Udhaifu wa vyombo vya habari tanzania na uandishi na yaliyotokea kwenye operesheni tokomeza

Ndugu, acha tu, kwanza vyombo vingi tulivyonavyo ni vya wanasiasa, wanaripoti kwenye mrengo wa Chama chake tu. Leo hii angali a star tv, tbc na baadhi ya magazeti yapo ccm. Tanzania daima CDM, hayo ni machache. Hukweli hakuna mwandishi anayejitolea kuelezea umma nini kinaendelea nyuma ya pazia. Vinginevyo usubiri kutolewa kuchwa au jicho bila ganzi.
 
kaka vyombo vyetu vya habari mpaka mwanasiasa aseme ndo wanaandika ndo maana taarfa zao nyingi unakuta furani kasema hivi hata kama kapotosha wao ni kuripoti tu...pili vyombo vingine vya habari vimekaa kikabila.....tatu baadhi ya vyombo vya habari vinachochoe ngono na maambukizi ya ukmwi,,,mfano clouds eatv....nne baadhi ya magazeti yapo kwa ajili ya chama tawala jamani waandishi siyo mpaka mwanasiasa aseme ndo muandike lazima mjue taaruma yenu iko wapi
 
A moment walipoifungia Mwanahalisi kwangu ilikuwa ndo mwisho wa kuwa msomaji wa magazeti... Hawa waandishi wa habari makanjanja wachumia tumbo hawana ummoja kwa kuwa wote ni wanafiki wakubwa ... unakuta mwandishi wa habari anatamka hadharani eti "shida mwana mandanda kulala na njaa kupenda"! btw kwanini wanaofeli huwa wanakimbilia tasnia ya habari?...
 
Ninachokiona katika suala hili ni self-censorship. Haiwezekani miongoni mwa vyombo vya habari lukuki Tanzania kusiwe na hata kimoja kilichopata fununu ya unyama iliokuwa ukiendelea katika operesheni Kimbunga na Tokomeza Ujangili. Nina hakika kama kungekuwa na chombo chochote cha habari ambacho kingethubutu kutoa habari hizo, basi hapohapo kingefungiwa kwa madai ya kuandika habari za uongo na uchochezi na kutokuwa wazalendo. Vingine vingedaiwa kuwakilisha na kutetea maslahi ya nchi jirani na kusukuma ajenda ya nchi hizo. Kwa kifupi, vyombo vya habari vilijawa woga, hasa baada ya kufungiwa kwa magazeti ya Mwananchi na Mtanzania.
 
Waandishi wengi hivi sasa wapo "busy" kumsafishia njia mwanasisa flani na kumchafulia mwingine kuelekea 2015,aghalabu wengine wanajipanga kuingia katika uchaguzi wao wenyewe hivyo wanajisafishia njia kwa kuwa karibu kihabari na viongozi flani!
 
Tukumbushe. Ni chombo gani na kililiport lini na wapi?

mkuu bora umemjibu, kama nape na kinana habari zao zilikuwa zinarepotiwa na kwenye tv zilionyeshwa kwa mbwembwe, hii inamaanisha waandishi walikuwa na wasahaa wa kufahamu hayo, laiti tume ingekuwa na lengo la upotoshwaji basi hawa haki zao zingepotea.
Hili kama taifa hatuwezi kulisahau, mfano, kumfanyisha mtu na mama yake mapenzi, kumfungia mtuu kwenye mti mwituni tena msitu wenye wanyama wakali.
 
Tatizo ni mkubwa zaidi ya tunavyofikiri, Tania zote zimekumbwa na tatizo hizi juzi watu walilalamikia wanasheria, siku nyingine alikuwa ni madaktari, malalamiko ya waalimumyalishawekwa , wanasiasa ndio kabisa usiseme hakuna aliye mzuri kihivyo
 
Hii si kwa waandishi tu hata humu JF.na hili linadhihirisha upumbavu wetu wa TANZANIA Tulipo andika kuhusu unyama unao fanyika humu JF tuliitwa wahamiaji haramu yakowapi sasa
 
Hii si kwa waandishi tu hata humu JF.na hili linadhihirisha upumbavu wetu wa TANZANIA Tulipo andika kuhusu unyama unao fanyika humu JF tuliitwa wahamiaji haramu yakowapi sasa

pole sana mkuu ni kweli nimeona jf kuna mtanzania mmoja aliripoti lakini hiyo ilichukuliwa kama habari binafsi, ingeripotiwa kwenye media kwa kutumia ustadi wa vyombo vya habari na mbinu za kitaaluma ya uandishi, watanzania tungestuka kuhusu unyama huu.
hii pia ichukuliwe kama fundisho kuwa jamii forum ni zaidi ya chombo cha habari, taarifa huku nyingi ni za kipelelezi, waandishi wetu wanaweza anziaa hapa kutafuta ukweli wa mambo.
 
ila Tokomeza imesaidia sana kupunguza uharamia na ujangili sababu imefanikiwa kushusha idadi ya Tembo wanauawa. mfano hapo awali ilikua tembo wawili(2) kila siku wanajangiliwa lakini toka Tokomeza imaenza walikufa tembo wawili tuu haya ni mafanikio. Kuhusu ilo swala la vyombo vya habari kwakweli sidhani kama wanasababu ya kulaumiwa sababu Operatin ya ndani ya hifadhi haikuwa rahisi kwao kwenda sababu ni mazingira hatarishi sana. Ila hizo habari za kufwatilia matukio ya kinyama wanayofanyiwa wananchi zimekua zikisikika kila leo. Mi kwa upande wangu nawashangaa sana wanaoipinga Tokomeza nadhani cha kufanya apo ni kuboresha utendaji wake na ufichuaji wa vitendo vya kinyama na kuvikomesha basi. ila we haramia ana silaha kali anajibizana nao kwa risasi apo nadhani kinachofwata lazima kiwe ni matokeo ya kujihami ambayo ni bayana kuwa ni vifo na majeraha. Labda mnielimishe kama kuna National Park journalists.
 
katika taifa ambalo wandishi wanauliwa kwa kulipuliwa na mabomu wakiwa kazini, katika taifa ambalo waandishi wananyofolewa macho. binadamu ameumbwa na hofu.

Licha ya hayo wanaandika habari nyepesi sana. Niambie habari ya Jana ya Mwakyembe juu ya usafirishaji wameandika nini zaidi ya Mwakyemebe apokea Tuzo. Waandishi wengi wavivu na hawajui habari za kuandika wanaandika habari zenye kusismua tu kama ... Mh mbunge kafum,aniwa, wanafunzi wa chuo looh nk.
 
Nimeshajiuliza sana kuwa waandishi walikuwa wapi mida yote hii.

Kuna magazeti nilitarajia wangeweza kuripoti mapema lakini wapi.

Jambo leo, Uhuru na dadake Mzalendo, Habari leo mida yote ni kuichafua CDM tu.
 
ila Tokomeza imesaidia sana kupunguza uharamia na ujangili sababu imefanikiwa kushusha idadi ya Tembo wanauawa. mfano hapo awali ilikua tembo wawili(2) kila siku wanajangiliwa lakini toka Tokomeza imaenza walikufa tembo wawili tuu haya ni mafanikio. Kuhusu ilo swala la vyombo vya habari kwakweli sidhani kama wanasababu ya kulaumiwa sababu Operatin ya ndani ya hifadhi haikuwa rahisi kwao kwenda sababu ni mazingira hatarishi sana. Ila hizo habari za kufwatilia matukio ya kinyama wanayofanyiwa wananchi zimekua zikisikika kila leo. Mi kwa upande wangu nawashangaa sana wanaoipinga Tokomeza nadhani cha kufanya apo ni kuboresha utendaji wake na ufichuaji wa vitendo vya kinyama na kuvikomesha basi. ila we haramia ana silaha kali anajibizana nao kwa risasi apo nadhani kinachofwata lazima kiwe ni matokeo ya kujihami ambayo ni bayana kuwa ni vifo na majeraha. Labda mnielimishe kama kuna National Park journalists.

Kama wewe si mzigo wa CCM ni Lumumba b7 Fc

Ni jangili gani kakamatwa.

Uhai wa mtu ni sawa na tembo wa ngapi ?
 
Mimi nitalaumu waandishi wa habari kama mtaniambia kuna angalau 2% yao walipata division 1&2 kwenye mitihanj ya form iv au angalau division 3 form six.
Else mnawaonea tu!
 
Mimi nitalaumu waandishi wa habari kama mtaniambia kuna angalau 2% yao walipata division 1&2 kwenye mitihanj ya form iv au angalau division 3 form six.
Else mnawaonea tu!

Kuna wenye Masters. Phd. Ila uandishi si kitu cha kusomea kama kipaji hujazaliwa nacho. Waandishi wasomi Tanzania ndio hovyo kuliko hata class seven dropouts
 
Wengi wa waandishi wanafuata upepo wa kwamba kozi ya uandishi wa habari ni rahisi na itawapa umaarufu fulani. Uandishi unahitaji pamoja na mambo mengine, muono maana unaielekeza jamii.

Lakini umaarufu wa watu kama Ken Sarowiwa na Sorious Samura haukuja bure bali ulikuwa ni wa kuielimisha jamii ya yale maovu yanayotokea ndani ya jamii hizo.

Tatizo lingine ni la wahariri wa habari zenyewe maana nao wanalinda maslahi yao na hata kama ripota atakuja na habari ambayo ina uzito lakini habari hiyo ikawa ina -compromise nafasi ya mhariri wa habari basi yeye mhariri ana uwezo mkubwa wa kuwadhibiti waandishi wenye uchungu na nchi yao.

Vinginevyo wengi wa waandishi wa habari hasa wale ambao ni wachanga katika tasnia hiyo wataendelea kuendekeza uandishi wa hundi "Chequebook Journalism" ambao utaendelea kuwadumaza na kuzidisha janga la waandishi makanjanja.
 
Na wakiandika wanaandika uongo....ndio maana wananchi wameanza kuwashikisha adabu (wananchi wa Ntwara). Mtu unaripoti uongo wakati watu wana access na riport zako watakuacha?...waliwapa fundisho
 
Back
Top Bottom