Udikteta mara nyingi hautarajiwi!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,990
22,523
Udikteta mara nyingi hautarajiwi. Udikteta mwingine, ulianza kwenye maeneo ambayo watu tayari ni wenye mafanikio, wenye elimu na wakulima ambao walionekana salama kuweza kufanikiwa bila ya uhitaji wa kuingia kwenye mfumo wa udikteta - Ulaya, Asia na Amerika ya Kusini ni mifano halisi.

Mfano Ujerumani ya Hitler, mojawapo ya matukio makubwa zaidi kwenye historia ya dunia.

Kufikia mwisho wa karne ya 19, Ujerumani ilionekana kuwa na mfumo bora zaidi wa elimu duniani. Kama mfumo wowote wa elimu ungeweza kuwaepusha watu dhidi ya uharibifu wa udikteta, hakika Ujerumani ingekuwa imeonyesha njia. Ilikuwa na elimu bora kuanzia chekechea. Shule za sekondari zilikazia sana mafunzo ya kitamaduni. Wajerumani walitengeneza vyuo vikuu vya kisasa vya utafiti.

Wajerumani walikuwa wanajulikana hasa kwa mafanikio yao katika sayansi - fikiria tu...

  • Karl Benz ambaye aligundua gari linalotumia petrol,
  • Rudolf Diesel ambaye alivumbua “compression ignition engine",
  • Heinrich Hertz ambaye alithibitisha kuwepo kwa mawimbi ya umeme,
  • Wilhelm Conrad Rőntgen aliyeunda mashine ya x- rays,
  • Friedrich Agosti Kekulé ambaye alianzisha nadharia ya muundo wa kemikali,
  • Paul Ehrlich ambaye aligunduwa dawa ya kwanza kutibu maradhi ya syphilis,
  • bila shaka, mwanafizikia wa kinadharia Albert Einstein.
Haikushangaza hata kidogo, kwa wasomi wengi wa Marekani, ambao wengi wao walienda chuo kikuu cha Ujerumani kwa digrii zao wakati wa karne ya 19.

Baada ya Vita Kuu ya Dunia, uandikishaji wa chuo kikuu cha Ujerumani uliongezeka. Mnamo 1931, idadi hiyo ilifikia 120,000 dhidi ya 73,000 kabla ya vita. Serikali ilitoa ushuru kamili na malipo kwa wanafunzi masikini wasio na uwezo.

Serikali ilisomesha watu wake bure kwa ngazi ya chuo kikuu, vitabu vyake ilikuwa ni bure. Na mahitaji mengine muhimu, mfano nguo, matibabu, usafiri na tiketi za kwenda kuhudhuria maonyesho na matamasha. Mwanafunzi alikuwa anapatiwa punguzo kubwa la bei nk, Pia walipatiwa chakula cha kutosha.

Wakati kulikuwepo na chokochoko za wajerumani dhidi ya wayahudi(anti-Semitic agitation), mwishoni mwa karne ya 19, Ujerumani haikuonekana kuwa ni mahali ambapo chuki hiyo inaweza kukua. Warusi hata hivyo, mambo yalikuwa tofauti. Walikuwa wakipambana na Wayahudi kwa kuwabagua, kuwapiga na kwatesa kwa miongo kadhaa.

Utawala wa Bolshevik wa Russia uliendeleza ubaguzi na chuki. Karl Marx na yeye chuki zake kwa wale "bourgeoisie", ambao alidai ndiyo wameleta matatizo na shida zilizomo kwenye jamii. Lenin na mrithi wake Stalin walisisitiza falsafa hiyo zaidi, ya kuwaangamiza wanaoitwa "matajiri" ambao hata hivyo, baadaye ilikuja kugundulika kuwa wengine ni wakulima na wana ng'ombe mmoja tu.

Kwa nini, Wajerumani wenye ujuzi walikubaliana na kichaa kama Adolf Hitler? Jibu fupi ni kwamba sera mbaya zilisababisha matatizo ya kiuchumi, kijeshi na kisiasa – recipee for tyranny. Wananchi walikuwa wamechoshwa na sera ambazo hazikuwa zinawapatia maendeleo wanayoyataka. Hata kwa upande wetu sisi, wananchi wengi wamechukizwa na shida na umasikini tulio nao, lakini ni sera mbovu ama pengine viongozi wabovu ndiyo wamesababisha tuwepo hapa tulipo. Na matatizo tuliyonayo, yamesababishwa na haohao wanaojidai kuwa wanataka kuyatatua, na sasa wananchi walio wengi, wamelishwa matango pori kuwa adui wao ni matajiri pamoja na upinzani. Yani hao ndiyo wanaonekana ama viongozi wetu wanataka waonekane kuwa ndiyo waliosababisha umasikini wa wananchi.
Tukirudi Ujerumani, hali ndani ya nchi ilizidi kuwa mbaya, kisiasa, kiuchumi na matatizo megine ya wananchi. Na watu walikasirika vya kutosha, wakati mwingine watu watasapoti vichaa ambao katika mazingira ya kawaida, wasingeweza kupata hata mtu wa kuwasikiliza.

Kama ilivyokuwa kwa vikosi vingine, Wajerumani waliingia katika Vita Kuu ya Dunia na matumaini ya kuwa watashinda na kuwalipisha gharama zote za vita hao watakaoshindwa vita.Serikali ya Ujerumani iliweza kuwaaminisha wananchi wake kuwa watashinda vita, hivyo kila mtu alishangaa wakati mambo yalipokuja kuwa tofauti. Rais wa Umoja wa Mataifa na pia marekani kwa wakati huo, mr. Woodrow Wilson alitoa hotuba inayoelezea mawazo yake ya juu hoja zake ambazo zilikuwa maarufu kama “14 points ama "Pointi 14," ambapo Wajerumani walitarajia mazungumzo ya amani. Lakini washirika wa Uingereza na Ufaransa – Washirika wa marekani - walikuwa wameamua kulipiza kisasi kwa hasara ambazo walizipata, na hivyo kuweka mikataba ya kuwalazimisha Wajerumani kulipa, ambao walichukia na kuhisi kwamba wamesalitiwa. Wakuu wa majeshi wa Ujerumani walitambua kwamba kila mtu aliyetia saini hiyo armistice angechukiwa na wananchi, kwa hiyo wakajiuzulu na kuwaacha maafisa wa kiraia kutia saini (ambaye hatimaye alikuja kuuwawa). Matokeo yake, jamhuri ya Weimar ilitambuliwa.

Hitler alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakipingana dhidi ya serikali ya Weimar. Alijiunga na chama cha Wafanyakazi wa Ujerumani. Chama ambacho mnamo Februari 1920, kilibadilishwa na kuwa National Socialist German Workers’ Party(NSDAP), ambapo baadaye kilifupishwa na kuitwa NAZI.

Chama kilichokuwa kikijinasibu na uzalendo, utaifa, ujamaa, kupambana na Uyahudi na kupambana na ubepari. Nyakati hizo, mwanahistoria wa Ujerumani Oswald Spengler aliwashawishi wananchi pale alipokuja na wazo lake la "ujamaa wa Prussia."

Kipaji kikuu cha Hitler, kilionekana kuwa kama ni utunzi, na pia alikuwa mwandikaji mzuri sana wa hotuba, hivyo alianza kutoa hotuba zilizowavutia Wajerumani ambao walikuwa wamekatishwa tamaa na matokeo ya vita kama ambavyo sisi tumekatishwa tamaa na matokeo ya ufisadi na wizi wa mali za umma na mikataba mibovu. Aliwakataa na kuwapinga Wayahudi, matajiri na mabepari, pamoja na "wasaliti" wengine waliotajwa kama vile inavyoonekana kwenye taifa letu ambapo “Taifa la wazalendo na wachapakazi” linajengwa, wao wajerumani, waliapa kuujenga ukuu wa Ujerumani.

Mwanahistoria Ian Kershaw alisema kuwa "kama siyo kushindwa kwa vita, mapinduzi, na hisia nyingi za udhalilishwaji wa taifa lao, Hitler asingeweza kuwa chochote na wala asingepata nguvu na kukubalika kama ilivyotokea.."

Baadaye, mambo yalizidi kuwa mabaya kutokana na mfumuko wa bei. Upande ule wa washindi, ulidai kwamba Ujerumani walitakiwa kutoa malipo makubwa, inaonekana walifikia maamuzi hayo bila ya kufikiri kwa kina ni kwa jinsi gani na ni wapi Wajerumani watapata kiasi hicho cha pesa. Vikwazo vya kibiashara vilisababisha ugumu zaidi kwa makampuni ya Ujerumani yaliyokuwa yakitegemea kupata pesa kupitia export au mauzo ya nje. Ushuru barani Ulaya kwa ujumla, ulipanda mara tatu zaidi, na ulikuwa zaidi ya 800% kuliko viwango vilivyokuwepo kabla ya vita.

Serikali ya Ujerumani ilishindwa kufikia makubaliano yale ya malipo. Ilipofikia Januari 1923, Wafaransa waliamuwa kuwalazimisha Wajerumani walipe kwa kupeleka askari eneo liloitwa “Ruhr”, sehemu ambayo ilikuwa imeshehena viwanda vikubwa vya wajerumani.Kwakifupi, ndipo industial sector yao ilipokuwa located. Serikali ya Ujerumani ilijibu kwa kutoa na kuwapa ruzuku wale waliokuwa wakipingana na wafaransa. Hayo yalishababisha mapungufu kwenye bajeti ya wajerumani(budget deficits went higher). Kwetu tunaona pia upendeleo kwa watu wa mkulu pamoja na chama, pia matumizi yanayotumika kununua wapinzani, what for?

Kwa upande mwingine, malipo wajerumani waliyotakiwa kuyalipa baada ya vita yalikuwa makubwa sana na ya kutosha kuwaumiza. Lakini pia walikuwa na hali mbaya sana ya kifedha. Karibu asilimia 90 ya matumizi ya serikali ya Ujerumani yalitumika kwa urasimu mkubwa, mipango ya jamii(welfare state), biashara zenye kuingiza hasara, na taasisi nyingine. Serikali ya Ujerumani ilitoa ruzuku kwa manispaa na majiji ili kuweza kusaidia...Ujerumani ilikuwa na mfumo wa pensheni kwa Jamii. Serikali ya Ujerumani ilitoa bima ya afya kwa mamilioni ya watu. Kulikuwa na mipango ya serikali ya Ujerumani kwa veterans wa vita. Wale veterans wenye ulemavu, waliokadiriwa kufikia milioni 1.5, serikali iliwasaidia kwa ruzuku nk. Kulikuwepo na maonyesho ya serikali na nyumba za serikali za opera. Reli inayomilikiwa na Serikali ilipoteza pesa. Serikali ya Ujerumani iliyokuwa na viwanda ambavyo vinazalisha siagi(margarines) na sausages, nazo ziliingia hasara kwa kupoteza pesa nyingi. Kuna kila dalili serikali yetu ndiko inakoelekea.

Benki kuu ya Ujerumani ilianza kuchapisha kiasi kikubwa cha pesa za kulipia matumizi yote hayo. Katika kilele cha mfumuko wa bei mwishoni mwa mwaka wa 1923, ni asilimia 1.3 tu ya matumizi ya serikali ya Ujerumani yalitokana na mapato ya kodi. Matokeo yake ni kwamba chini ya miaka mitano bei iliongezeka mara bilioni 100.(100 billion-fold)

Mfumuko wa bei ulimdhuru kila mtu kwa namna moja ama nyingine. Mabenki mengi yalifilisika. Mwanahistoria Gerald D. Feldman aliripoti kwamba makundi ya wachimbaji wa makaa ya mawe waliokosa kazi waligeuka majambazi na kuisambaratisha nchi. Pia kwa sababu wakulima walikataa kuzalisha mazao yao kwa fedha za karatasi zisizofaa(devalued currency). Serikali ilianza kudhibiti mfumo wa kodi ya pango, wakapandisha sana kodi ambapo ilipunguza uwezo wa wamiliki wa nyumba kuweza kurejesha gharama zao, na wajenzi waliovunjika moyo na kukata tamaa za kujenga nyumba zaidi. Hivyo miji ilikopa kutoka kwa wakopeshaji wa kigeni kujenga nyumba ambazo zilipoteza pesa. Maktaba na makumbusho hawakuweza kufanya shughuli zao kwasababu ya mfumuko wa bei. Utafiti mkubwa wa kisayansi ulikuwa hauwezekani kwasababu za ukosefu wa fedha.

Mwahistoria mwingine aliyeitwa Konrad Heiden aliripoti, "Siku ya Ijumaa mchana mwaka wa 1923, mistari mirefu ya wale wafanyakazi wa maofisini, ama “whitecolors” walijipanga nje ya madirisha ya malipo. Kuanzia viwandani, maduka na idara, mabenki na ofisi. Kila mmoja alipokea mfuko uliojaa makaratasi(kama Zimbabwe). Watu walikwenda kwenye maduka ya karibu ya chakula ambako mistari tayari ilikuwa mirefu. Kipindi hicho, pound ya sukari, kwa mfano, inaweza kufikia milioni mbili kabla hata mnunuaji hajafika dirishani wakati yuko kwenye msitari kungojea zamu yake ya kununua; lakini pia wakati mwingine wanapofika dirishani, hiyo milioni mbili unakuta inaweza kuwapatia nusu paundi tu ya sukari, ndivyo mambo yalivyikuwa yakibadilika kwa kasi. (Wao wajerumani wanatumia au walitumia mfumo wa kupima wa pounds au lb’s badala ya kilograma au kg’s).

Kila mwananchi alijitahidi kupambana na hali yake hadi pale atakapolipwa tena, yani paycheck to paycheck wenzetu wanaita.

Watu walioajiriwa katika sekta binafsi walikasirika pale wafanyakazi wa serikali walifanikiwa kulipwa mishahara yao in advance. Serikali ilifanya hivyo kwa wafanyakazi wake ili waweze kununua bidhaa haraka kabla pesa haijashuka thamani zaidi. Toleo la “Soziale Praxis” liliripoti hivi: "Inaonekana kuwa maoni ya wananchi sasa yanageuka hatua kwa hatua dhidi ya watumishi wa umma kwa kiasi ambacho kinaongeza wasiwasi mkubwa. Ni kiasi gani cha chuki kila siku kinachoelekezwa kwa wafanyakazi hao wa umma. Wale wote waliokuwa wakishabikia hizo huduma nyingi za umma sasa wakawa wanapingana na serikali".

Hitler alitoa hotuba zilizowavutia wale aliowaita "mabilionia wenye njaa" ambao walikuwa na fedha za mabilioni za karatasi lakini hawakuweza kununua japo mkate. Kwa ujumla, wakati wa mfumuko wa bei, Hitler aliajiri Nazi members 50,000 na akawa na nguvu kubwa sana ya kisiasa kuwahi kutokea nchini humo.

Hitler alijaribu kuipindua serikali(Novemba 8, 1923), lakini alishindwa na akafungwa jela. Hata hivyo, alifanikwa kuwabakisha wafuasi wake wakuu, na aliandika memo yake yenye sumu ya “Mein Kampf “ ambayo ilifanywa kuwa Biblia ya chama cha Nazi.

Ilipofikia mwishoni mwa miaka ya 1920, uchumi wa Ujerumani ulianza kutengamaa, na kulikuwa na riba ndogo kwa wale wanachama wa Nazi. Katika uchaguzi wa 1928 wa Reichstag (bunge), walishinda 2.6% tu ya kura.

Endapo mambo yangeendeela kuwa mazuri, Hitler angeweza kusahaulika. Alihitaji mgogoro mwingine ili aweze kunufaika na kupata nguvu za kisiasa...

Mgogoro ulikuja, kwa wale wanaokumbuka, “Great Depresion” Serikali ilitaka kupunguza mfumuko wa bei kwa kupitia “deflation”. Iliweka bei katika viwango vya juu vya soko ambavyo viliwavunja moyo watumiaji kutaka kununua, na waliweka mishahara katika viwango vya juu vya soko ambavyo vilisababisha wale wanaotoa ajira washindwe kuajiri wafanyakazi. Kodi kubwa ilifanya kuwa vigumu kwa watu kuweka akiba na kuwekeza. Ushuru wa juu ulipoteza biashara. Wakati wazalishaji wa Ujerumani waliweza kuuza nje bidhaa, walikuwa na ugumu kukusanya malipo kwa sababu ya udhibiti wa mfumo wa kubadilishana. Sera hizi zote zilisababisha ama kupelekea ugumu kwa uchumi kukua.

Zaidi ya hayo, mabenki ya Ujerumani yalikuwa “vulnerable”, kwani hawakuwa wamesha “fully recover” baada ya mfumuko wa bei ambao ulimaliza kiasi kikubwa cha mitaji yao, hivyo kuwasababisha wategemee amana za muda mfupi kutoka kwa wageni ambazo hatahivyo nazo zinaweza kuondolewa muda wowote.

Kadri idadi ya wasio na kazi ilivyozidi kuongezeka, ndivyo wajerumani wengi walifurika kwenye chama cha Hitler cha NAZI, na idadi ya wanachama wa Nazi kama ilivyo kwa ccm sasa, ilipaa juu.

Hitler aliendeleza harakati zake za kujichimbia mizizi ya nguvu za kisiasa, alisafiri mara kwa mara, akihutubia nchini Ujerumani. Alitaka wapinzani wake wahangamizwe na kupotezwa, kwa hiyo akawaita wasalaliti wa taifa na wahalifu. Aliwashutumu kwa usaliti kama jiwe anavyoshutumu wengine mfano ilivyotokea kwa Lissu. Nazi walikuwa na vitengo vyao vya paramilitary vilivyojulikana kama S.A. na S.S.. Vikosi hivyo vilianzisha mashambulizi ya kumwaga damu kwa wapinzani wake. Hii ilivutia vibaka zaidi ambao walipenda vurugu na walikuwa wako vizuri upande huo. Nina uhakika kuna mifano mingi sana nchini mwetu yenye kuendana na hili.

Kila usiku huko ujerumani, kulikuwa na makusanyiko ya wanachama wa Nazi. Watu wa Hitler walimtukuza kwa kuchapisha gazeti la Nazi, kusambaza kumbukumbu za Nazi na kukuza sinema za Nazi.

Kiligeuka na kuwa chama kikubwa zaidi cha kisiasa nchini Ujerumani, na hadi Januari 30, 1933, Hitler aliibuka kama Kansela wa Ujerumani - mkuu wa serikali. Aliendelea kujiimarisha zaidi na kujilimbikizia madaraka yasiyo na ukomo! kabla ya mtu yeyote kushtukia kile kinachoendelea.

Kama ilivyo kwa madikteta wengi, Hitler hakutaka kabisa kuwa na madaraka machache. Hakujali kuhusiana na mihimili ya uongozi...Alichukua madaraka hayo kutoka kwa Kansela Otto von Bismarck. Biashara zote binafsi ambazo zilihusika kwa namna moja ama nyingine na vita zilitaifishwa na vingine viligeuzwa kuwa ofisi za serikali. Serikali ilifunga baadhi ya biashara za watu binafsi, ambazo viongozi hao walidai kwamba “hazihitajiki”. Kulikuwa na kazi za kulazimishwa(forced labor), na hakuna mtu anayeweza kubadili kazi bila idhini ya serkali. Serikali ilicontrol uchumi wa nchi kiasi kwamba hakuna mtu aliyethubutu kuipinga serikali ya Hitler au yeye mwenyewe.

Ingawa Hitler alitaka mipango ya uchumi kama ile ya waSoviet, pale alipokuja na “four year plan”, kulikuwa na umiliki binafsi wa mali nchini humo, lakini pia na udhibiti mkubwa sana wa serikali. Alihusika na ukosefu wa ajira kwa kuanzisha kazi za kulazimishwa kwa wanaume na wanawake(forced labor). Udhibiti wa Serikali hasa kwenye uchumi ulisababisha iwe vigumu kwa mtu yeyote kutishia utawala wa serikali yake. Hitler aliongeza polisi wa siri(wasiojulikana), kambi za mateso na vifo.

Mfumo wa elimu wa Kijerumani, ambao ambao ulikuwa wa kupigiwa mfano hata na wamarekani wengi, ulihusika kwa kiasi kikubwa katika yote haya. Katika kipindi cha karne iliyopita, serikali ilikuza udhibiti kamili wa shule na vyuo vikuu, na kipaumbele chao kikubwa kilikuwa ni kufundisha utii. Wasomi wa wasomi walisisitizia “ujamaa” au “collectivims”. Wito mkubwa na uzalendo ilikuwa ni kufanya kazi serikalini, kama ilivyo sasa kwa watu kujitoa ufahamu kwasababu ya ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa na teuzi nyinginezo.

Mnamo mwaka wa 1919, mwanasayansi wa jamii, Max Weber, aliripoti kwamba "heshima ya mtumishi wa umma ilitolewa kwa uwezo wake wa kutekeleza uamuzi/maamuzi kutoka juu." Ndivyo ilivyo hata kwetu, heshima ya mtumishi wa umma, inatokana na ukichaa wake wa kufuata amri kutoka juu na kunyanyasa wapinzani.

Tunayoweza kujifunza:

  • Sera mbaya za kiuchumi na sera za mataifa ya nje, zinaweza kusababisha matatizo ambayo yana madhara ya kisiasa kwa taifa letu.

  • Wanasiasa, hata ilivyo kwa jiwe, hupenda kutumia nguvu zisizo za lazima kukabiliana na wananchi wake wenyewe, hata kama wananchi hao wana madai yenye haki za kimsingi, na hata kama matatizo hayo ya wananchi yalisababishwa na serikali hiyohiyo ama sera zake na za chama, kwasababu matatizo mengi ya kimsingi, husababishwa na sera mbaya za serikali. Mfano halisi ni chama cha mapinduzi. Sasa juzi tu, kiongozi wa upinzani kapigwa risasi mchana kweupe(Lissu), kisa ni matatizo ambayo yamesababishwa na ccm hiyohiyo yenye viongozi waliyotuma watu wa kwenda kumuuwa Lissu.

  • Katika nyakati ngumu, mara nyingi watu wengi wanapenda kuwa pamoja na kuunga mkono juhudi za kiongozi dhidi ya "maadui wa taifa", na hata mambo mabaya ambayo yasingeweza hata kufikiriwa nyakati ambazo mambo ni mazuri kwa taifa. Kwetu sisi kama tunavyoona, ugumu wa maisha unatumiwa na serikali hii dhidi ya wapinzani wake kama alivyofanya Hitler na chama cha cha Nazi. Kumekuwepo na chuki kwamba matajiri ndo wamesababisha shida za masikini na matatizo yote nchini yameletwa na upinzania ambao ni wasaliti wa taifa.


  • Wale ambao wanasapoti utawala wa udikteta nchini, wanahitaji kufikiria ambavyo unaweza kusababisha mazingira yetu kuwa mabaya zaidi, especially kisiasa kuliko ilivyo sasa - kama matumizi ya serikali yasiyokuwa na maelezo wala kupitishwa na bunge nk, kodi kuongezeka, biashara kuwa ngumu na kufungwa, mfumuko wa bei na kuanguka kwa uchumi ni viashiria tosha kabisa kuonyesha huko tunakoelekea.

  • Watawala dictators wakati mwingine huaribu kile wanachoita “nia zao nzuri”, kwa hamu yao dhahiri ya kuuwa upinzani. Kwahiyo ni kama kujipiga risasi ya mguu. Nchini mwetu yako wazi kabisa haya. Wengi wanasema jiwe ana nia nzuri, lakini hamu yake kubwa ni kuumaliza upinzani!


  • Hakuna njia ya kuaminika ya kuzuia watu wenye nia mbaya au wasio na uwezo wa kuongoza kupata madaraka.
  • Mfumo wa kisiasa unaotegemea mihimili yote muhimu na kuhakikisha “checks and balances” ni muhimu.Kama jinsi ilivyo katiba ya Umoja wa Mataifa, na hata ya marekani – ambapo inafanya kuwa vigumu zaidi kwa muhimili mmoja wa serikali kuutawala mwengine.

  • Mwisho, uhuru unaweza kulindwa tu ikiwa watu watajali vya kutosha kuupigania na siyo kupiga tu kelele na kulalamika, kwa sababu kila mahali serikali inataka kuuminya uhuru huo, na haupatikani kwa hiyari.
 
Unamaelezo mazuri mkuu ila hii mada yako tu inaweza kukuletea shida....waonee huruma watu wa familia yako
Kama hata hii inaweza kuniletea shida, basi nadhani tuko kwenye hali mbaya kuliko nilivyokuwa nikifiri.

The fact kwamba nilimpigia kura ndo ninapata shida kuridhika na uamuzi ambao niliuchukua.
 
Kama hata hii inaweza kuiletea shida, basi nadhani tuko kwenye hali mbaya kuliko nilivyokuwa nikifiri.

The fact kwamba nilimpigia kura ndo ninapata shida kuridhika na uamuzi ambao niliuchukua.
pole mkuu ni kawaida watu wengi hutafsiri tofauti na kile mtu alichokimaanisha
 
Tumuombe Mungu atujalie ujasiri na mbinu ya kudai tupate katiba mpya.Hili andiko lako likisomwa na kueleweka na Watanzania 5m kinaeleweka.Hongera umetimiza wajibu wako.
 
Those who want to live let them fight,those who dont want to fight dont deserve to live

what a lucky for rulers that men dont think

ADOLF HITREL


if i go forward follow me, if i fight fight with me, if i retreat kill me

MUSSOLIN

"I use emotions for the many and reserve reasons for the few"

HITREL
 
Tumuombe Mungu atujalie ujasiri na mbinu ya kudai tupate katiba mpya.Hili andiko lako likisomwa na kueleweka na Watanzania 5m kinaeleweka.Hongera umetimiza wajibu wako.
Pamoja sana, together we can make change to our dear nation.
 
Kinachofanya mayalla asichukiwe jf na asitishwe na wasiojulikana ni tabia yake ya kung'ata na kupuliza. Leo ataipiga serikali na nondo za ukweli kesho ataupiga upinzanzi au lissu adui mkubwa wa serikali ya sasa, so ni ngumu kumu attack mtu kama mayalla ndio maana watu hatumchoki hongela kwa hilo broh
 
Kinachofanya mayalla asichukiwe jf na asitishwe na wasiojulikana ni tabia yake ya kung'ata na kupuliza. Leo ataipiga serikali na nondo za ukweli kesho ataupiga upinzanzi au lissu adui mkubwa wa serikali ya sasa, so ni ngumu kumu attack mtu kama mayalla ndio maana watu hatumchoki hongela kwa hilo broh
Hahaha! Daah! emeona mkuu? Inahitaji akili ya ziada kuona hiyo!
 
Back
Top Bottom