UDSM transcript zimekuwa biashara

Mponjoli

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
668
152
Wadau naomba kuwasilisha mada yangu ijadiliwe hapa JF na pia watu watoe maoni ni namna gani tutakomesha hili suala.

Kuna mtundo umezuka pale UDSM kwenye ofisi inayohusika na utoaji wa transcript na vyetu kwa wahitimu. Mara nyingi unapoomba kupatiwa transcript yako inachukua muda mrefu sana kuhudumiwa.

Kimsingi, inatakiwa ichukue maximum of 7 days kupata transcript yako,lakini kinyume na hapo, pale jamaa wako in
efficient sana na inachukua zaidi ya mwezi kupata transcript yako.

Hivi karibuni umejitokeza mtindo wa kudai choochote ili transcript yako iwahi kutoka. Kuna watumishi pale ukiwapa pesa kidogo unapewa transcript yako baada ya siku moja.

Kinachoshangaza kwa sasa wanaprocess transcript za mwezi December wakati ilitakiwa mtu aliyefanya application last week apate transcript this week.

Kibaya zaidi ni kuwa,kuna watu wanatoa chochote na wanachukua transcript after one week.

UDSM tumesoma kwa shida sana lakini hata vyeti vyetu kuchukua inakuwa shida hivyo hivyo.

Najua wadau wengi mmekutana na usumbufu huu, naomba tuchange mawazo ni namna gani tutakomesha hili suala pale.

Transcript ni haki ya mtu,kwanini kusiwe na utaratibu mzuri wa kutoa? Kuna watu wanatoka mikoani kufuata transcript zao lakini inawachukua zaidi ya mwezi kwa sasa,inabidi warudi bila transcript huku wakiwa wametimiza masharti yote ya kupata.

Lini ofisi za serikali zitakuwa efficient na kuacha kuweka mazingira ya rushwa kiasi hiki?
 
Mh! ndo maana mi niliamu kwenda kusoma Masters yangu Kenya, hicho chuo unaweza soma Masters miaka saba!!!!!
 
SIO UDIZM ULIZIA NA IFM USIKIE MACHUNGU YAO. Utadhan hukusoma chuo. Inasikitisha sana.
 
Usemayo ni kweli kabisa mkuu. Rushwa imekuwa ni tatizo ndani ya taasisi zetu hizi. Kila ofisi unayotaka huduma yao unaambiwa kitu kidogo. Tanzania imekuwa ni nchi ya kitu kidogo (Rushwa).
Wazo nililonalo waweza kuwatafuta TAKUKURU wakakupa pesa ili iwe ni trap itakayowabana hao wala rushwa. I think it will work out.
 
Mh! ndo maana mi niliamu kwenda kusoma Masters yangu Kenya, hicho chuo unaweza soma Masters miaka saba!!!!!

Wewe sema sababu nyingine lakini hiyo ya kusoma Masters miaka saba inaweza kuwa wakati mwingine inasababishwa na uzembe wako mwenyewe. Au uwezo wako mdogo. Iwaje wewe umalize kwa miaka saba wakati wenzako wanamaliza ndani ya mwaka mmoja?
 
poleni sana watu wa UDSM.
Labda mkuje hapa kwa SAUT-Mwanza.
maana hakuna hiyo biashara ya urasimu.
Unachotakiwa kufanya ni kulipia bank then unacome back na bank statement yako kwa basa then within NO minutes unakabidhiwa hiyo nininhiii yako...! TURANSIKIRIPUTI.
 
And u can imagine hii ni University ambapo ilitegemea wawe mfano bora wa kutoa huduma mswano zilizonyooka. Nway, hiyo ni tabu ya kuweka wanasiasa watawale kila mahali. Hakuna kuwajibika wala kuwajibishwa. Ukiuliza utapewa jibu la kisiasa. Maisha yanaendelea.
 
Hii nchi inanuka ufisadi kila kona ni vilio tu.....nani tatuokoa na hili jamani?twende wapi?tumlilie nani?
 
Ajabu sana hiki chuo,yaani wamelala mpaka vyuo vingine vinakuja kuwa bora kwa huduma kuliko chuo cha miakak ya sitini.

Wao wanajivunia kuwa na profesas wengi na ranking wanazopewa na institution za nje. Sijajua vigezo vinavyotumika kuipa ranking UDSM kama vinaangalia mambo yanayoendelea pale.

Chuo hiki kimejaa urasimu kila kona,kuanzia kwenye kusoma,matokeo yanapikwa, sasa hivi hadi procedures za kubakisha wanafunzi ziko kiaina aina tu kwa baadhi ya faculty na schools hasa pale UD School of Business.
 
Hilo la transcripts ni tatizo kubwa sana ndugu yangu, mimi nilichukua yangu wakati ule unalipia sh. 5000 lakini sasa nasikia zimepanda unalipia nadhani kitu kama sh. 10,000 hivi, lazima tujiulize hivi ni kwa nini tulipie transcript zetu?, chuo kile kimeshikwa na wajasiriamali sana, ile trancript ukigeuza nyuma utakuta imeandikwa kuwa isipokuwa na seal ya chuo basi ni invalid, hii ina maana kuwa usitoe photocopy maana hiyo seal haitaonekana..huku kama sio kulazimisha biashara ni nini,transcript zenyewe wanakupa copy 3 tu, ajira zilivyo za shida hivi si kila siku utajikuta unaenda kulipia ili upate copies nyingine?
 
Ajabu sana hiki chuo,yaani wamelala mpaka vyuo vingine vinakuja kuwa bora kwa huduma kuliko chuo cha miakak ya sitini.

Wao wanajivunia kuwa na profesas wengi na ranking wanazopewa na institution za nje. Sijajua vigezo vinavyotumika kuipa ranking UDSM kama vinaangalia mambo yanayoendelea pale.

Chuo hiki kimejaa urasimu kila kona,kuanzia kwenye kusoma,matokeo yanapikwa, sasa hivi hadi procedures za kubakisha wanafunzi ziko kiaina aina tu kwa baadhi ya faculty na schools hasa pale UD School of Business.

Si unajua tena ajira za serikalini? Siye anayejituma ndiye anayetambuliwa katika ajira za serikalini. Kiongozi mmoja alikuwa anamwambia subordinate wake kwamba,"Fanya unachoambiwa na bosi wako, sio kila kitu unachokiona wewe no cha haki kila mtu atakiona hivyo. Wengi wanaona unachosema unawajibika ipasavyo ni sahihi" Kijana akaishiwa nguvu. Hapo alikuwa akimtetea fisadi mmoja anayetumwa kufanyia kazi vituo wanavyotaka fisadi huyo akavivuruge kwa maslahi yao, akilazimisha fisadi aliyeshitukiwa na kukataliwa na wadau na kutimuliwa arudi kituoni kuendelea kuvuruga.

Mpaka kizazi chenye kuabudu fikra za mtu binafsi zidumu kitoweke, kikashika usukani kizazi chenye kuamini ufanisi wa kazi wenye tija, kamwe Tanzania haiwezi kusonga mbele. Tutaendelea kunawa mikono mbele ya chakula lakini tusiweze kula.

Leka
 
Nchi zigine zenye wahitimu mamilion na kwa undergraduate credits mpaka 130 ili upate degree lakini ukimaliza tu na transcript unaondoka nayo sasa hapa nyumbani mmh yataka moyo. Transcript zinaandaliwa toka unaingia chuoni. kila mwisho wa semester idara inatuma matokeo ya wanafunzi. idara inayousika na vieti wao ni kuyaingiza tu kwenye transcript moja kwa moja. wanafunzi wakimaliza na vyeti vimekamilika. Ndani ya wk mbili DVC and VC wanaweka signature. Yaani unaondoka na vyeti vyote.na wanafunzi ni makumi ya elfu. Sasa hapa wahitimu ni nadra kufika elfu 20 lakini transcript mpaka uonge. Ni ile ile usemi wa miafrika ndo tulivyo.
 
......Hili tatizo sio chuo tu, limeanzia huku high school.Nchi imeoza kila sehemu wanahitaji rushwa.
 
hivi kwenye huu ulimwengu wa computerized records why should it take even a day to get an academic transcript?

Please Dar keep computerized records, I should be able to get my transcripts instantaneously after paying for the service. If I walk in.

A few days ago I needed my transcript forms an academic institution here in the US, I went online around noon on a certain day, I got my transcripts at around the same time ( by mail) the following day.
 
Back
Top Bottom