Udhalilishaji vyuo vikuu

Kuna Dr mmoja aliwahi kuniambia Hawafaidi mshahara Bali in madenti tu ndo wanachofaidi

inaweza kuwa mkuu mana kuna lecter mmoja kati vyuo tajwa kwao mambo safi huyo ndo hatar na ana course kama 2 wadada zetu wanaumizwa,mwingine ambaye yuko pale mza yy ni dvc dah hatar sana
 

nilichokiona ndicho nilichowakilisha na nashukuru MUNGU kuniumba kidume mateso wanayopata wadada siyo ya kuvumilika kama ww ni mmoja wao stop it ni dhambi kubwa usifiche ukwel unaoonekana,lakin pia ulipewa ubongo si tu kwa ajili ya kukusadia kwenda toilet fanya utafiti hata kidogo hoji hata wadada wa vyuo viwili karbu yako utastaajabu hadi sms za vitisho wanazopewa,ufaham kuwa bado dada zetu ni dhaifu hawajiamin ingawa sio wote
 
Bwana Nasami. Waambie hao wanawake unaosema wanaonewa na kunyanyaswa na wahadhiri, wajitokeze, watetee haki zao. Kwani sheria ipo upande wao. Kama kweli wamenyimwa alama katika mitihani na majaribio kwa sababu za kingono, wana uhakika kuwa walifanya vizuri mitihani yao, walihudhuria madarasa bila tatizo, hawajaruka kufanya majaribio hata mara moja, waelekeze sasa waende kwa dean of students, wakitoka hapo wakajaze fomu za kukata rufaa na nakuhakikishia watafaulu, na wahadhiri wataumbuja na kuchkuliwa hatua. Lakini kama hao mabinti ni wale wale, wategemea huruma na miili yao, wasijaribu hilo, kwani wataonekana hawafai hata kuwepo chuoni. Kwa uzoefu wangu, hakuna mwanamke mwenye akili za kutosha darasani aliyeiosa alama zake za masomo kwa sababu za mizengwe ya wahadhiri.
 

Mkuu hili limenigusa.

Mimi nilijikuta katika mazingira haya. Kwa umri ni mdogo ukinilinganisha na yule mwalimu ila kwa shughuli zinazoniweka mjini niko level nyingine sasa due to that mwalimu akawa hanipendi coz ana inferiority complex akawa na bifu za kijinga sana dhidi yangu.

Siku moja nikamfuata ofcn nikamuomba asimame kwenye nafasi yake kama mwalimu kutokana na ishara kwamba zile bifu zingetugharimu pia akamind.

Kwenye test alinipiga panga mno, sikuenda kumuona coz nilijiamini kwamba kwnye final ningempiga bao. Aise kwenye final ndo alinipiga zaidi akanipa sup kwa mara ya kwanza na ilikuwa semester yangu ya mwisho. Sikumfuata ila nilienda department nikawaambia kwamba nina contest yale matokeo na la pili nilitishia kumuua yule mwalimu ila kabla ya hapo nitafuatilia utaratibu wa kusahihisha mtihani wangu upya.

Kwenye jopo la walimu wiopendekezwa kusahihisha wakaogopa ila baadae alipatikana kichaa baili wa marks. Huyu jamaa alitoa majibu kwamba mshkaji alinipunja marks 25 kwa makusudi. Siku ya kupokea majibu hayo walimuita mwalimu husika naye kwa woga aliniomba msamaha kama mtoto.

Ukijitambua mbona easy tu!
 

ushaur mzuri wengine wamo humu naamini watafanyia kazi ushaur wako
 

uchunguzi wako umefanya upende mmoja mimi nadhani ungechunguza upande wa pili kwa nini hao ma dada wanafeli. kila siku wanakesha kwenye madisco, bbm, whatsApp, twits zakumwaga, mara selfie mara nini unafikiri watafaulu vipi kama si kutoa mbunye? mimi naona wasipojierekebisha watapata tabu sana na lazima wafanye wanavyofanyiwa.
 
Msipinge ukweli, mnahusika nini? Macho yamewatoka
 

Hata ungevaa kama sista some of the lecturer are crook na isitoshe
 

Absolutely mimi kuna lecturer mpuuzi alinisumbua na vituko kibao siwezi kuelezea maana machungu hayaisha wakati nafanya taratibu za kwenda mahakamani issue ikasolviwa watu wanatetea subirini wake mabinti na dada zenu with time mtakuwa na hizo proof mlizotaka
 
Mnaombishia mleta mada nendeni mkaone yanayofanyika kwny vyuo km CBE, IFM n.k, acha na vyuo vyenye mfumo rasmi wa kiuendeshaji km UDSM, MZUMBE na vinginevyo

Nakubaliana na wewe mimi nikisoma vyuo 2 sikupata shida yoyote nilipokuja kusoma cha 3 among the above nimeishia kupata peptic ulcer watu wanapinga tu ila hbr anayo huyo mwalimu
 
Nakubaliana na wewe mimi nikisoma vyuo 2 sikupata shida yoyote nilipokuja kusoma cha 3 among the above nimeishia kupata peptic ulcer watu wanapinga tu ila hbr anayo huyo mwalimu

pole sana,hii tabia lazima ikome malecter hatuko tayar kutudhalilishia dada/mama zetu
 
Ukiona Lecturer anakulazimisha kwa nini usitoe taarifa?

Tatizo la wanawake wanaficha uovu halafu baadae wakishaathirika wanaanza kulaumu mfume dume.

Mrikodi huyo Lecturer wakati anapochanganya kazi yake na mapenzi.
Kisha Toa taarifa.
Utapata watetezi wengi na huyo Lecturer atawajibishwa tu.

Ukificha itakula kwako. Utapigwa tu hakuna nmna nyingine.Maana wote lazima tukubaliane kuwa hii nchi haina maadili.
 
Kitakachowasaidia kwa sahiv ni kitu kimoja tu, kutaja majina ya hao malecturers wenu hadharani hapa jamvini mbali na hapo mnaendelea kushughurikiwa tu
 
Ingawaje sijawahi kusoma chuo na sifahamu mazingira ya ufundishaji huko vyuoni..lakini nikitumia fikra zangu naona kuwa hili swala hawa wahusika inaosemekana kuwa wanadhalilishwa itakuwa kwa namna moja au nyingine watakuwa wanaupenda huo mchezo kwa maslahi yao binafsi..kwani naamini kabisa sehemu kama vyuoni huwa kuna kamati za maadili na hushughulikia masuala kama hayo...sasa kama muhusika anakumbana na hali kama hiyo..na mwenyewe haripoti sehemu husika ili mtuhumiwa ashughulikiwe kwa mujibu wa taratibu...hapo wakulaumiwa ni mtendwa na wala si mtenda.....
 
tukiungana kukemea jambo hili litapungua kama si kuisha,na soon tutaweka majna ya malecturer wasio na maadili wasipojirekebisha
 

dah umeongea kitu kizito sana mkuu yani umenifanya nitoe machozi
Nimekuwa muhanga wa hilo jambo kama ilo nilipishana na lecturer kauli wakati nadai haki yangu badala yake alinifanyia visa mpaka akanidisco kwa ajili ya somo lake tu na maisha yangu yote ya chuo sikuwahi pata sup zaidi ya iyo moja ya huyo jamaa ambayo mwisho wake ilinifanya nidisco
Huwa naumia sana nikimkumbuka jamaa ila ninachomshukuru mungu sikukataa tamaa na sasa ninasonga mbele
Mi niliamua kuachana nae tu kwa sababu nilikuwa siwezi kabisa eleza popote nilijawa na hisira nilikua najikuta nalia tu badala ya kueleza shida yangu kwenye mamlaka husikaa kwa kwel iliniumiza sana mwishowe nikaamua ondoka tu na kuachana kabisa na ilo jambo mana nilihisi kabisa naweza kufa mana hayo ndo mawazo pekee yaliyoutawala moyo wangu kwa kipindi kile, na hapo kumbuka nilikuwa nimeshamaliza semister yangu ya mwisho ya mwaka wa tatu.
Ila kiukwel nashindwa kabisa msamehe mshikaji moyo wangu umejawa na kisasi juu yake huwa naomba mungu anisaidie niweze msamehe lakin kibinadamu siwezi kabisaa
 
mi kila siku naomba mungu anipe moyo wa ujasiri la sivyo yule jamaa lazimaa ata pay the price kabisaa yani hawezi likwepa hili jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…