ecolizer baba
Member
- Sep 29, 2010
- 88
- 310
Watanzania sisi tupo bado kwenye process wa evaluation ya kuwa binadamu kamili bado hatujakamilika.Tunachokiweza Watanzania ni kifo tu mengine kamwe hatuwezi. Huu mradi ulikuwa mradi bora na kuigwa lakini kama kawaida ya mwafrika mtanzania ameshauharibu. Nasisitiza tunachokiweza watanzania ni kifo tu.
Inashangaza kuwa eti vituo vyote sh 50, 100 na 200 hazipo. Zimeenda wapi?? Au wanataka kutuambia kuwa hiziz silver zinataka kuondoshwa kwenye mzunguko wa BOT?? Wizi wizi wizi.
So what?Wiki kadhaa pia Nimekutana hicho unachokisema
halafu huduma zao ni mbovu mbovu mno mno ktk maeneo haya;
1. Kukaa vituoni mida mrefu (hadi saa 1) bila kupata usafiri.
2. Kujaza abiria kwa kaisi cha kutisha hadi kukosekana hewa ndani ya mabasi yao.
3. Lugha chafu sana kwa wakataji tiketi (hasa kituo cha kimara terminal)
4. Hakuna huduma za kijamii ktk vituo vyao (ie washroom na maji ya kunawa ktk vi tank)
sisi tumelaaniwa kwa wiziKitu ambacho naona ni kuwa huenda jamaa walikuwa na namna ya kupata hela bila kuibia abiria ila sasa huo mrija umezibwa kwahio imebidi wageukie abiria na kuanza kuwapiga mchana kweupe na maboss wao wamebariki hilo bila shaka.
Walivyoacha kutumia electonic devices kwenye kuhakiki tiketi nilijua tushapigwa...Siku za hivi karibuni hawa watu wa mabasi yaendayo Kasi(UDART) Wameanza wizi wa wazi wazi. Ukienda kukatq ticket halafu ukatoa hela kubwa zaidi ya gharama ya ticket yako wanakuambia uwaongezee 150 au 200 ndipo upewe change yako. Kama huna itabidi wakusubirishe. Na kama una haraka zako utachukua ticket yako na kuwaachia hiyo 150 au 200.
Kwa hesabu za haraka haraka unaweza ona ni hela ndogo sana hiyo 150 hadi 200 kwa mtu mmoja. Lakini ukikaaa na kufikiria kama endapo abiria 1000 wataachia hiyo 150 hadi 200 basi jumla yake ni 150,000 hadi 200,000. Maana ni vituo vyote vya mwendokasi wanafanya hivyo.
Sasa huu ni wizi wa mchana kweupe. Hizi hujuma zimeanza tokea kuanza kwa mwaka mpya. Hakukuwa na tatizo la change mwaka jana na kurudi nyuma. SUMATRA, LATRA pamoja na TAMISEMI liangalieni hili. Hawa UDART wanatuibia Watanzania.
Inaanza lini hii.Dawa ni Ncard waanze kazi tofauti na hapo mapato yataendelea potea
https://www.facebook.com/halafu huduma zao ni mbovu mbovu mno mno ktk maeneo haya;
1. Kukaa vituoni mida mrefu (hadi saa 1) bila kupata usafiri.
2. Kujaza abiria kwa kaisi cha kutisha hadi kukosekana hewa ndani ya mabasi yao.
3. Lugha chafu sana kwa wakataji tiketi (hasa kituo cha kimara terminal)
4. Hakuna huduma za kijamii ktk vituo vyao (ie washroom na maji ya kunawa ktk vi tank)