Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Mama sidhani kama hii ni factor, unless kama tunataka kuleta yale ya Kenya ambako wakikuyu wanadai haki ya kutawala Kenya kwa vile maumau mengi walikuwa wakikuyu.

si unaona mwenyewe wakikuyu walivyodominate siasa za kenya?
 
Mzee Mwanakijiji,

Hili ndilo najaribu kuliongelea hapa, tukianza kwenye dini za watu, tutaenda zaidi na kuanza kuangalia vipande na migawanyiko kwenye hizo dini. Kwa waislam, tutaanza kuangalia nani ni shia na nani ni sunni, kwa wakristo tutaanza na protestants na wakatoliki.

Kwa ukabila, hata tukianza na wachagga, tutaenda kwa warombo, machame na kadhalika, hii itaendelea na haitakuwa na mwisho. Nasisitiza kuwa binafsi sijali kabisa kama viongozi wote wa ccm watakuwa waislam kama vile nisivyojali kama viongozi wote wa UDP watakuwa wasukuma.

Utendaji na ubora ndio viwango, na hili inabidi liangaliwe na wote, wanaccm wanaoita vyama vingine kama vyama vya kidini au kikabila na wale wapinzani ambao wameanza kukiita ccm kama chama cha kiislam. Hii itafikia hatua hata viongozi wataogopa kufanya jambo kama hilo la mahakama ya kadhi ingawa lilikuwa kwenye kampeni yao kwa kuogopa kuwa wataitwa wadini.

Aibu kubwa sana.
 
Mzee wa falsafa ya messenge sent si mmemtimua

Mbowe namuogopa kwa kweli CHAMA choka mbaya anakikopesha fwedha harafu anang'ang'ania kuruka na helkopita harafu wanakuja kukidai CHAMA milion 700.Hii hajatulia kabisa

Tutoeni emotion tuliangalie swala hili.kwa makini ni swala nyeti.
 
Acha kutwist point, hii nchi imepiganiwa uhuru na waislamu?je wengi waliokuwa na mwamko na siasa na kugombea uhuru ni waislamu? sijui nauliza tu?

Unauliza swali au unasema fact? mimi sidhani kama nchi hii imepiganiwa uhuru na watu wa dini yoyote ile. Kama wewe unaamini kuwa waliopigania uhuru ni waislam basi elewa kuwa mimi naamini tofauti na wewe kwenye hili.
 
Mimi mambo ya udini siyajui na historia sijasoma; nimeuliza swali na nimekuuliza wewe.
 
Mama,

I dont think you are about to write what I think, Are we rewarding freedom fighters right now in this country? the Zimbabwe way?

ohh my GOD, a very long way to go.
 
Mimi mambo ya udini siyajui na historia sijasoma; nimeuliza swali na nimekuuliza wewe.

Na mimi nimekujibu tayari kuwa waliopigania uhuru hawakuwa na dini yoyote ya kigeni au influence ya dini za kigeni - uislam au ukristo. Walipigania uhuru kama waafrika wenye uchungu na ardhi na malighafi zao.
 
naomba supporting facts za jibu lako.
 
kwa hiyo hicho kichwa cha topic ni cha kukurupuka tu hakina base?

Haya yaweza kuwa maoni yako na una kila haki ya kutoa maoni yako kwa kadri yoyote unayotaka. Suala la kuwa na viongozi wengi wa kiislam ndani ya ccm kuliko wakristo ni suala ambalo Kikwete ninamshauri hapa kuliangalia.
 
Kichwa cha hii topic hazina base? uliota hilo suala na kuja kufungua thread?

Kikwete atalingaliaje wakati wale ni viongozi wa kuchaguliwa? au unataka aitishe kikao awafukuze?
 
Kichwa cha hii topic hazina base? uliota hilo suala na kuja kufungua thread?

Kikwete atalingaliaje wakati wale ni viongozi wa kuchaguliwa? au unataka aitishe kikao awafukuze?

Labda nikuulize hili swali wewe.

Wewe unafikiria afanyeje?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…