UDSM chapinga kudahili vilaza, NACTE pia waipinga TCU

ENANTIOMER

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
1,419
804
16836687_1367829649954050_2152111161348238515_o.jpg
SIKU moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Baraza la Vyuo vya Ufundi Tanzania (NACTE).

Taarifa ya UDSM Kwa upande wake, UDSM kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga aliliambia gazeti hili jana kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.

“Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tulivyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza:

“Hiki ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi tunaowachukua, wote wanakuwa na sifa stahiki”, alisema Profesa Luoga alisema uhakiki ambao umefanywa na TCU na kutoa idadi ya wanafunzi 224 wanaosoma chuoni hapo, kuhakikisha wanawasilisha ushahidi wa nyaraka zao, wanaufanyia kazi, kwani kuna uwezekano tume hiyo haina taarifa kuhusu programu zinazoendeshwa na chuo hicho.

Alifafanua kuwa kuna baadhi ya programu maalumu, ambazo Serikali ya Tanzania imeingia na nchi nyingine kwa ajili ya kuendesha programu maalum.

Alisema kozi hizo zimekuwepo chuoni hapo kwa muda wa miaka 40 sasa na zinafanywa kutokana na makubalino ya Serikali ya Tanzania na nchi husika.

Alisema chuo hicho kikongwe Tanzania, kutokana na kuwepo makubaliano hayo kimekuwa kinapokea baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka nje ya nchi na akasisitiza kuwa yawezekana ndio hao ambao TCU imeshindwa kupata nyaraka zao.

“Yawezekana kuna taarifa ambazo hazijakaa sawa, tumepokea taarifa ya TCU sisi kama chuo ni jukumu letu kuitekeleza,” alieleza Profesa Luoga

Chanzo: Habari Leo
 
Mambo yanafanywa kiujanja ujanja tu.. watu wanajifanya wanajua zaidi kuliko wengine...
 
Kama UDSM isingekuwepo kwenye iyo list basi tungeshuhudia baadhi ya wanafunzi wa pale wakisumbua humu mtandaoni kwa kuwaita wenzao vilaza, ila kwa kuwa na wao wapo wametulia kimya mana wametoa idadi kubwa kuliko baadhi ya vyuo wanavyoviponda kila siku.HUJAFA HUJAUMBIKA.
 
Hata hivyo UDSM hakuna vilaza, ndio maana wao tu ndio wamenyoosha mkono na kupinga. vyuo vyenye vilaza vimeinamisha nyuso zao chini kwa aibu na woga.
 
Ila kwanini leo serikali (TCU) inafukuza wanafunzi ambao iliwadahili wao wenyewe?

Najiuliza sana:

1.serikali hakuona kuwa hawajakidhi vigezo vya kujiunga na elimu ya juu wakati inawafanyia udahili?

2.Hao wanaofukuzwa leo wako mwaka wa 3 bado semister moja amalize hawaoni kuwa tayari mtu ana degree bado certification ya chetu tuu?

3. Kuna waliopewa mkopo..wako mwaka wa 3 now , ukiwafukuza wanarudishaje mkopo? Manake huna kidhibiti cha kumbana tena....

My Take:

Hapa serikali ijilaumu yenyewe kwa uzembe, na watumishi wa TCU..

Busara zitumike kwa hao ambao wameshadahili na wana mkopo ww serikali..lakini pia wale wanaojilipia wameshaspend hela nyingi waruhusiwe wasome tuu...
 
2.Hao wanaofukuzwa leo wako mwaka wa 3 bado semister moja amalize hawaoni kuwa tayari mtu ana degree bado certification ya chetu tuu?
mtu akiwa mwaka wa tatu, kafaulu semester zote, huyo sio kilaza. tena wanamkosea heshima kusema hana sifa. wasio na sifa ni wale waliodisco.
3. Kuna waliopewa mkopo..wako mwaka wa 3 now , ukiwafukuza wanarudishaje mkopo? Manake huna kidhibiti cha kumbana tena....
kosa lilishafanyika na kwasasa busara itumike kwa hili. kama ni kilaza, basi angalia matokeo yake ya chuo, kilaza haana uwezo ya kumudu madesa yaa chuo.
 
Tunataka watendaji wanaojiamini kama hawa.
Prof.Luoga simamia haki
Wanasiasa wafanye Kazi zao za siasa mambo ya taaluma wayaache wafanywe na wenye taaluma husika
 
Hata hivyo UDSM hakuna vilaza, ndio maana wao tu ndio wamenyoosha mkono na kupinga. vyuo vyenye vilaza vimeinamisha nyuso zao chini kwa aibu na woga.
Kuna washona cherehani hapo eti textile engineering nakumbuka mwaka 2014 walichukuliwa hadi wenye daraja la nne,jamaa yangu alipoomba chaguo la kwanza alitemwa kwenye vyuo kama DIT,MUST na vingine akaomba hapo akapata na four yake, mimi huwa namuita kilaza kila siku japo yeye ananiambia kuna four wenzake wapo nao.
Labda sijui tafsiri ya kilaza naomba unieleweshe pia uje uwasafishe hao washona cherehani.
 
Kama UDSM isingekuwepo kwenye iyo list basi tungeshuhudia baadhi ya wanafunzi wa pale wakisumbua humu mtandaoni kwa kuwaita wenzao vilaza, ila kwa kuwa na wao wapo wametulia kimya mana wametoa idadi kubwa kuliko baadhi ya vyuo wanavyoviponda kila siku.HUJAFA HUJAUMBIKA.
Hujazaliwa kuwa great thinker.sasa umeongea nin na unajadili topic ipi? Badilika.
 
Back
Top Bottom