UDSM ilipokataa kuundwa kwa board ya mikopo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDSM ilipokataa kuundwa kwa board ya mikopo.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Jackbauer, Feb 7, 2011.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka wanafunzi wa UDSM kupitia DARUSO walitoa waraka wa kupinga uanzishwaji wa bodi ya mikopo.
  Ni chuo pekee kilichopinga kuanzishwa kwa HESLB,walipingwa na serikali pamoja na vyuo binafsi especially Tumaini University.

  Kutokana na hali ya migomo ya wanafunzi inayoendelea kila kona ya nchi,

  Je UDSM walikua sahihi?
  Mwenye huo waraka atuwekee hapa tuone 'hofu' ya UDSM ilijikita kwenye issue gani zaidi.
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu nakumbuka vizuri sana wakati UD wakigoma kuanzishwa kwa hii bodi Tumaini wakaenda kwenye vyombo vya habari kuwapinga na kuwatukana wakiwa chini ya Godwin Gondwe..... sasa mambo yamewarudi na wao wenyewe!!
   
 3. s

  sirgeorge Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka wakati ule waziri wa elimu ya juu alikuwa ni Pius Mwandu, ule mswada wa kuanzishwa kwa bodi ya mikopo ulipingwa na udsm kwa kuwa hakuwasilikisha wananchi na wanafunzi kwa ujumla wake. Muswada ule ulikuwa na vipengele vyenye masharti magumu kuwa ili uweze kupata mkopo ni lazima uwe na mali isiyo hamishika (kama nyumba,mashamba etc). Na muswada huu ulipelekwa kwa siri sana bungeni na ulitakiwa usomwe cku ya jumanne sikumbuki tarehe ila wanafunzi wa mlimani wakapata taarifa hiyo wikend(jumapili), kilichofuatia jumatatu kuna wanafunzi walienda dodoma kumsihi waziri asiwasilishe muswada huo lakini ilishindikana, kwa madai ya Mwandu kuwa wanafunzi walishirikishwa (ilikuja kuonekana ni baadhi ya wanafunzi wa mzumbe ndo walishiriki kongamano fulani, na lilikuwa si kongamano la kujadali mambo yaliyomo katika muswada huo, hivyo wanafunzi wa udsm hakushiriki hilo kongamano). Kwa hiyo siku ya jumanne wanafunzi walianza kunji zito sana chini ya jamaa mmoja anaitwa Bahati Tweve (alikuwa anasoma sheria), nakumbuka Mwandu mpaka alimtaja huyu jamaa bungeni kuwa amefutiwa ufadhili wa serikali kwa jinsi alivyosimama kidete. Lakini cha ajabu Tumaini University waliusifu sana muswada huo eti wakisema ulikuwa ni mkombozi wa elimu ya juu kwa watanzania. Tulichokuwa tunadai wanafunzi wakati ule ni kuwa mambo mengi sana yalikuwa hayaendani na mazingira halisi ya mtanzania na yalikuwa yanapingana na ripoti ya prof. mmoja(jina nimelisahau) ambaye alipewa kazi na mhe.Mkapa kutathmini hali ya watanzania katika suala ya kupata mikopo bank, ripoti ile iliweka wazi kuwa watanzania hawakopesheki katika bank kutokana na kutokuwa na mali/rasilimali ambazo zinatambulika kisheria katika kupata mkopo bank. Sasa ule muswada haukuzungiatia hayo yote na hiyo ndo ilikuwa hoja ya sisi wanafunzi kwa wakati ule na ilikuja kujulikana ule muswada walikopi na kupaste kutoka Botswana.

  Nimeweza kukumbuka machache kutokana na ule mgomo wa mwaka 2004, kwa wanafunzi waliokuwepo wakati ule mlimani wanaweza kuongezea, ila chuo kilifungwa kwa wiki mbili kutokana na mgomo huo.

  Matokeo ya migomo inayoendelea leo ni shauri ya kutosikiliza maoni ya wasomi ya UDSM.
   
 4. K

  Kinombo JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii issue ilianza 1990-1996 hivi chini ya wizara ya sayansi na teke linalokujia
   
 5. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  Bodi ya mikopo kwa faida ya nani?kila mara wanavyuo kugoma chanzo bodi hii bora ivunjwe na uandaliwe utaratibu kwa kushirikisha vyote na c tume za kuchunguza ni kulea jipu,hivi mwenyekiti c alitajwa na Dr Slaa miongoni mwa mafisadi kumi au c yeye?hivi hatuna wataalam wengine hadi mtu mmoja nyazifa lukuki?
   
 6. b

  bakarikazinja Senior Member

  #6
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yaani umenikumbusha mbali maana tulipigwa na tulitukanwa tukaitwa wa vuta bangi sasa naona yana warudi wenyewe ndio wanaonekana wavuta bangi
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ndio wanasiasa wetu wasioheshimu maoni ya wasomi.
   
 8. U

  UZEE MVI Senior Member

  #8
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  KAMA KAWAIDA YAO POLISI WALITUMIKA KUTAWANYA WAANDAMANJI KWA MABOMU PALE KARIBU NA MAENEO AMBAPO SASA HIVI KUNA MLIMANI CITY.

  KABLA KABLA YAKE JIONI YALIFANYIKA MAANDAMNO kutoka Nkruma Hall hadi mabibo hostel ambapo barabara zililazimika kufungwa kwa muda.

  Wanachuo katika maeneo mbalimbali walikuwa na kazi ya ziada kuwaeleza nini lengo la mgomo huo kwani wengi wa wazee wetu walikuwa bado wametawaliwa na falsafa ya kuwa wanafunzi ni wakorofi. Katika maeneo mengi wanachuo walionekana wakisisitiza kwamba madhara ya uundaji wa sheria ya Bodi yangekuwa kwa vizazi vijavyo lakini watnzania wengi wkiwamo wasomi wa Tumaini University hawakuelewa somo. Nadhani sasa hivi linaanza kueleweka. Lakini tayari majuto ni mjukuu.

  N
  PHP:
  akumbuka pia kuwa mara baada ya kalikizo kalikosababishwa na mgomo ule yalifanyika tena maandamano kwa lengo hilohilo hadi katika viwanja vya Jangwani ambako yalihitimishwa kwa mkutano wa hadhara. Awamu hii ya pili walau wananchi na wafanyabiashara wa manzese walituunga mkono.

  Further comments plz.
   
Loading...