UDSM kuna nini jamani?

Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,597
1,005
Ktk taarifa ya habari ya jana mlimani tv nilimuona doctor mashuhuri na mtaalam bingwa wa siasa za africa na dunia kwa ujumla doctor Azaveli Rweitama akichambua kwa ufanisi mkubwa kuhusu kuundwa kwa baraza jipya la mawaziri.

Kama kawaida yake alichambua kwa ufanisi mkubwa sana, alisema mfumo mzima wa serikali ni mbovu kuanzia chini. Chakushangaza ni pale nilipoona maandishi haya kwenye jina lake, doctor Azaveli Rweitama mhadhiri mstaafu udsm!!!.

Hivi kwa nini wataalam ambao si wanafki wanaondolewa udsm? Tunajua labda mkataba wake umeisha lakini umri wake bado unaruhusu sana. Kwa siasa za Tanzania usishangae yakamkuta ya Profesa Baregu!, lakini naamini chuo kinachokuja juu sana Kwa sasa St Agustino hawatamwacha mtaalamu huyu kama udsm watamwacha bingwa huyu wa siasa.

Nakumbuka usemi wake mmoja aliowahi kuusema pengine ulikuwa shubiri kwa ccm, alisema hivi (MIMI NI CCM MFU! Mwanachama asiyelipia kadi!) tafakari maneno haya kabla ya kuchangia.
 
Hiyo ndo hali ya aibu inayolikumba taifa, watalaam wazuri wasema ukweli wanasumbuliwa sana na siasa za matumbo za watalawa; LAKINI MPIGANAJI hawi mpiganaji mzuri na mkubwa bila kupigana, Dr A. atadhihirisha hilo.
 
mimi namjua sana huyo mzee yupo bright kweli na muelewa wa mambo............
 
UDSM MUDA SI MREFU ITAKUWA KAMA CHUO KIKUU CHA KATA! WANAINGIZA SIASA ZISIZO NA TIJA. HIVI KWELI KULIKUWA NA MANTIKI YA KUMTOSA BAREGU? NA KAMA UNAVYOSEMA WANATAKA KUJICHANGANYA TENA KWA JEMBE LINGINE, Dr. LWAITAMA!!!..... HALAFU WAWAUNDIE ZENGWE KINA MKUMBO, BASHIRU, PARAMAGANDA.....
 
Hata uwe muhim kiasi gani umri wa kustaafu utumishi wa uma unapofika yabidi ukae pembeni upishe wengine wapate nafasi
 
Umri wake umefika kustaafu. Ulishawahi kuona mtu anacheza soka ya ushindani mechi zinazotambulika akiwa na miaka 50? Roger Milla tu anashikilia rekodi ya kukipiga kombe la dunia na miaka yake 42, so itafika mahali lazima ustaafu tu
 
kuna mtu kacomment dr muuza sura sio kweli anatumia njia mbali mbali kuelimisha umma wa wawatanzania ambao hawawezi kuwa nae ana kwa ana....pili ni kulelea uozo uliojaa kwa viongozi wetu na kamwe hatutaweza kukalia kimya uozo huu udsm imekosa mwelekeo
 
Umri wa kustaafu ukifika lazima mtu astaafu! kanuni ya utumishi wa umma unaruhusu kwa wahadhiri kupewa mkataba anapostaafu kwa masharti sio lazima kila anayestaafu apewe mkataba. Baadhi ya masharti ni kuwepo na upungufu wa wahadhiri, kutokuwepo kwa mhadhiri mwenye ujuzi alionao mstaafu na mengine. Vilevile, kanuni haziruhusu mtu kundelea kupewa mkataba akishafikisha umri wa zaidi ya miaka 70. Kwa iyo kabla hamjatoa lawama lukuki mngeuliza idara aliyokuwa anaifanyia je walikuwa wanamuhutaji wakanyimwa kupeleka maombi?
 
sheria ya utumishi wa umma ni kwamba ukifika miaka sitini unastaafu. Je huyo Lwaitama ana umri gani? Je na huyo Prof Baregu ana umri gani? na je wamelalamika kwamba wamestaafishwa kabla ya umri wao haujafika? si vizuri kulaumu CCM kwa kila kitu, msiharibu JF ionekane ya watu ovyo ni vizuri kufikiri kwanza kabla haujaandika.
 
Hivi kwa nini wataalam ambao si wanafki wanaondolewa udsm? Tunajua labda mkataba wake umeisha lakini umri wake bado unaruhusu sana. Kwa siasa za Tanzania usishangae yakamkuta ya Profesa Baregu!, lakini naamini chuo kinachokuja juu sana Kwa sasa St Agustino hawatamwacha mtaalamu huyu kama udsm watamwacha bingwa huyu wa siasa.

Nakumbuka usemi wake mmoja aliowahi kuusema pengine ulikuwa shubiri kwa ccm, alisema hivi (MIMI NI CCM MFU! Mwanachama asiyelipia kadi!) tafakari maneno haya kabla ya kuchangia.

Wamesema ni Mhadhiri mstaafu. Kustaafu ni jambo jema. Kama watamuhitaji watamuajiri kwa mkataba mwingine tofauti. Hata hivyo, ni jambo jema mfanyakazi kustaafu akiwa na nguvu zake bado. Xvery ni mwanataaluma hivyo hatakosa kazi sehemu nyingine.

Nampongeza Dr. Lwaitama kwa kustaafu bila kashfa.
 
Umri wa kustaafu ukifika lazima mtu astaafu! kanuni ya utumishi wa umma unaruhusu kwa wahadhiri kupewa mkataba anapostaafu kwa masharti sio lazima kila anayestaafu apewe mkataba. Baadhi ya masharti ni kuwepo na upungufu wa wahadhiri, kutokuwepo kwa mhadhiri mwenye ujuzi alionao mstaafu na mengine. Vilevile, kanuni haziruhusu mtu kundelea kupewa mkataba akishafikisha umri wa zaidi ya miaka 70. Kwa iyo kabla hamjatoa lawama lukuki mngeuliza idara aliyokuwa anaifanyia je walikuwa wanamuhutaji wakanyimwa kupeleka maombi?

na kwa kuongezea tumekuwa tukilaumu kwamba vijana hawaajiriwi kwa kuwa hawa wazee hawataki kuachia ngazi, leo hii tunabadilisha goal post na kulaumu kwanini wazee wanastaafu? which is which? lazima vijana wachukue nafasi nao wapate uwezo waje kuwa wachambuzi wazuri kama akina Lwaitama
 
Kumbukeni UDSM inakufa hata kina Prof. Kabudi, Dr. Mvungi, Dr. Fauz na majembe kibao wameanzisha chuo chao kinaitwa university of bagamoyo. Hapo watabaki kina Misanya Bingi na kundi lake pamoja na dr. Bana na Mukandara.
 
kwanini tusiongelee kuwaanda watu wengine kama wao bali tunaongelea kuendelea kuwa nao, je ikitokea wakaaga dunia inakuaje. Mi sina shaka na utendaji na umahiri wao, ila ninatatizo la kuwaendelea kuwatumia bila ya kuwaanda na kuwajenda vijana ili wawe mahiri kama wao.
 
Anafahamu sana masuala ya siasa na amekuwa akichambua siasa kwa muda mrefu lakini yeye hasa ni mwalimu wa philosophy na linguistics hayuko kwenye idara ya sayansi za siasa. Kudhihilisha kwamba ccm hawana ubaguzi utaona Dr. Bana naye akistaafu hawatamuongezea mkataba.
 
Umri wa kustaafu ukifika lazima mtu astaafu! kanuni ya utumishi wa umma unaruhusu kwa wahadhiri kupewa mkataba anapostaafu kwa masharti sio lazima kila anayestaafu apewe mkataba. Baadhi ya masharti ni kuwepo na upungufu wa wahadhiri, kutokuwepo kwa mhadhiri mwenye ujuzi alionao mstaafu na mengine. Vilevile, kanuni haziruhusu mtu kundelea kupewa mkataba akishafikisha umri wa zaidi ya miaka 70. Kwa iyo kabla hamjatoa lawama lukuki mngeuliza idara aliyokuwa anaifanyia je walikuwa wanamuhutaji wakanyimwa kupeleka maombi?

Sio kweli mkaka, Prof. Abdu Khamis Mtajuka wa IKS turns 76 this year, na anaendelea kufundisha bila kokoro. Last semester alinifundishia Sintaksia, na semista hii anafundisha darasa la Masters na wale wa Ph.D by coursework.
Tuko pamoja?
 
Back
Top Bottom