Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,077
- 136,517
Kuna wakati huwa sielewi kabisa jinsi ambavyo akili zetu sisi Waafrika hufanya kazi. Nasema hivi hususan kurejea ziara ya rais Obama huko Kenya wiki iliyopita na ile ya mwaka juzi alipokuja Tanzania.
Kabla ya ujio wake Tanzania, kulikuwepo na jitihada nyingi za kulisafisha jiji la Dar, ikiwemo kuosha barabara na kufukuza wachuuzi wa biashara ndogondogo kutoka kwenye sehemu ambazo zilisemwa kuwa atapitia.
Huko Kenya nako hii majuzi haikuwa tofauti sana na tulivyofanya sisi. Kuna watu waliondolewa kwenye makazi au maeneo yao ya biashara. Kuna nyasi mpya zilipandwa siku chache tu kabla ya Obama kuwasili mpaka watu wakaanza kumtania Gavana Kidero kwa kuziita hizo nyasi 'Nyasi za Kidero'.
Sina hakika sana na sehemu zingine za Afrika ambazo marais wa Marekani wamewahi kuzitembelea lakini nadhani hakuna tofauti sana.
Sasa mimi huwa najiuliza, kwa nini huwa tunahamisha watu? Ni nini ambacho huwa hatutaki hao marais wakione? Kwani kutokuona kwao ndo kunaondoa ukweli au kunaondoa hali halisi?
Halafu huwa tunamdanganya nani hasa tukifanya hivyo? Hivi kweli tunadhani labda wao hawajui hali jinsi ilivyo? Wao siyo wajinga kiasi hicho.
Na kwani huwa wanapita kwenye hizo sehemu zote ambazo hufagiliwa na kupigwa deki na ambazo watu huhamishwa?
Huko Kenya eti walipanda hadi nyasi kwa lengo la kupendezesha mji. Ndo kusema hilo wazo lilikuja baada ya Obama kutangaza atakwenda Kenya?
Ni kama vile sisi hatupendi vitu vizuri. Kwa sababu, kwa nini isiwe hivyo kila siku? Kwa nini tusipande nyasi pale ambapo tunaona panahitaji kupandwa nyasi? Kwa nini tusiwe na mazoea na utaratibu wa kusafisha mazingira yetu kwa ajili yetu sisi wenyewe na si kwa sababu ya kumvutia mgeni ambaye labda atakaa siku moja au mbili tu?
Tuna udhaifu mbaya sana sisi Waafrika.