5 .
Wengine wanasema hawataka kuingiliwa uchaguzi wao , kama unajua uongozi wa chuo umemsimamisha mmoja wa wanafunzi aliyekuwa mgombea tokea nchini uganda , huyu mwanafunzi anapendwa sana hapa chuoni na yeye alitoa upinzani mkubwa sana kwa wanafunzi wengine wanaogombea sasa hapo kuja jambo
Mwisho kabisa mmoja wa wagombea uraisi hawa kwa jina nahifadhi yeye anaishi Msewe , huyu ni ndugu wa mmoja wa maprof hapa chuoni , sasa sijui yeye pia anahusika nini na kuingiliwa uchaguzi huu wa chuo .
Naishia hapa lakini wanafunzi wana mashaka kweli kweli haswa hawa wa mwaka wa mwisho wengine wanafikiria kuhusu maisha yao ya baadaye kwanini wasiachiwe wamalize mambo yao wakaendelee na maisha yao ?
MCHANA MWEMA
jamani wakuu, tatizo ni kwamba hawa vijana siku hizi ujuaji mwingi, boom linawasumbua na kwa kuwa wengi ni familia zetu, matokeo huwa ni kununua televisheni na music systems, na aghalabu computer ambazo matumizi makubwa huishia kwenye music na pichachafu...semester ikienda mwisho lazima watafute sababu ili chuo kifungwe...mbona hawajagoma barabara ya Sam Nujoma ikamilike? au hatuwasikii hata wakitoa press release kukemea maovu mbalimbali ya serikali? msaada wangu kwao; wajitambue, kisha wawe reasonable, si kila kitu mgomo..after all, wenzao wamesimamishwa na hawajafukuzwa! tunakubali serikali na menejimenti ni vimeo, lakini wasomi onyesheni busara na upeo!!!
Hawa vijana inabidi wapate ujumbe kamili na waambiwe ukweli hata kama utakuwa mchungu kama Kwinini. Mimi sioni kama ni dawa kuwa tunatetea kila kitu eti tu kwa sababu wanavutana na viongozi wa serikali ambayo hatuipendi. Hawa vijana wa sasa wameshindwa kujiwekea mazingira ya kuheshimika.Siku zote ukijiwekea mazingira ya kuheshimika, misimamo isiyoyumba,ukawa na hoja zenye nguvu zinazosimama zenyewe, kutamfanya mtu yeyeote afikirie mara mbili kabla ya ku-interfare mambo yako. Kama hatutawaambia sasa na kubaki kuwatetea tu,hawatojirekebisha.Ni vizuri wakaelewa pia kuwa UDSM sio form V au VI
Habari nilizobnazo,ni kwamba kama khali hii ikiendela mpaka leo saa sita ya mchana basi Makamau mkuu wa chuo atafunga chuo hicho,Jana jioni nilitembelea udasa kuongea na walimu ambao ni rafiki zangu na wako pale Mlimani,
wanashangaa jambo ambalo hawa vijana wanalogomea,wangomea bila kuwa na sababu,watu wamefanya kosa ambalo linapingana na student bylaws,eti wanataka waache kisa wao wanataka,
tunajenga taifa gani lisilofuata shera??lazima watu wajue uhuru wao unaishia wapi na sheria ziwe zinafuatwa tangu wakiwa vijana wadogo.
Nawashauri wadogo zangu,ngudu zangu vijana wa Chuo Cha Mlimani ,Mdogo wangu Daudi Deo..hakikisheni mnalinda Heshima yenu na pia muwe na nidhamu kwa kufuata sheria za Chuo,na ninavyomfahamu mkandara(prof.) ni mtu muungwa na mpenda haki toka yuko pale FASS.
kama ulipata opportunity kusoma Mlimani utaelewa dhahiri kwamba elimu yetu ya juu ni zaidi ya duni. Yaani is somewhere between hell and devel deepsea. Haina chochote zaidi ya mchakato wa kukram na kusolve maswali magumu. Walimu ni wazee wasio taka kurefresh their idea with new world.
Try developed country and you will see the difference.
wewe sisi watu wa UD tuko active sana humu JF.
sema tu shida hatujiandiki kuwa ni watu wa ud
What was the aim ya kugoma? Nini kilikuwa kiini? Let not look at the top, let focus on each corner.
Kama hawakuwa na kibali cha kuandamana then kwa nini waliandamana? Na kwa nini walikwenda kutoa wanafunzi walio madarasani? Mnapochaguliwa mlimani kila mtu anapata jina lake kwa wakati wake, sasa kwa nini mtu asiyetaka kugoma afanyiwe fujo?
Hawa watoto are out of touch, far away from reality.
sasa kama hamjiandiki tutafahamu vipi??
anyway ni bora mmekuja hapa leo?hii inaonesha ni kwamba mko tayari kujadili masuala yenu binafsi na kuacha kujadili mambo yanayohusu taifa hapa katika JF,na nadhani mijadara kama ile iliyokuwa inaandaliwa na DUPSA itakuwa haipo coz tabia hizi mnazozionesha ni kwamba mmekosa ustaraabu na chuo kwa sasa kimejaa wanafunzi msio na subira na wenye jazba zaidi ya yote msiopenda majadiliano
siku zote kama unataka kmaliza jambo lazima kuwe na majadiliano yaliyo mauzri ili kuleta mafanikio hapo mbeleni,Jana mlipewa ushauri wa Bure nendeni kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa akwasiaidie.
,endeleeni kujiandikisha tutakate ushi,embu tuambie nini kinachowafanya wagome??na leo nasikia mnandelea tena,
Kweli thinkpad,
vijana wa UD mpo na mnawakilisha nchi yetu vizuri sana, Hao wengine ni chuki zao tu na dharau ila baadhi yetu tuko very proud of you guys kwa vile mnasomea kwenye mazingira magumu lakini mnapata elimu ya nguvu hapo mlimani.
Wanafunzi wa UD ambao wako wengi sana hapa tena wengine wakiwa membaz machachari hapa JF hawana sababu ya kujitambulisha kama vile wewe na wenzako hamjajitambulisha kuwa ni nani na mnafanya nini huko ccm.
Katika hili la kwenda kwa mwenyekiti wa mkoa wa ccm linaoenyesha jinsi gani wewe na dikiteta na fisadi mkandara mnavyoweka siasa kwenye hii issue.
wanafunzi wa UDSM hawana hoja yoyote ya msingi hadi kufikia kuomba msaada hapa JF. wanachokihitaji ni kufanya vurugu na kuharibu mali na kuhatarisha maisha ya watu kwa kurusha mawe. sidhani kama suluhu ya 'matatizo yao' wanayodai itafikia kwa kufanya hivyo.