Blank page
JF-Expert Member
- May 28, 2015
- 4,728
- 3,173
Umeenda nje,ya mada mkuu.Mkuu na wewe jina lako lipo?mana naona kama umedata, soma maelezo yangu upya.
Umeenda nje,ya mada mkuu.Mkuu na wewe jina lako lipo?mana naona kama umedata, soma maelezo yangu upya.
Hata hivyo UDSM hakuna vilaza, ndio maana wao tu ndio wamenyoosha mkono na kupinga. vyuo vyenye vilaza vimeinamisha nyuso zao chini kwa aibu na woga.
unakanusha kwa maneno au kwa kukupeleka vyeti vihakikiwe,, tuliwahi siku nyingi humu kusema kuhusu udahili wa hovyo unaofanywa hapo udsm tukatukanwa leo ukwel uko adharani ..waache maneno wapeleke vyeti & then wakishahakikiwa watoke hadharani waseme .Hata hivyo UDSM hakuna vilaza, ndio maana wao tu ndio wamenyoosha mkono na kupinga. vyuo vyenye vilaza vimeinamisha nyuso zao chini kwa aibu na woga.
ulishasema ni fundi sherehani, sasa unataka achukuliwe mwenye division one kwenda kusomea ufundi cherehani!Kuna washona cherehani hapo eti textile engineering nakumbuka mwaka 2014 walichukuliwa hadi wenye daraja la nne,jamaa yangu alipoomba chaguo la kwanza alitemwa kwenye vyuo kama DIT,MUST na vingine akaomba hapo akapata na four yake, mimi huwa namuita kilaza kila siku japo yeye ananiambia kuna four wenzake wapo nao.
Labda sijui tafsiri ya kilaza naomba unieleweshe pia uje uwasafishe hao washona cherehani.
Cha kwanza ni kukanusha uzushi na kuomba umma upuuze uzushi huo wa TCU. Hatua kali zitachukuliwa dhidi ya hao wazushiunakanusha kwa maneno au kwa kukupeleka vyeti vihakikiwe,, tuliwahi siku nyingi humu kusema kuhusu udahili wa hovyo unaofanywa hapo udsm tukatukanwa leo ukwel uko adharani ..waache maneno wapeleke vyeti & then wakishahakikiwa watoke hadharani waseme .
muda ni shaidi mzuri tusubiri tutapeana mrejesho.Cha kwanza ni kukanusha uzushi na kuomba umma upuuze uzushi huo wa TCU. Hatua kali zitachukuliwa dhidi ya hao wazushi
ukiona kimya kwa muda mrefu, ujue TCU walikua wanataka kuandikwa kwenye magazeti tu. midomo yao ulikua umeanza kuchachamuda ni shaidi mzuri tusubiri tutapeana mrejesho.
mtu akiwa mwaka wa tatu, kafaulu semester zote, huyo sio kilaza. tena wanamkosea heshima kusema hana sifa. wasio na sifa ni wale waliodisco.
kosa lilishafanyika na kwasasa busara itumike kwa hili. kama ni kilaza, basi angalia matokeo yake ya chuo, kilaza haana uwezo ya kumudu madesa yaa chuo.
inauma sana, hizi namba tunazosomeshwa zimeanza kukeraSiku hizi kila mtu anatamani kuonekana amebuni kitu kipya ili aonekane anampendeza baba mwenye nyumba.Bahati mbaya sana kila wanalokuja nalo daah mpaka aibu.Kaja mtu na madawa ya kulevya,mara mashoga nk.Hata wa wale wa bodi ya mkopo wamekuja na asilimia 15,bila kujali take home ya mtu.Kuna jamaa alijikuta anarudi na 90,000 tu katika mshahara wake.Nikweli bodi watakuwa wamepata hela yao,familia kilio,je ufanisi kazini itakuwaje? atafanya kazi huyo? yaani ni shida tupu.
Mimi naangalia hata wabunge wetu nao sijui.
Kama umekiri kuwa mafundi cherehani ni vilaza basi kubali kuwa UDSM vilaza wapo mana wanafunzi wa textile engineering ni sehemu ya UDSM over.ulishasema ni fundi sherehani, sasa unataka achukuliwe mwenye division one kwenda kusomea ufundi cherehani!
Tatizo lake huyo dogo alijiona kipanga akaomba kozi tofauti na ufundi chelehani hapo DIT. kama angeomba ufundi cherehani, asingekosa. ufaulu wake ulikua ni wakusomea ufundi cherehani au kwenda upolisi.
JIULIZE
kwanini UDSM hawakumchagua ktk kozi ya maana kama CIVIL ENG. badala yake wakamchagua ktk kozi ya UFUNDI UCHEREHANI?
UDSM hawajawahi kua na vilaza hata mwaka mmoja. kama wagekua wanapokea vilaza, basi Jesca Kilaza (yule mtoto wa dakitari) asingekimbilia shamba la bibi, wakati baba, mama na familia yake kwa ujumla walikua wanaishi Dar. Angejiunga UDSM.Kama umekiri kuwa mafundi cherehani ni vilaza basi kubali kuwa UDSM vilaza wapo mana wanafunzi wa textile engineering ni sehemu ya UDSM over.
huyu jamaa hakawiagi. napenda sana alivyo mkweli. hana ile hali ya kukurembaremba na kusifia pumba.:’Kuchezea elimu ya Tanzania ni hatari zaidi ya dawa za kulevya’ -Bashe
Moja ya habari kubwa hivi sasa Tanzania ni pamoja na hatua ya Serikali kupitia TCU kutoa orodha ya majina ya baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wasio na sifa za kuwa wanafunzi wa vyuo.
Badhi ya watu na taasisi mbalimbali kikiwemo chuo kuku Dar es salaam UDSM kilichoikataa orodha hiyo. Kwenye Exclusive interview ya Ayo TV na millardayo.com tunaye Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe ambaye na yeye ametoa ya moyoni baada ya kuiona taarifa hiyo huku akisisitiza kuwa Serikali imefanya makosa.
Bashe amesema…>>>’Tunatatizo kubwa la mfumo wa elimu kwenye nchi yetu, toka nimekuwa na ufahamu na kufuatilia mambo nimeona kila Waziri amekuwa akija na movie yake, ukijiuliza swali nani aliwadahili hawa wanafunzi jibu ni TCU‘ –Hussein Bashe
‘Leo mwanafunzi amekaa chuoni na katumia gharama nyingi achilia mbali matarajio yake aliyojiwekea na familia yake alafu unaenda kuzima mshumaa wake, tujiulize mara ya kwanza wakati wanadahiliwa walikuwa na sifa alafu sasa hawana sifa?‘ –Hussein Bashe
‘Hii inatafsiri kwamba mfumo wetu wa elimu unatatizo kubwa lakini la pili wakati unawaadhibu wanafunzi hao kwa kuwaita hawana sifa aliyewadahili umewachukulia hatua gani? leo chuo kikuu Dar es salaam wametofautiana na TCU na umeona‘ –Hussein Bashe
‘Mimi nasema kama Mbunge kwamba hili jambo la kuchezea elimu ya nchi hii ni hatari mno kuliko hata dawa za kulevya, kuifanya elimu hii kama ni sehemu ya kuifanyia majaribio ni hatari‘ –Hussein Bashe
‘Tumekuwa ni watu wa kusukumwa na matukio, Moja kati ya mtu aliyekuwa nilikuwa na matarajio makubwa sana kwenye nchi hii ni Profesa Joyce Ndalichako lakini siku zinavyokwenda naona kama anashusha viwango vya elimu ya Tanzania huyu ni mama ninayemuheshimu lakini kwa hili hatuwezi kucheza na elimu ya nchi hii‘ –Hussein Bashe
‘Mimi nataka nitumie fursa hii kumweleza Rais Magufuli kwamba anakila sababu ya kuwatazama watendaji wake aliyowaamini, anaweza kuwa na nia njema pamoja lakini chakutazama ni je, amewapa watu sahihi kwenye hizo nafasi?‘ –Hussein Bashe
Vipi kuhusu TCU kudaiwa kutaja majina ya wanafunzi ambao hawapo vyuoni? Bashe amesema>>’Hii inaleta tafsiri kwamba ukurupukaji uliopo ndani ya Serikali, hakuna lugha nyingine unaweza tumia na suala la kudahili ni kazi ya vyuo na TCU wao wanafanya kazi ya udalali na ni mambo ya kukurupuka‘ –Hussein Bashe
huyu jamaa hakawiagi. napenda sana alivyo mkweli. hana ile hali ya kukurembaremba na kusifia pumba.
kosoa mheshimiwa ili wajirekebishe, sio kupiga meza na kusema ndioooooo
We jamaa sio mzima kichwani, textile engineering wachukue div 4 hebu punguza chumvi mkuu.Kuna washona cherehani hapo eti textile engineering nakumbuka mwaka 2014 walichukuliwa hadi wenye daraja la nne,jamaa yangu alipoomba chaguo la kwanza alitemwa kwenye vyuo kama DIT,MUST na vingine akaomba hapo akapata na four yake, mimi huwa namuita kilaza kila siku japo yeye ananiambia kuna four wenzake wapo nao.
Labda sijui tafsiri ya kilaza naomba unieleweshe pia uje uwasafishe hao washona cherehani.
Hakuna lolote, katika awamu tuliyowahi kua na watu wakurupukaji ni awamu hii peke yake, hasa huyu Ndalichako sijui PhD yake kama ni halali.muda ni shaidi mzuri tusubiri tutapeana mrejesho.
Kwani hajapata listi?SIKU moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Baraza la Vyuo vya Ufundi Tanzania (NACTE).
Taarifa ya UDSM Kwa upande wake, UDSM kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga aliliambia gazeti hili jana kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.
“Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tulivyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza:
“Hiki ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi tunaowachukua, wote wanakuwa na sifa stahiki”, alisema Profesa Luoga alisema uhakiki ambao umefanywa na TCU na kutoa idadi ya wanafunzi 224 wanaosoma chuoni hapo, kuhakikisha wanawasilisha ushahidi wa nyaraka zao, wanaufanyia kazi, kwani kuna uwezekano tume hiyo haina taarifa kuhusu programu zinazoendeshwa na chuo hicho.
Alifafanua kuwa kuna baadhi ya programu maalumu, ambazo Serikali ya Tanzania imeingia na nchi nyingine kwa ajili ya kuendesha programu maalum.
Alisema kozi hizo zimekuwepo chuoni hapo kwa muda wa miaka 40 sasa na zinafanywa kutokana na makubalino ya Serikali ya Tanzania na nchi husika.
Alisema chuo hicho kikongwe Tanzania, kutokana na kuwepo makubaliano hayo kimekuwa kinapokea baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka nje ya nchi na akasisitiza kuwa yawezekana ndio hao ambao TCU imeshindwa kupata nyaraka zao.
“Yawezekana kuna taarifa ambazo hazijakaa sawa, tumepokea taarifa ya TCU sisi kama chuo ni jukumu letu kuitekeleza,” alieleza Profesa Luoga
Chanzo: Habari Leo
Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tulivyompa,” alisema Profesa Luoga
Mwaka 2014 ilikuwa ata mtu mwenye four anakuwa amekidhi vigezo vya kuingia University mana mfumo uliotumika ni wa tofauti kipindi kile three iliishia point 13.We jamaa sio mzima kichwani, textile engineering wachukue div 4 hebu punguza chumvi mkuu.
Kozi yoyote inayoitwa engineering ukitaka kuisoma lazima unywe maji kwanza