UDHALILISHAJI WATOTO UJERUMANI UNATISHA

UDHALILISHAJI WATOTO UJERUMANI UNATISHA

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
9 June 2019
Polisi nchini Ujerumani imetoa taswira ya kutisha kuhusu udhalilishaji watoto nchini humo. Kulingana na takwimu za uhalifu za mwaka 2018, zaidi ya watoto 100 waliuawa, na maelf walidhalilishwa kingono.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto 136 waliuawa kinyama mwaka 2018, ambapo asilimia 70 ya waathirika walikuwa chini ya umri wa miaka 6. Watoto wengine 98 walikuwa pia wahanga wa majaribio ya mauaji.
Idadi ya watoto waliodhalilishwa kingono mwaka uliopita iliongezeka kwa asilimia 6.43 kutoka mwaka 2017, na kufikia visa 14,600 -- ambao ni wastani wa visa 40 kila siku.
Tunafikiri visa vingi haviripotiwi
Polisi inasema tarakimu halisi zinaweza kuwa juu zaidi, lakini mnamo wakati wakosaji wana kawaida ya kuwa wanafamilia, marafiki au majirani, inakuwa vigumu mara nyingi kwa watoto kuripoti uhalifu kama huo.
Rais wa Ofisi ya shirikisho inayoshughulikia uhalifu nchini Ujerumani (BKA), Holger Münch, alisema ingawa polisi waliweza kutatua karibu asilimia 80 ya kesi walizoshughulikia kuhusu udhalilishaji wa watoto kingono, takwimu zinawakilisha tu uhalifu ulioripotiwa polisi. Akaongeza kuwa "tunahisi - na watalaam wakadiria - kuwa uhalifu mwingi unapita bila kutambuliwa."
DW
 
Paganism and occult practice on the flik.
 
Duuh
Hata hapa bongo hali si nzuri ila ripoti hua hazitolewi watoto wote waliofanya mapenzi chini ya miaka 18 tayari niudharilishaji
 
Back
Top Bottom