Udhaifu wa msamaha wa “Nisamehe lakini....”

Zurie

Platinum Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,087
Reaction score
5,955
Msamaha ni jambo lenye nguvu sana. Msamaha ndio nguzo ya mahusiano yote duniani. Hata uhusiano wa Mungu na binadamu umejengwa kuzunguka msamaha kwa sababu binadamu tu viumbe wakosefu.

Katika msamaha kuna vitu vikuu vitatu. Aibu, Majuto, Matarajio. Aibu kwa kulazimika kuweka majivuno pembeni yaani kujishusha mbele ya uliyemkosea, majuto kwa kushindwa kufikia matarajio ya uliyemkosea na matarajio ya kufuta ama kusahau kosa kwa unayemuomba msamaha na kurudia hali ya awali.

Ni katika kipengele cha aibu/kujishusha ambapo msamaha huweza kwenda mrama na kushindwa kuonesha majuto wala matarajio ya muomba msamaha.

Kumbuka ulipokuwa mdogo na mwalimu au mzazi akakulazimisha kuomba msamaha kwa rafiki yako. Ukasema “samahani” huku umekunja sura, macho yakiangalia chini na mdomo ukiwa mzito.

Hali hii ni kwa sababu haukueleweshwa vema ni kwanini umekosea na kupelekea kuona kuna upendeleo katika kumchagua mwenzio kuwa ndiye anastahili kuombwa msamaha. Ni kutokana na matukio haya hata katika ukubwa wetu tunashindwa kuomba msamaha kwa ufasaha na kuhisi kuonewa ama kufanya kutimiza tu wajibu.

Chukua muda wako kutafakari muktadha mzima ukijaribu kujiweka katika nafasi ya uliyemkosea.

Nisamehe lakini...

Naamini umeshawahi kuomba ama kuombwa msamaha wa namna hiyo. Kama wewe ni mkosewa ulijisikiaje? Kama wewe ndiye ulikosea, kwanini uliomba msamaha wa namna hiyo?

Nisamehe lakini... ni msamaha uliojaa kujitetea kwa kuonesha kuwa hukuwa na jinsi bali kutenda hilo kosa, ama kujaribu kuonesha kuwa mkosewa ndiye aliyekulazimisha kutenda kosa, au kuonesha kuwa halikuwa kosa lako bali umeamua tu kuomba msamaha ili kumaliza mambo.

Misamaha ya namna hii huweza kuwavusha wahusika katika kipindi wanachopitia lakini haiponyi maumivu, hairudishi imani wala kumpa ahueni aliyekosewa. Hivyo unakuwa umenunua muda kwa gharama ya malimbikizo ya maumivu.

Je, msamaha wa kweli huwa vipi?

1. Unatambua tendo lililoleta uhitaji wa msamaha na kuonesha umiliki kamili. Mfano: Samahani nilipitia sehemu na rafiki zangu baada ya kutoka kazini. Nilitakiwa kutoa taarifa kama tulivyokubaliana kabla. Nimekukosea.

2. Unatambua madhara ya tendo hilo kwa mkosewa. Mfano: Najua utakuwa umenitafuta sana kupitia simu bila kunipata kwa sababu iliisha chaji. Pia hukulala na kunisubiri hadi niliporudi usiku sana.

3. Unaonesha dhahiri ni maadili ama makubaliano gani umevunja. Mfano: Sisi ni wanandoa na ni wajibu wetu kujulishana tulipo muda wote. Kwa kwenda mahali bila kukuambia nimevunja ahadi ya uwazi, kukukosea heshima, kukupa hofu, kukupotezea muda na kuonesha kutojali hisia zako.

4. Unaonesha majuto kwa kosa lililotokea. Mfano: Samahani kwa kukufanya unitafute bila mafanikio na kunisubiri sana. Samahani kwa maumivu niliyokupa. Ninathamini sana uhusiano wetu na ninatakiwa kuupa kipaumbele.

5. Unatoa ahadi ya matendo ya baadaye na jinsi gani unapanga kubadilika. Mfano: Naahidi kutorudia tena. Najua unaweza usiamini hili lakini nitahakikisha nakueleza kila sehemu nitakayoenda na kununua kifaa cha kutunza chaji ili kuweza kuchaji simu muda wote iwe rahisi kwako kunipata.

6. Onesha nini uko tayari kufanya kufidia kosa. Mfano: Sijui jinsi ya kukulipa kwa ufanyalo lakini ukinipa nafasi naomba wikiendi twende ufukweni pamoja.

Ni nini kinakosekana kwenye ombi hili la msamaha? Ni maneno “naomba unisamehe/ kubali msamaha huu/nisamehe bure”. Usimlazimishe mtu akusamehe, kukusikiliza tu ni jambo kubwa kwake hasa baada ya ulilomfanyia hivyo acha afanye uamuzi huo bila shinikizo.

Ombi dhaifu la msamaha hutokana na dhana kuwa mkosewa hastahili kuombwa msamaha lakini naamini msamaha ni ada unapomsababishia mtu maumivu au hasira aidha kwa kudhamiria au la.
 
Nakupenda.... Ila, samahani.
 
Back
Top Bottom