UDOM inakera!

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Ni takribani miezi minne sasa tangu mahafari ya kwanza ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ifanyike na kuhudhuriwa na mkuu wa nchi ambaye pia alitunukisha Shahada ya uzamivu. Lakini inasikitisha kuwa hadi sasa wahitimu hao hawajapewa Transcripts zao. Hali hiyo imewasababishia usumbufu mkubwa kwani wanashidwa kutafuta ajira au kupandishwa madaraja/vyeo makazini kwao. Kila waulizwapo kuhusu hilo hutoa majibu rahisi tu -subiri wiki ijao, subiri mwezi ujao nk. Mamlaka zinazohusika zisaidie ili wahitimu hao wapate haki yao.
 
Back
Top Bottom