UDART yaongeza mabasi 70

UDART yaongeza mabasi 70

Ajabu kabisa. Sisi watumiaji wa usafiri huu malalamiko yetu siku zote ni uchache wa mabasi sasa kama wameongeza 70, basi hii ni nafuu sana kwetu. Muhimu tu walete na kadi pia na kuboresha mapungufu madogo yaliyopo au waliyojifunza kwa kipindi walichofanya kazi....
Yaani humu sikuhizi mpaka panakera,tunatatuliwa matatizo yetu lakini hatuna shukrani hata chembe zaidi ni lawama,malalamiko,kebehi na upuuzi wote uliotujaa mioyoni.

Staili anayotumia magu inatufaa kabisa kwa asilimia 100,maana hatujui tunataka nini hivyo wala hakuna haja ya kuulizwa wala kudekezwa.

Tulipofikia hata tungeongozwa na malaika bado tungelalamika.
 
Tutapandaje xaxa wakati braza kafungia hela,kama zake vile
 
Ushindani ni muhimu sana katika Mradi huu.DART wawe makini katika kusimamia uendeshaji wa huu Mradi kama ilivyopangwa.LKuwa kuwe na washindani wawili washindanishwe kutoa huduma.Swala hili la ku monopolise si la msingi aslani.Nijuavyo mimi hii ilikuwa iwe tenda ya Kimataifa tupate waendeshaji wenye uwezo na uzowefu.Lakini kumpa mwendeshaji mmoja ni kuuwa kabisa dhana ya kuwa na Mradi kama huu.Nimebahatika kuwa kwenye Majiji memgine ya Kimataifa na kuona jinsi gani wanaendesha miradi hii ya kusafirisha abiria wengi(Mass transit).Hakika hapa kwetu tunafanya dhihaka ya hali ya juu.Usafiri huu hauna viwango vya mfumo wa BRT japo kimuundo ulipaswa kuwa hivyo.Sina mashaka kabisa na Wakala husika kwamba wamefumbia macho na masikio haya tunayoyasema.Angalieni wingi wa abiria wakati wa asubuhi na jioni.Pia siyo dhambi wakafanya kazi masaa 24 hii itapunguza baadhi ya kero.Wapo wataalam wa kutosha tena wenye ujuzi na uwezo wa kushauri jinsi nzuri ya kuendesha Mradi huu watumieni kikamilifu.Tatizo la kadi za kielectronic lisiwe kikwazo ,Ziuzwe hata kwa bei ya sh.Elfu kumi au hata Ishirini.O
Daah...watu mnapenda kuandika !
 
Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imepokea mabasi 70 kutoka China ambayo yataongeza nguvu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 16, 2018 wakati wa kupokea mabasi hayo yaliyokuja na meli ya MV Treasure katika Bandari ya Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, Charles Newe amesema ujio wa mabasi hayo utaifanya kampuni hiyo kuwa na mabasi 210.

Newe amesema mabasi hayo ambayo kila moja gharama yake ni dola 260, yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 150 hadi 160 yatasaidia pia katika kuongeza ajira, kuimarisha uchumi wa Tanzania na kurahisisha hali ya usafiri katika Jiji hilo.

“Bado kuna watu walikuwa wanatumia magari binafsi kutokana na magari yetu kujaa, lakini ujio wa mabasi haya naamini utawafanya wayaache nyumbani magari yao na kupunguza gharama kutoka Sh8,000 hadi Sh2,000 kwa siku kwa ajili ya usafiri binafsi,” amesema.

“Pia itasaidia kupunguza gharama za uendeshaji , kwani kutokana na kubeba abiria wengi kupita kiasi yamejikuta yakiaharibika mara kwa mara na badala ya basi kukaa miaka nane, linakaa miaka minne.”

Amesema pamoja na kuongezeka kwa mabasi hayo, utaratibu wa abiria kusimama utaendelea kwa kuwa ndio usafiri wa majiji katika miji yote duniani.


Mwananchi

huenda m ndo sijaelewa dola 260 ?

260x2300= haizidi 700,000/=

au takwim zimekosewa?
 
Simon Group wahuni tu, tunataka apate mshindani haraka, labda kama ameiweka serikali kwenye mfuko wa boxer!!
 
UDART au DART? Jamani nani mwenye hisa nyingi ?
 
650 Feri hadi Kimara, jumlisha 400 Kimara hadi Mbezi inakuwa ngapi na wewe? Daladala ni bei gani ruti hiyo? Siyo 800?
Kwahiyo wakiweka card utapanda 650 feri-mbezi?..si utalipia hivyohivyo 1050 bado!..
 
Kwa shida ya usafiri wa hayo magari ninayoisikia huko, sitaki kuamini kama kuna magari 140 barabarani yanayotoa huduma kwa wananchi. Kama kweli magari hayo yapo barabarani then kuongeza hayo 70 kwa ajili ya kutatua changamoto iliyopo ni upuuzi mwingine ulio zoeleka
Mabasi yapo 200 na sio 170. Lakini pia capacity ya shirika ni kuongeza mabasi 70 na sio kama fikra zako zinavyokutuma. So unapofikiria kuanza kulaum kuliko kupongeza think twice. Maana hakipo kizuri serikali ya 5 inafanya mkasifia
 
waongeze na route zitapakae mpaka huko tegeta na kila kona irahisishe usafiri foleni inachelewesha maendeleo kwakweli
Barabara zinazofegemewa kuwa nanudart ni kilwa, morogoro, samnjoma,na mwenge tegeta, ila ni long term plan. Inayofuata ni kilwa. Nafikiri itakuja mandela na baadae mwenge tegeta
 
Isilete huu uozo uitwao UDART hapa. Kampuni inayoendeshwa kizembe kuliko zote Tanzania. Leo tumebanana kwenye basi kama wakimbizi wakati tumelipa nauli kubwa kuliko ya daladala. Shithole vompany. Shithole management
 
Back
Top Bottom