UDIKTETA: Maisha ya ufahari wakati wa madaraka. Machungu mwisho wa utawala. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDIKTETA: Maisha ya ufahari wakati wa madaraka. Machungu mwisho wa utawala.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Nov 26, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Heri dikteta aliyevaa ngozi ya chui kuliko yule aliyejivika ngozi ya kondoo.
  Adorf Hitler, Samwel Doe, Idd Amin, Mobutu Seseseko kuku wa Zabanga, Saddam Hussein, Charles Tyler, Hosni Mubbarak, Muamar Gadaff hawa ni miongoni mwa watawala wanaotajwa kuonja pepo ya madaraka ambayo mwisho wa utawala wao huwa na machungu makubwa ambayo hufuta kabisa ladha na historia ya ufahari wa maisha yao. Wengi wamejikuta wakiuawa kinyama pamoja na familia zao. Ni nini raha na faida ya utawala wa kidikteta ikiwa mwisho wake ni mateso na majuto makubwa? Lakini kwa upande mwingine kuna madikteta waliovaa ngozi za kondoo na kujificha katika kichaka cha demokrasia. Hawa ndio wengi na hatari zaidi katika ukandamizaji wa haki za raia. Miongoni mwao ndio hawa wanaotutawala ndani ya mipaka ya nchi yetu.
   
Loading...