Hebu na sisi wananchi kama wadau tuumize kichwa kidogo kwa kujiuliza; je, mradi huu ukifa kutakuwa na faida gani? Ni nani ataumia? Je, ni kweli usafiri wa daladala uliokuwapo mwaka mmoja na nusu tu uliopita kati ya Mbezi/Kimara hadi Posta/Kivukoni/Kariakoo ulikuwa bora kuliko huu wa MWENDOKASI?
Watoto/wanafunzi wanauchukuliaje mradi huu wa MWENDOKASI? Wazazi tuliokuwa tukilalamikia unyanyaswaji wa watoto wetu uliokuwa ukifanywa na makondakta bado tunalalamika leo hii? Je, daladala zikirejea kwenye hizo 'monopolized' routes watoto wetu watapewa huduma kama wanayopewa leo hii?
Je, ni kweli kwamba miradi (ya huduma kwa umma) inayoendeshwa au iliyowahi kuendeshwa na wageni (Wahindi/Wazungu) ilifanikiwa? Na kwa kiwango gani? (NOTE: NET GROUP SOLUTION versus TANESCO and CITY WATER versus NUWA).
Kwa UDART/Mwendokasi; nini kifanyike? Wameshindwa kuongeza idadi ya mabasi au kuna urasimu fulani? Ni kweli ni wao ndio hawataki kuuza kadi za usafiri? Yaani hawapendi kuwapa huduma bora abiria wao ambao kwao ni wafalme? Nauli inayotozwa inakidhi uendeshaji wa mradi mkubwa na wa kisasa kama huu?
Tukipewa majibu ya maswali haya tunaweza kutoa 'uamuzi' kuwa UDART wameshindwa au la!
NI MTAZAMO TU!