Udhalilishaji vyuo vikuu

Udhalilishaji vyuo vikuu

nasami

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2015
Posts
237
Reaction score
42
Katika hali isiyo ya kawaida imegundulika uwepo wa udhalilishaji mkubwa kwa wanawake wanaosoma katika vyuo mbalimbali nchini, data zinaeleza kuwa vyuo vingi vimekuwa na lecturer ambao hutumia nafasi hyo kuwataka kimapenzi wanafunzi na pindi mwanafunzi huyo akikataa basi matarajio yake katika masomo huwa yanapotea.

Wakati hilo likifanyika mkuu wa chuo pamoja na idara zake wanalijua hili lakini hakuna hatua zinazochukuliwa, kwa kuumizwa na suala hili nimeona nilete kwa wanajamvi ili ujumbe ufike kwa haraka wanawake wanateseka sana vyuoni mfano ni chuo kikuu kilichopo Tanga, DUCE na kile chenye idad kubwa ya wanafunzi Dodoma.

Serikal kupitia vyombo husika chunguzeni haraka sana hali za wamama wetu vyuoni zinatisha.
 
usilete habar za vichocholoni hapa. leta source ya habar yako
 
...kama wamemlamba mkeo we sema tu wahusika wajirekebishe,sasa ukifichaficha mjadala utakuwa juu ya mapungufu ya mada yako na si mantiki ya mada...
 
Anachokisema huyo mtoa mada ni kweli tupu,kwa sisi tuliopitia vyuoni tunajua hayo mambo yalivyo na jinsi wanawake wanavyodhalilishwa bila kujali kama ni mke wa mtu au la, kama dr au prof akikutaka basi atafanya kila hila ikiwemo hata kukufelisha,

na wengi wamejikuta wanavuliwa nguo za ndani kwa sababu hizi ingawa wapo ambao wanajilengesha ili wapewe maksi za juu but haiondoi ukweli kuwa wengi wao wanawake wanapata shida sana kwenye hivi vyuo vyetu.
 
Huo uchunguz udom umeufanyia collage ipi

Acha upuuzi wewe we ndo umesoma vyuo peke yako? Hayo yapo , hata vyuo vya nje mambo hayo yapo. Nilishawahi kusoma na kufundisha chuo part time. Mambo ni disaster
 
Ilimradi siku hizi unajua kuandika imekuwa shida!
 
Acha upuuzi wewe we ndo umesoma vyuo peke yako? Hayo yapo , hata vyuo vya nje mambo hayo yapo. Nilishawahi kusoma na kufundisha chuo part time. Mambo ni disaster

mbna unaongea kama sio mkufunzi ulifundsha chuo kipi na mm kisa lang lipi kuulza alifanya uchunguzu collage gan au??
 
anachokisema huyo mtoa mada ni kweli tupu,kwa sisi tuliopitia vyuoni tunajua hayo mambo yalivyo na jinsi wanawake wanavyodhalilishwa bila kujali kama ni mke wa mtu au la,kama dr au prof akikutaka basi atafanya kila hila ikiwemo hata kukufelisha,na wengi wamejikuta wanavuliwa nguo za ndani kwa sababu hizi ingawa wapo ambao wanajilengesha ili wapewe maksi za juu but haiondoi ukweli kuwa wengi wao wanawake wanapata shida sana kwenye hivi vyuo vyetu.

wanawake wepi wanaodhalilishwa? Hawa wanaopiga picha za uchi na kuzirusha kwenye mitandao?
. Hao wanajirecord video wakikata viuno uchi wa mnyama?
Hakuna ukweli wowote hawa dada zetu wanapenda miteremko sana acha wavuliwe tu. Walishajidharirisha wao wenyew
 
Kila sekta mwanamke akienda vibaya/kizembe lazima adhalilishwe kwa kuombwa rushwa ya ngono!
 
Haya mambo ya kudhalilishwa wanawake ni kweli yapo sana vyuoni ila kwa upande mwingine wanawake wenyewe hujitakia, unakuta hawa dada zetu hawapendi kusoma ila wanataka ufaulu wa marks za juu, sasa unategemea atafaulu vipi kama sio kujipeleka kwa hao ma Dr na Prof kuwa kitoweo! wanawake wenye misimamo na ambao wako vizuri kichwani huwa wanaviruka hivi vizingiti kwa misamamo imara. ukipenda mtelemko inakula kwako!!
 
Back
Top Bottom