UDOM ndiyo chuo bora Tanzania

UDOM ndiyo chuo bora Tanzania

..Inaonyesha kabisa hujui sifa ya Chuo bora na kama ulikua hujui Mkuu,hamna chuo kinachotoa Elimu bora kuliko kingine hapa Tanzania Its all the same na sitafuti kujifariji najua ukweli upo wapi!!
Sweet Lord!!!!!!!!! Kweli UDOM ni *****
 
The university of Dodoma.
Embracing knowledge.
[HASHTAG]#imeeleweka[/HASHTAG] mkuu.
 
Yani ubora wa chuo unapimwa kwa kuangalia vigezo ivyo??? tuliwahi sana kumuondoa Mzungu for sure
 
Zipo sababu Nyingi unaweza kutumia kupima Ubora wa kitu Lakini kikubwa ni Kwamba Kifit Preferences Nyingi za kuweza kuitwa Bora and UDOM Fits most of those Preferences!!

1.MAHALI(LOCALITY)
Kipo dodoma ambayo ndo Habari Ya mjini sasa Hivi alaf Geographically kama tunavyojua dodoma Ipo katikati Ya Tanzania hivo Usafiri sio changamoto kwenda Muda wowote unaotaka kwenda Plus Fact Ya Kuwa dodoma Is Now Growing kinaipa Fursa Kubwa sana in terms Of services.

2.GHARAMA ZA MAISHA(COST OF LIVING)
Unlike Vyuo karibia Vyote Tanzania UDOM Ina cost ndogo za Maisha,tukianza Na Fact kuwa Kuna Hostels Mia Kidogo za wanafunzi kulala where u Just pay 5oo/- kwa siku which is More than Enough,alaf misosi Yenyewe Iko cheap Kinyama Yaan starting from 1ooo/- ambapo Unakula na kushiba Kabisa kuna villages za wajasiriaMali along the university ambapo unapata vitu mbalimbali kwa Bei Ya Nyanya.

3.VIFAA VYA KIMASOMO(EDUCATION FACILITIES)
Kila College Ina Maktaba Yake na Labaratories ambapo unakuta Materials mbali mbali za considering the Fact Kuwa ni cha Juzi Juzi Facilities Bado zipo katika Ubora wake Unlike Vyuo Tangia enzi za Nyerere na Mitaala Ya nchi Hii inayobadilika havipo Updated Kabisa,na due to wingi wa Colleges ukipita Kila Maktaba hutakosa unachotafuta.Pia kuna Buses za Chuo Just Incase kuna Trip Yoyote

4.VIFAA VYA KIMICHEZO+RECREATION
Kila college Ina kiwanja chache cha Mpira,basketball na Volleyball infact vya hii michezo ni viwili viwili ni some colleges na Mpka tennis courtYards Pia zipo nets,mipira na Facilities zingine sitaki kuongelea Maana huwezi Kujenga viwanja viwili viwili alafu ukakosa Mipira,Kuna Club Kuntu pale Humanities kwa wale wapenda Bata,kuna swimming Pool pia Just costs 3000 kwa wanafunzi

5.MADHARI(ENVIROMENT)
Udom Ina Mazingira Bora sana especially kuanzia February to september kuna milima na mabonde Ya kutosha tu kifupi the view is Just Perfect,na kutokana na baridi Ya usiku hamna mbu kabisa,kimajengo sihitaji kuongelea maana watu wanasomea kwenye Bunge la zamani alaf Yapo mengi Mpka Yanazidi Mengine Yanaazimwa kabisa na serikali

5.UMBALI KUTOKA MJINI.
Sio zaidi Ya 8km nauli ni 400 na mabasi Yapo pale pale Chuo kwaio Usafiri sio Kero hata kidogo any time Of the day unafika tu Pale chuoni without hurting ur head Yaan huwazi sana

6.QUALITY YA ELIMU.
Ipo kawaida tu kama chuo chochote Kile hapa nchini kuna lectures wa kutosha na Pia kuna hata new courses zimeanzishwa hapa ambazo huzipati kwenye vyuo vingi Tanzania baada ya serikali kuona haja alaf Pia masomo kama chinese ni Free kabisa kusoma no Charges wachina wapo pale wanafundisha and people Go to china every Now and Then
Sijawahi kuamini hiki ni chuo kweli
 
Jamani mbona mapaka sasa hivi Udom hawajatoa joining instructions ili tukajiandaa mapema
 
Naipenda udom ule upande wa IT tuu, kweli nimeona product bora zenye impact kwenye jamii. sehemu nyingine sijui.
 
Najiuliza tu hapa,hv chuo bora kinadahili ******? Rejea kauli ya jpm,chuo bora kina mgomo wa wahadhiri? Chuo bora kinachelewesha fedha za wanafunzi kila siku had wanagoma na kupigwa na ffu?chuo bora kimezuiwa kudahili prog ya md medicine? Chuo bora hakina hta prospectus online? Hadi kuna thread ililetwa humu mtu analalamika haoni prospectus online? Je chuo bora kinaazima wahadhiri toka vyuo vingine vikuu mfano udsm? Chuo bora mkuu wake hana msimamo anaagizwa adahili ****** na anafanya? Chuo bora kinatawaliwa na siasa hadi baadhi ya taasisi za serikali zinaomba kutumia majengo yake kma ofisi ktk safari ya kuhamia dodoma?..........kiufupi ukiweza kujibu maswali yote haya ndo uje tuongee sasa
Kweli na ww umechanfanyikiwa ubora wa chuo ni kutogoma au prospectus kuwekwa online?? Mhu halaf nan kakuambia kuna chuo ambacho hakiazim wahadhir Tanzania hii!!af unaijua sbb ya kutochukua MD mwak huu au unafuata mkumbo!!
 
Kusifia sehemu uliyosoma ni kawaida kwakuwa ata kama kuna mabaya na mazuri yapo pia ambayo yalikufurahisha, ila kwenye ukweli haina haja ya kumumunya maneno, ukitaka kujua udom ni vigumu sana kukitetea we maliza vizuri alafu nenda kwenye kazi ya kupita kwa interview, kama hiyo course uliyosoma utakuta wanafunzi kutoka UDOM, SUA, MZUMBE, MUHIMBILI we jua tu ushakuwa fungu la kukosa labda utumie alternative ingine

Mwisho wa siku mtoa mada yuko sawa kulingana na mawazo yake, ila tatizo lake yeye hataki mawazo ya wengine anataka anachokiamini yeye ndo iwe hivo ilhali aliandika hii thread akiwa kashiba tu ugali na amekaa hostel ghorofa ya 4 akaona atililike, ikiwa hajafanya research yoyote ya kulinganisha ubora wa elimu na vyuo vingine

Hao walioweka ranking ya vyuo na kuweka udom ya 5 Tz na 185 kwa Africa hawakuendeshwa na mahaba kama huyu mtoa mada, bali wanafanya research na wanatumia vigezo vyao ili makelele University iwe mbele ya University of South Africa

Penda ulichonacho maana kuna wanafunzi wa Kampala University nawao wanaamini chuo chao ni bora kuliko vingine hapa Tanzania
 
Jamani mbona mapaka sasa hivi Udom hawajatoa joining instructions ili tukajiandaa mapema
Usiwe na was was bro itawekwa tuu mtandaon !chuo kinafunguliwa tareh 29/10!! Udom inawanafunz weng sana so itakuwa wapo kweny utaratib wakuingiza registration namba zenu ili ukifika chuo usipate shda
 
INFACT UDOM NI CHUO AMBACHO NI KICHANGA LAKIN KWA SKU ZA USONI KINAENDA KUWA CHUO KIKIBWA SUALA LA UD AU MUHIMBILI KUWA NA RESEACH NYINGI NI SABAB NI VYUO VYA ZAMZN TANGU 1961 TOFAUTI NA UDOM CHUO CHENYE MIAKA TISA HADI SASA...........................
 
Ivi mlishawai kufikilia maisha baada ya chuo, mkikua mtaacha kubishania kipi chuo kizuri na hasa pale unapomaliza chuo ambacho wewe unakiamini ni kizuri alafu unasugua mitaani haliyakua best wako ambaye alisoma chuo cha ajabu ambacho ulikua ukijui kama na chenyewe ni chuo kikuu ulikua unahisi kam banda fulani la mifugo lakini mchizi wako ndo vile kapata kazi kupitia ako ka degree chake ambacho wewe hukitambui ila TCU wanakijua.
Sio siri mnanifurahishaga saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana.
 
Back
Top Bottom