UDSM kurusha satellite ya mawasiliano 2023

UDSM kurusha satellite ya mawasiliano 2023

Mimi sio mwana sayansi,je wakirusha kutakuwa na impact gani kwa watanzania?
Mkuu siunaona makampuni ya Television na mawasiliano yanatumia satellite za nje kurusha mawimbi yao ambapo huwagharimu kulipia na pia ww mteja kulipia hivo cost kuwa kubwa but tukiwa na sat yetu means tuta code na kudecode through hio sat na kurahisisha upatikanajupatikanaji wa local events
 
mwandish tupe faida ya satelaiti hyo. na nn maana ya satelaiti, utasaidia weng!!!
satellite ni kitu kinacho zunguka sayari, mwezi ni sat asilia wakati hizi tunazorusha ni man made au artificial sattelite faida ni kuwa mawasiliano bora kabisa ni kwa njia ya satellite,kupiga simu kutazama tv sambamba na kuangalia hali ya hewa pia mambo kama Global positioning system vyote ni mazao ya sattelite
 
Heee hata kuwasifu wamejitahidi kufikiria tofauti
 
Chuo kikuu cha Dar es Salaam kushirikiana na kitengo cha uhandisi na teknolojia (CoET) pamoja na kile cha uhandisi wa kompyuta na mawasiliano (CoICT) wamezindua mpango maalumu wa miaka 7 wa kurusha satellite ya kwanza Afrika Mashariki, ifikapo mwaka 2023.

Mkuu wa mradi huo ndugu Magaka amedai Kituo maalum cha mambo ya anga cha Mfaume Kawawa Space Centre (MKSC) ambacho kipo katika hatua za mwanzo kabisa za ujenzi kinaendelea kwa kasi ili kufikia malengo yake ya kuwa tayari hapo mwaka 2023.

Baada ya kurushwa kwa satellite ya kwanza hapo mwaka 2023, kutakakuwa na mpango wa kurusha satellite nyingine kila baada ya miaka mitatu mitatu huku nyingine zikirushwa mwaka 2026,2029,2032 na mwaka 2035.

Hii ni baadhi ya miradi ambayo chuo kikuu cha Dar es Salaam kinafanya ili kuendelea kuwa chemchem ya maarifa Afrika na dunia kwa ujumla huku nyingine ikiwa ni mpango wake wa kusambaza nguvu za jua kwa watanzania milioni 15 hapo mwaka 2030.

Kila la kheri UDSM
 
Africa mashariki bado iko nyuma sana katika Teknolojia ya mawasiliano mana mpaka leo bado wanatumia mikonga kurusha mawasiliano, wakati nchi zingene wanatumia Satellite kwa mda mrefu sana.
 
Haiwezakani ... bado sana.hata ulaya sio nchi zote zina hio kitu.wenyewe wameungana
No offense, ila kwa nchi yetu bado sana! Bajeti ya kupeleka satelite ipo ktk trillions, tuna matatizo mengi sana kama taifa, hiyo hela ingetumika kwa mambo mengine!
Ya satelite tutafanya 2050 na kuendelea.
 
For tz haiwezekani kurusha satellite zetu wenyewe labda itengenezwe pia kwa ushirikiano wa nchi au kampuni nyingine kwa sababu mpaka sasa kuna nchi kumi tu duniani zinazoweza kutongeneza satellite na kuzilusha wenyewe pia zipo nchi nyingi zinatengengeneza sat ila hurushwa kwenye nchi nyingine. Nchi 10 ambazo zinauwezo was kuweka sat kwenye orbit kwa vifaa vyao wenyewe
1. USA
2. RUSIA
3. JAPAN
4. ISRAEL
5. IRAN
6. INDIA
7. CHINA
8. BRAZIL
9. FRANCE
10. NORTH KOREA
Hii ya UDSM nadhani itakuwa ni mipango tu ila good luck.
 
No offense, ila kwa nchi yetu bado sana! Bajeti ya kupeleka satelite ipo ktk trillions, tuna matatizo mengi sana kama taifa, hiyo hela ingetumika kwa mambo mengine!
Ya satelite tutafanya 2050 na kuendelea.
80px-GSLV.svg.png

hii ni satellite lunch vehicle - GSLV Mk II. ya gharama ndogo tu lakini isome hapo chini gharama, utanyanyua mikono.
Function Medium Lift Launch System
Manufacturer ISRO
Country of origin India
Cost per launch Mk II ($36 million)
hapo hujajenga lunch pad ambayo ni gharama kubwa kuliko, sisi tujenge shule kwanza
 
Mkuu siunaona makampuni ya Television na mawasiliano yanatumia satellite za nje kurusha mawimbi yao ambapo huwagharimu kulipia na pia ww mteja kulipia hivo cost kuwa kubwa but tukiwa na sat yetu means tuta code na kudecode through hio sat na kurahisisha upatikanajupatikanaji wa local events
Nimeridhika na majibu yako braza ila kuna jamaa kalibeza swali langu....asante sana
 
Back
Top Bottom