UDSM: Huu ni Ufisadi wa aina yake... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDSM: Huu ni Ufisadi wa aina yake...

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ngoshwe, May 26, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Miongoni mwa masharti ya kujiunga na shahada ya Uzamili katika vyuo vingi vya nje (Ulaya, Marekani na kwingineko) ni kuwa na uthibitisho wa kujua lugha ya Kiingereza kwa usahihi. Katika hili unapaswa pamoja na cheti chako cha shahada ya kwanza, transcipts nk, uwasilishe cheti cha masomo ya Lugha ya Kiingereza.

  Japo kuwa Kiingereza ndio lugha ya kufundishia Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na moja ya kozi ya lazima ukiwa hapo ni somo la mawasiliano (communication Skills), unapotaka kupata uthibitisho wa chuo Kikuu cha Dare es salaam (UDSM), inaoneka kuwa chuo hicho kupitia Idara yake ya Lugha kinatoa tena kwa gharama ya zaidi ya Tshs. 10, 000 Cheti cha kinachoitwa " Certificate of Proficiency in English" (CPE).

  Kwa wale ambao wamewahi kupata cheti hicho kwa kweli unaweza kuona ni bishara ya kitapeli inafanyika hapo, kwani kwa mtazamo halisi, cheti hicho ambacho binafsi nilikipata kwa zaidi ya Tshs, 15, 000 ni kijikaratasi tu cha "A4" ambacho kinatolewa na Idara ya "Foreign Languages & Linguistics" na kimesainiwa na kimegongwa muhuri wa "rubbers stamp" na "Coordinator - Communication Skills Unit". pia, binafsi hata nilipolipia, fedha nilitoa kwa Katibu mhtasi (sekretari) na kupewa risiti ya "pay cash" isiyo na nembo yeyote ya UDSM...

  Cha ajabu, tofauti na cheti cha shahada na Transcript ambavyo unaweza kutoa na kutuma nakala kivuli kwa kila chuo unachoomba, hiki cha kujua Kiingereza cha UDSM inabidi uwe na nakala halisi (orignal copy) kwa kuwa kwenye kila cheti wanaandika "Only orignal copies with official stamp should be considered genuine" yaani wakimaanisha hako ka "rubber stamp" ka Mratibu wa Kitengo cha Lugha ndo jenuini yenyewe.

  na UDSM wanataka ulipie fedha kila nakala watakayokupa. Cha kusikitisha zaidi, cheti hicho cha UDSM kimekataliwa na zaidi ya vyuo vitatu kuwa hakina hadhi yeyote ya kuthibitisha uwezo wa kujua kiingereza. Hivyo kulazimika kuchukua masomo ya Lugha yanayotolewa na British Council.

  Ninachojiuliza, hivi ni kwanini ikiwa mtu umesoma hapo UDSM na kufuzu vizuri somo la "Communication Skills" bado chuo kna shindwa kukusaidia na badala yake kuachia huu uhuni wa baadhi ya walimu wa Idara ya Lugha kujipatia fedha kupitia hivi vyeti ambavyo pangine havimsaidii mhusika au kwa muonekano haviwezi kuwa na gharama kubwa ya zaidi ya Tshs. 10, 000??.

  Ni kama ka ufisadi fulani hivi!!.
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Mkuu pole kwa yaliyokukuta ila napata tatizo kidogo kujua waliokuomba uthibitisho wa uwezo wako katika matumizi ya lugha ya kiingereza walikuwa wanategemea kupata uthibitisho wa namna gani?Maana kwa uelewo wangu mdogo najua vyuo vingi duniani inapofika suala la kuthibitisha ni lazima wanakuwa very clear juu ya nini hasa wanataka.Vyuo vingi Ulaya na Marekani vinataka TOEFL au IELTS kama uthibitisho wa kukimanya kingereza na huwezi kupeleka matokeo tofauti zaidi ya hayo.Sasa sijui kama ulifanya utafiti kabla ya kuamua kwenda kufuatilia hiko cheti huko UDSM?

  Kuna cases nyingine pia,unaweza kuangalia kama unaweza ku-wave hizo requirements za uthibitisho wa kukimanya kingereza hasa kama chuo unachotaka kwenda kusoma kinatambua mfumo mzima wa elimu wa nchi uliyotokea au tuseme mtaala wa elimu katika taasisi ya elimu uliyohitimu awali.

  Kifupi UDSM haina utamaduni wa kusaidia watu waliokwishahitimu shule pale na mara zote unapoenda kufuatilia mambo yako pale unachukuliwa kama mgeni ambaye utasababisha usumbufu tu nafikiri hii ndo attitude ya baadhi ya wafanyakazi na uongozi wa UDSM.Yaani hata ukiomba recommendation toka kwa baadhi ya wahadhiri ambao wamekufundisha na kimsingi wana kufahamu nayo inaweza kuwa shida.

  Kwa mfano unapata barua pepe ya mhadhiri toka kwenye tovuti ya chuo au ya kitivo fulani na unaamua kumuandikia e-mail kuhusu jambo fulani ambalo yuko kwenye nafasi ya kukuelewesha au kukusaidia lakini hatokujibu....basi at least nijibu niandikie..."Please do not disturb,I have better things to do"...kwa maana ukishapata e-mail kama hiyo unajua huyo mtu hayuko kwenye nafasi ya kukusaidia kuliko kuwa kimya!

  Kwa sasa UDSM ni sehemu ya mfano wa watu waliopata elimu lakini hawajaelimika...sisemi kila anayefanya kazi
  UDSM hafanyi mambo yake vizuri lakini nafikiri wafanyakazi wengi wa taasisi hii wanafanya kazi kwa mazoea zaidi,wamejisahau na wamelewa na sifa ambazo zimejengwa na watu waliovuja jasho katika kuijengea UDSM sifa
  na uwezo wake.

  Nimesoma UDSM na yanayotokea sasa yanatia aibu na kuumiza moyo!Tujifunze toka kwa wenzetu...!


   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Asante sana Mkuu. Hitaji lilikuwa ni TOEFL . Baada ya kujaribu kuulizia nikaambiwa hata UDSM cheti ambacho kinakubalika kama kwa vyuo vya kimataifa na ndiipo hapo nilipokutana na hali hiyo..nilikwenda Jumatatu wakaniambia niende Alhamisi, hapo nikakutana na wengine kibao. Kuna utartaibu wa kuonana tena na Wanazuoni wa hapo, unakalishwa chini kama mtoto wa chekechea na kuanza kuulizwa kwa kimombo unakimanya uzuri, kama unajua kujieleze, iwapo umesoma kwa lugha ya kiingereza nk. Fikiria hapo hujapewa hata quiz ya kuandika wala kusikiliza lectures lakini baada ya zoezi la kuojiwa, Sekretari ana kuandalia hako ka cheti kama ka recomendation letter kenye particulars zifuatazo na unapewa baada ya kusainiwa na alie kuhojia na kulipa mpunga wa kutosha (by then I had to pay Tshs. 15, 000 for the first and 3, 000 for each copy):

  University of Dar Es Salaam
  Department of Foreign Languages and Linguistic
  Certificate of Proficiency in English

  (logo ya Uni)

  Name: (first, Middle, last) Ngoshwe wa JF

  Citizenship: Tanzanian Date of Birth: 5 February 1977


  Knowlegde of Engilish Language:

  I Listening Comprehension

  a)understanding converstaions and lectures without efforts [ ]
  b)Understands almost everything when spoken to slowly
  c)Understands with difficulty, needs repetition [ ]
  d) cannot follow conversations and lectures al al l[ ]

  II: Writing

  a) writes well with no mistakes [ ]
  b) writes with few Mistakes [ ]
  c) writes with difficulty and makes many mistakes [ ]
  d) Cannot express simple ideas in writting[ ]


  II Speaking
  a) Speaks fluently, correctly and is easily [ ]
  to understood [ ] b) Is easily understood, but is not always fluent and correct [ ]
  c)Speaks broken English with Mistakes [ ]
  d) Cannot express simple ideas in spoken English[ ]

  IV: Reading

  a) Reads and understands without difficulties [ ]
  b) Must read slowly, but understands the context [ ]
  c) has problem understanding and must use a dictionary often[ ]
  d) cannot understand even simple text [ ]

  Remark: This certificate is for application to the University of .Kanumba of Hollywood, the applicant studies from secondary school to University level through English Medium


  Examiner: Dr. Kilaza Mkamataji:

  Senior Lecturer and Coordinator, Communication Skills Unit

  Date: ................................Signature: ................................ (stamped with rubber stamp)

  (only orignal copies with official stamp should be considered genuine)

  WIZI WAO UPO HAPA:
  a) kama ulisoma kwa kiingereza, inakuwaje wakukalishe tena chini kukuuliza iwapo unajua kiingereza
  b) kama wanajua kuwa ulisoma kwa kutumia lugha ya Kiingereza toka shule ya msingi, iweje waanze kukuandindika "remarks" ambazo zinaweza kuthibitisha tofauti na matokeo yako ya somo la mawasiliano (communication Skills- CL) ambayo yapo kwenye Transcript yako.
  c) Ikiwa somo la CL linasomwa kwa mwaka mzima kama somo la lazima (compulsory course) na linafundishwa na wakufunzi wa Kitengo hicho cha Lugha, inakuwaje tena wanakukalisha chini baada ya kuwaambia ulihitimu hapo ili wakusaili kwa lugha ya Kiingereza na ulipie tena kupata cheti.

  d) kwa nini hiki cheti hawatoi kwa muhuri rasmi wa chuo badala yake ni wa Kitengo cha Lugha na kipo kwenye karatasi ya kawaida tu kama barua na malipo hayafanyiki kwa mfumo wa kawaida wa kulipia kwa "cash office".ili itakiwe stakabadhi halali ya chuo.
   
 4. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Ndugu yangu mimi nakuambia shida ya hawa watu ni kuwa wanafanya mambo kwa mazoea.Pesa kwao ni kila kitu na wanasahau kuwa vitendo vyao hivi vinashusha thamani ya chuo yaani chuo kwa sasa kimebaki jina tu.Watu wanakosa commitment na dedication katika mambo wanayoyafanya.Vitu kama hivi ndo vinakufanya ufikiri...hivi kama UDSM,watu wamesoma na tunatarajia watakuwa chachu ya maendeleo na utendaji bora wa kazi wanafanya mambo kama haya,je huko mashambani hali ikoje?
   
 5. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Aisee, huyu Kilaza Mkamataji kumbe bado hajastaafu? Ameji''masauni'' nini?
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Funny stuff indeed.
   
 7. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2010
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Aisee i also got tht certificate yani,and bad things is KINA EXPIRE AFTER THREE YEARSSS!
  Ndo mara ya kwanza nasikia eti cheti cha academic merits kina expire!!!
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Vyeti vya kingereza vina muda wake..kuanzia EILTS na TOEFL etc ..havitumiki till death.
   
 9. S

  Subira Senior Member

  #9
  May 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  tangu mwanzo wa hii thread na majibu yake yameniacha hoi kwa kicheko ilove you people yaani nimecheka sana, swali langu kuu ni kwanini watu wa lugha huko ud wanataka kiswahili kiwe ndio lugha kuu ya kufundishia ? kumbe nyuma yake ilikuwa haka kamradi wallahiiiiiiii
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,325
  Trophy Points: 280
  Pole Ngoswe,
  Kwa UDSM hiyo ni biashara au sehemu ya ujasiliamali wa idara mbalimbali za chuo.
  Concern yangu ni moja tuu, jinsi hivi vyuo vya ulaya vinavyotudharau sisi kwenye lugha yao. Mpaka imefikia kiwango cha kudharau lugha ya UDSM kwa graduate wake mpaka wafanye TEOFIL, huu ni unyanyasaji na dharau ya hali ya juu. Hawa wazungu walipotutawala tukifanya mitihani ya Cambridge walituheshimu, leo tumejitawala, tangu O-Level medium of instruction ni Kiingereza, leo graduate wa Chuo Kikuu chetu kwenye Linguistics hawamtambui!, kisa sio wao ni sisi.

  Halafu wana double standarsd za ajabu, wakati sisi hawatutambui, wenzetu Wakenya na Afrika Kusini eti wanawatambua, wanakiingereza kizuri!. Ukienda mikutano ya kimataifa, Watanzania wanazungumza kiingereza kizuri kuliko Wakenya, tatizo letu ni intonation ya kutojidai wazungu na wengi wetu hawajiamini sana, hivyo stammaring ni nyingi, lakini Wakenya wana Kiingereza kibovu huku wakijiamini ndicho chenyewe, na ndicho wanachofundishwa wanetu kwenye hizi Academy schools!.

  Udhaifu huu yaonekana Watanzania tumeukubali kwa kuajiri Wakenya wengi kwenye Ualimu na kazi za hoteli, hapo milango ya free labour migration bado haijafunguliwa, ikifunguliwa tutaimport mpaka mesengers wanaozungumza kizungu!.
   
 11. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inaelekea Ngoshwe ulikipata kile cha zamani sana. Siku hizi unaweza ukatoa photocopy na kukitumia sehemu nyingine ila ni valid for 3 years, na ndio maana Iteitei ameandika hapa chini. Kwa sasa hivi haufanyiwi mahojiano, ila kuna paper kali sana, na mimi nilipokuwa nasaka scholarship nililazimika kufanya mtihani huo. jaribu kupita tena pale, utaratibu umebadilika. Ila kuhusu hoja ya kwamba idara hiyo inafanya ufisadi, hapo sina maelezo
   
 12. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :angry:
   
 13. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Thanx mzee. Inawezekana ikiwa hivyo. Lakini sasa hawatanipata tena hapo UDSM manake ni chuo ambacho hakina msaada kabisa kwa wasomi waliohitimu hapo so to say. Japo waadhiri wengi wamesoma nje ya nchi ambapo walipaswa kujifunza jinsi wenzao wanavyoendesha vyuo lakini ni upuuzi mtupu hapo UDSM. Ubinafsi mwwingi, ujasiliamali umekuwa kipaumbele kuliko kuelimisha wengine nao waweze kujua.

  Kwa hoja na mzee Pasco , kwa kweli nakubalina nawe kabisa jinsi watanzania tunavyodhalilika kwa elimu zetu. Tupo katika nchi za Jumuiya ya Madola (Common wealth Countries) lakini bado wazungu wanatuona kuwa hatuna uwezo hata wa kuongea kiingereza. Cha ajabu ukifuatilia kiingereza wanachoongea wakenya, Waganda, wa Afrika ya Kusini (bantuz) na wale wa kutokea Afrika ya Magharibi unaweza kusema wanaongeza kilugha cha kwao ambacho waweza ita ni "Pidgin English"..hawaeleweki kabisa. Lakini hali ya kujamini kumewanusuru kuathiriwa na kasumba hii ya wamadharibi wanavyotuchukuliwa wa Tanzania.

  Binafsi naona pia kwa mfumo huu ambao hata vyuo vyetu waanafanya kama hili la UDSM, ni moja ya chanzo cha sisi kujidhalilisha kwa mataifa mengine..Kwa nini kama mtu amesoma "Communication Skills" au Lugha ya Kiingereza katika Kozi nzima akiwa chuoni na walishasoma masomo ya lugha huko sekondari nk, lakini bado wanataka kumkalisha chini ili wamsaili badala ya kumpa cheti ambayo kinaonyesha kuwa alifaulu lugha iwapo matokeo kwenye Transcipt hayatoshelezi kuthibitisha uwezo wake wa kujua lugha.

  Ukiwa katika vyuo vya nje unaweza kujionea ni jinsi gani watu wa mataifa mengine hata hao wenyewe wazungu wasivyoelewa kwa ufasaha lugha hiyo ya Kiingereza (kwa mfano wazunu wa England na Wales, wanajiona wao ni bora zaidi kwa kuwa wanaongea Kiingereza cha Malkia na hivyo kuwadharau waScottish).

  Iwapo Mscottish atasoma kwenye chuo cha upande wa England, au hata kwa wale wabunge wanaoingia katika Bunge la Commons na Hosue of Lords bado wanaonekana hajui kabisa Kiingereza kwa kuwa tu wanapoongea kiingereza huwa wana kwenda haraka na kukata maneno kama si kuyameza.

  Vinyo hivyo, kwa wazungu toka nchi za Scandinavia, Ufaransa, Ujerumani na kwingineko, wakiwa Ulaya au Marekani wanaonekana ni maskini kabisa wa lugha ya Kiingereza kwa kuwa wakizungumza au kuandika wanachanganya maneno na lugha za kwao lakini kwa matakwa ya vyuo, hawatakiwi kuwasilisha hizo TOEFL na IELTS kuthibitish kuwa wanafahamu kiingereza.

  Nadhani haina haja hata kurejea kwa wenzetu wa masharuki ya kati na wale toka mashariki ya mbali kama China na Bara Asia....!!!.

  Ebu sikiliza mtu kama huyu anasema kiingereza:

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kama nakumbuka viziru pale UD, kituo cha kufanya mitihani ya TOEFL kipo pale computer centre! japo kuwa ni kweli pia idara ya lugha wanatoa cheti lakini hakifanani kwa namna yoytote ile na cheti cha TOEFL! na kumbuka niliwahi kupata scholarship ya chuo kimoja kule US na hitaji lao ilikuwa nifanye TOEFL test, nilipoenda ubalozio wa US pale msasani wakanielekeza vituo vya kufanyia huu mtihani, wakati ule ilekuwa ni International School of Tanganyika (IST)- Dar, British Council-Dar na UDSM Computer Centre-Dar, na kuna tarehe maalumu ya kufanya hii mitihani nafikiri kwa mwaka ni mara 3 au 4 hivi sikumbuki vizuri. Na mwisho hii mitihani sio kwa watanzania tu, nawafahamu jamaa zangu wawili watatu wa mataifa ya kigeni (sio Tanzania) nao pia walitakiwa kufanya mtihani huu!
   
 15. K

  Konzogwe JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 441
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Haya!!!! Nimewasoma wandugu zangu toka Tz.Kuhusu TOEFL mie 'no comment'! Jambo nalotaka kuzungumzia toka vyuo vyetu Tanzania ni poor information/dharau kwa watendaji,hawajibu e-mail za maulizo sanjari na kuchelewa ku update tovuti zao.
  Nitoe mfano: nina mdogo wangu kafanya Mature age entry examination pale Udom tar 24 April. Tangu hapo hawajaweka results kwenye tovuti ilhali watahiniwa hawakuzidi hamsini,sijui kwanini kuchelewa kwa kazi ndogo kama hiyo! Kama haitoshi vile ukiwapigia simu wale receptionist wao wanamajibu ya karaha hamna mfano,ukiwaomba wakuunganishe na ofisi ya undergraduate admissions wanasema haiwezekani, inashangaza!
  Nikaamua kuandika email kwa adress zao: vc@udom.ac.tz, dvc-pfa@udom.ac.tz nikiwaulizia maana mie ndo sponsor wa mdogo wangu,leo ni wiki mbili sijapata jibu. Nawasifu vyuo vya Ulaya na Marekani kwa upande wa info wako juu sana,ukiandika email unajibiwa within 24hrs hata wakichelewa ni 48hrs.........Wa tz hata kama tutaendelea ni kwa kuchelewa mno.
   
 16. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Bado watu wanaumwinyi ambao hautakiwi katika tanzania ya leo, hebu watu wabadilike! Mimi nawewe najua hatumo hata kama tumo kwenye hizo dhambi, lakini tunaweza kubadilika jamani! Unakuta mtu anataka kunyenyekewa wakati kaajiriwa kwenye hiyo kazi! Loh, sina mbavu kwakweli.
   
 17. n

  nndondo JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Mimi sikupi pole maana mambo mengine ya usumbufu tunajitakia,, watanzania tuache kupenda mikato wewe umeona wapi dunia hii chuo kikataka karatasi ya udhibitisho wa kiingereza toka chuo cha walimu wasiojua kiingereza? mengine tujipunguzie matatizo mimi nilifikiri unalalamika ukiritimbwa kwenye kupata hizo transcripts yaani ukiwa nje usitegemee kutuma mawasiliano ukapata cheti sahau ni mpaka uende mwenyewe physically ni ushenzi usiokua na kichwa hata kidogo na kama una opportunity yoyote mbele yako unaipoteza. Ushauri watanzania tujiandikishe na kufanya mitihani ya kimataifa ya qualifying tests hata kabla hujaomba chuo GRE na GMAT zina validity yamiaka mitano unachotakiwa kama kwa marekani ni pass ya 750 points kaa nayo kibindoni hakuna mtu atakaetambua hivyo vipeperushi vya watu wa communication skills kwanza enzi zetu ilikua ni kashfa mtu kusoma hiyo kozi ilihusishwa na wasiojua hata hicho kiingereza chetu mbuzi. Someni blog a ernest makulio jr juu ya how to get scholarships na fuatilieni media kwa kuwa yeye mwenyewe anaondoka California may 30 2010 kuja huko kwa mapumziko na kuwaletea habari za opportunities free of charge.
   
 18. F

  Fungu la kukosa Member

  #18
  May 30, 2010
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndugu Ngoshwe kwa hayo yaliokukuta. Wewe tukio hilo waliita Ufisaadi mimi nitapenda kutumia terminology ya "UKISUMA" yaani Udhulumati wa Kimasomaso na Udhaifishaji Maendeleo. Kwanza sioni mantiki ya mtu ambaye tayari ana shahada ya kwanza ambayo kaifanya kwa kutumia English kama medium of instruction na akafaulu kwa kiwango cha ima upper second au lower second au hata kama ilikuwa ni just a pass eti anapotaka kusoma Shahada ya Uzmili Kiingereza kiwe ni Big issue kwa uongozi wa chuo. Ni kweli kwamba vyuo vingi vya Uingreza na Marekani huweka mkwala kwa Muombaji atakaye kusoma Masters ikiwa tu degree yake ya kwanza kaifanya kwa kutumia lugha tofauti na Kiingereza. Muombaji huyo atalazimika kuonyesha ushaidi wa ufahamu wake wa kiingereza sambamba na sifa za degree yake ya kwanza. Inaelekea hapo UDSM kuna psycholocial theift under the control of senior managers through the so called loophole of " English Inefficiency" Nivizuri hao maafisa uchoro wa UDSM wakaelewa kwamba si kila mtu atakuwa ni mfuaswaha katika kuongea na kukiandika hicho kinachoitwa Kiingereza na wala kukiongea sio kigozo sahihi cha kuelimika. Wapo wanaoweza kukiongea lakini hawana uwezo wa kukiandika ipasavyo
  na wapo wanao weza kukiandika lakini hawana uwezo wa kukiongea. Hali hiyo ni very comon globaaly. Hata hapa Uingereza wapo wanafunzi kibao wa namna hiyo. Wazaliwa wa Uingereza lakini wana kiingereza kibovu wachilia mbali kukiandika. Imefika wakati wa wapuuzi hao kurekebisha mwenendo wao.
   
Loading...