tisa desemba
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 434
- 115
Wakuu suala la ukosefu wa maji hapa udom college of education limezidi kushika kasi hasa kwa wiki hii, maji yamekuwa yakitoka kwa nadra sana tena katika block chache sana (si zaidi ya 4 kati ya 20 zilizopo) nyakati za asubuhi na jioni wanachuo wengi wamekuwa wakizunguka huku na huku kutafuta maji bila mafanikio! Vyooni hali si nzuri! Nyuma ya block R, M, J na D nimeshudia vinyesi vya binadamu vikiwa vichakani! Tunakolekea si kuzuri! Serikali ya wanafunzi wako kimya! Naomba wakuu wa Udom mnaopitia hapa msaidie kutatua tatizo hili kwani ikiendelea hivi wikiendi hali itakuwa mbaya zaidi! Naomba kutoa hoja!