UDART yaongeza mabasi 70

UDART yaongeza mabasi 70

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,195
Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imepokea mabasi 70 kutoka China ambayo yataongeza nguvu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 16, 2018 wakati wa kupokea mabasi hayo yaliyokuja na meli ya MV Treasure katika Bandari ya Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, Charles Newe amesema ujio wa mabasi hayo utaifanya kampuni hiyo kuwa na mabasi 210.

Newe amesema mabasi hayo ambayo kila moja gharama yake ni dola 260, yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 150 hadi 160 yatasaidia pia katika kuongeza ajira, kuimarisha uchumi wa Tanzania na kurahisisha hali ya usafiri katika Jiji hilo.

“Bado kuna watu walikuwa wanatumia magari binafsi kutokana na magari yetu kujaa, lakini ujio wa mabasi haya naamini utawafanya wayaache nyumbani magari yao na kupunguza gharama kutoka Sh8,000 hadi Sh2,000 kwa siku kwa ajili ya usafiri binafsi,” amesema.

“Pia itasaidia kupunguza gharama za uendeshaji , kwani kutokana na kubeba abiria wengi kupita kiasi yamejikuta yakiaharibika mara kwa mara na badala ya basi kukaa miaka nane, linakaa miaka minne.”

Amesema pamoja na kuongezeka kwa mabasi hayo, utaratibu wa abiria kusimama utaendelea kwa kuwa ndio usafiri wa majiji katika miji yote duniani.

Mwananchi
 
Kwa shida ya usafiri wa hayo magari ninayoisikia huko, sitaki kuamini kama kuna magari 140 barabarani yanayotoa huduma kwa wananchi. Kama kweli magari hayo yapo barabarani then kuongeza hayo 70 kwa ajili ya kutatua changamoto iliyopo ni upuuzi mwingine ulio zoeleka
 
Urongo. Niko gerezani watu full. Hakuna pa kukanyaga na ni saa 7 ikifika jioni itakuwaje?
 
Msitufanye wajinga UDART mlipewa mkataba wa majaribio kwa miaka miwili,hiyo miaka miwili mmefeli mtihani mnaongeza mabasi ya nini? ondokeni hatuwataki,hata mkiongeza mabasi elfu kumi ondokeni
Hata Mimi nakubaliana na wewe - hawa jamaa waondoke; hiyo kazi imewashinda. Maana idadi ya abiria wanaokuwa vituoni asubuhi na jioni - inaonyesha kabisa hawa jamaa hawana "capacity" ya kuwabeba.
 
Hayo magari 210 yanapita wapi? In short huu usafiri wa mwendokasii bado una changamoto nyingi sana.

Kuna ukiritimba wa hali ya juu!
 
Kwa shida ya usafiri wa hayo magari ninayoisikia huko, sitaki kuamini lama kuna magari 250 barabarani yanayotoa huduma kwa wananchi. Kama kweli magari hayo yapo barabarani then kuongeza hayo 70 kwa ajili ya kutatua changamoto iliyopo ni upuuzi mwingine ulio zoeleka
UDART wana magari 140 tu na siyo 250 kama unavyosema na kwa ujio huo wa 70 sasa watakuwa na mabasi 210 kwa ujumla wake.
 
Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imepokea mabasi 70 kutoka China ambayo yataongeza nguvu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 16, 2018 wakati wa kupokea mabasi hayo yaliyokuja na meli ya MV Treasure katika Bandari ya Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, Charles Newe amesema ujio wa mabasi hayo utaifanya kampuni hiyo kuwa na mabasi 210.

Newe amesema mabasi hayo ambayo kila moja gharama yake ni dola 260, yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 150 hadi 160 yatasaidia pia katika kuongeza ajira, kuimarisha uchumi wa Tanzania na kurahisisha hali ya usafiri katika Jiji hilo.

“Bado kuna watu walikuwa wanatumia magari binafsi kutokana na magari yetu kujaa, lakini ujio wa mabasi haya naamini utawafanya wayaache nyumbani magari yao na kupunguza gharama kutoka Sh8,000 hadi Sh2,000 kwa siku kwa ajili ya usafiri binafsi,” amesema.

“Pia itasaidia kupunguza gharama za uendeshaji , kwani kutokana na kubeba abiria wengi kupita kiasi yamejikuta yakiaharibika mara kwa mara na badala ya basi kukaa miaka nane, linakaa miaka minne.”

Amesema pamoja na kuongezeka kwa mabasi hayo, utaratibu wa abiria kusimama utaendelea kwa kuwa ndio usafiri wa majiji katika miji yote duniani.

Mwananchi
niletee mabasi 3 japo sijui nitaendeshea barabara gani.
**aya ya 3 bado inaniumiza kichwa!
 
waongeze na route zitapakae mpaka huko tegeta na kila kona irahisishe usafiri foleni inachelewesha maendeleo kwakweli
 
“Pia itasaidia kupunguza gharama za uendeshaji , kwani kutokana na kubeba abiria wengi kupita kiasi yamejikuta yakiaharibika mara kwa mara na badala ya basi kukaa miaka nane, linakaa miaka minne.”

Kwani mlikuwa hamlijui hili siku zote!!?
 
Ushindani ni muhimu sana katika Mradi huu.DART wawe makini katika kusimamia uendeshaji wa huu Mradi kama ilivyopangwa.LKuwa kuwe na washindani wawili washindanishwe kutoa huduma.Swala hili la ku monopolise si la msingi aslani.Nijuavyo mimi hii ilikuwa iwe tenda ya Kimataifa tupate waendeshaji wenye uwezo na uzowefu.Lakini kumpa mwendeshaji mmoja ni kuuwa kabisa dhana ya kuwa na Mradi kama huu.Nimebahatika kuwa kwenye Majiji memgine ya Kimataifa na kuona jinsi gani wanaendesha miradi hii ya kusafirisha abiria wengi(Mass transit).Hakika hapa kwetu tunafanya dhihaka ya hali ya juu, jinsi tunavyouendesha mradi huu ni vichekesho vitupu.Usafiri huu hauna viwango vya mfumo wa BRT japo kimuundo ulipaswa kuwa hivyo,Lakini ujanja ujanja wa kibongo umedumaza juhudi za waasisi wa mfumo huu.Sina mashaka kabisa na Wakala husika kwamba wamefumbia macho na masikio haya tunayoyasema.Angalieni wingi wa abiria wakati wa asubuhi na jioni.Pia siyo dhambi wakafanya kazi masaa 24 hii itapunguza baadhi ya kero za kurudikana kwa kwenda na saa za kazi.Wapo wataalam wa kutosha tena wenye ujuzi na uwezo wa kushauri jinsi nzuri ya kuendesha Mradi huu watumieni kikamilifu.Tatizo la kadi za kielectronic lisiwe kikwazo wala kero ,Hizo kadi Ziuzwe hata kwa bei ya sh.Elfu kumi au hata Ishirini ili wale wasio hitaji kero za kukata tiketi mara kwa mara.Ondokeni na dhana ya kusema watu hawatamudu .Basi asiyemudu akubali kupanga foleni akisubiri kukata tiketi.Swala hili lirahisishwe kwa kiwango cha juu kukidhi matakwa ya ukusanyaji mapato lakini pia kukidhi hitaji la msafiri.
 
Ushindani ni muhimu sana katika Mradi huu.DART wawe makini katika kusimamia uendeshaji wa huu Mradi kama ilivyopangwa.LKuwa kuwe na washindani wawili washindanishwe kutoa huduma.Swala hili la ku monopolise si la msingi aslani.Nijuavyo mimi hii ilikuwa iwe tenda ya Kimataifa tupate waendeshaji wenye uwezo na uzowefu.Lakini kumpa mwendeshaji mmoja ni kuuwa kabisa dhana ya kuwa na Mradi kama huu.Nimebahatika kuwa kwenye Majiji memgine ya Kimataifa na kuona jinsi gani wanaendesha miradi hii ya kusafirisha abiria wengi(Mass transit).Hakika hapa kwetu tunafanya dhihaka ya hali ya juu.Usafiri huu hauna viwango vya mfumo wa BRT japo kimuundo ulipaswa kuwa hivyo.Sina mashaka kabisa na Wakala husika kwamba wamefumbia macho na masikio haya tunayoyasema.Angalieni wingi wa abiria wakati wa asubuhi na jioni.Pia siyo dhambi wakafanya kazi masaa 24 hii itapunguza baadhi ya kero.Wapo wataalam wa kutosha tena wenye ujuzi na uwezo wa kushauri jinsi nzuri ya kuendesha Mradi huu watumieni kikamilifu.Tatizo la kadi za kielectronic lisiwe kikwazo ,Ziuzwe hata kwa bei ya sh.Elfu kumi au hata Ishirini.O
 
Kwa shida ya usafiri wa hayo magari ninayoisikia huko, sitaki kuamini lama kuna magari 250 barabarani yanayotoa huduma kwa wananchi. Kama kweli magari hayo yapo barabarani then kuongeza hayo 70 kwa ajili ya kutatua changamoto iliyopo ni upuuzi mwingine ulio zoeleka
Ungetoa hata suluhisho nini kifanyike huenda ungesaidia kuliko hiki ulichoandika hapa.

Ulitaka wafanyaje?

Sent from my VFD 300 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom