UDOM kufungwa tarehe 4.6.2012

Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
646
415
Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma,Profesa Kikula,ameahidi kukifunga chuo ikifika tarehe hiyo bila bodi ya mikopo kutuma hela za chakula.Wanafunzi Udom walitakiwa kupewa hela hiyo tarehe 3.5.2012 lakini hadi leo bado hawajapata na hawajui inaingia lini.

Taarifa hizo zinakuja wakati kukiwa na taarifa kuwa hazina ya serikali imekauka na hakuna hela.Wanafunzi hapa Udom katika vitivo vyote hali yao kiuchumi ni mbaya sana,isipokuwa kitivo cha afya ambao wao muda wa kupewa bado kidogo.
 
poleni sana wana udom na itakuwa ni busara kwa mkuu huyo kufanya hivyo kwani kufa hamtakufa ila cha moto mtakiona mpaka ifike tarehe hivyo.
 
Du wasomi nasikia wasomi wa ngongona wanashindia viazi na mihogo poleni ndugu zetu
 
kama mmeweza kuvumilia siku hizo zote fanyeni kuvumilia na mda uliosalia
 
sasa nimeelewa vizuri wale vijana wa UDOM kwaanini walikimbilia wali wa sisiemu ,

poleni wadogo zangu
 
Mbona udsm huwa wanapewa hela hata kabla ya chuo kufunguliwa??mmendekeza sana magamba sasa washawadharau
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom