UDART imeshindwa kutoa huduma bora

UDART imeshindwa kutoa huduma bora

sanachanya

Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
9
Reaction score
10
Kuna tatizo kubwa katika utoaji huduma kwa mabasi ya mwendokasi, ni dhahiri kwamba wahitaji wa huduma ni wengi na watoaji wa huduma wamezidiwa labda kwasababu ya monopoly power ya route wanayoenjoy na hivi hakuna competition wanafanya wanavyojitakia bila kuwa na ubunifu na kumbuka hii ni pre payment service. Kero kubwa kila Siku ni

1. Kupakia abiria kupita kiasi. Mabasi yanajaza na watu husimama hata sehemu iaiyoruhusiwa kusimamisha, hii ni hatari kwa usalama wa abiria.

2. Mabasi kupita hayana watu na kuacha watu wamesimama vituoni. Ni kihoja sana unapokuta gari linatoka jangwani kwenda kuanza route kimara au kivukoni ama gerezani kupita yanaacha watu kisa yanaenda kuanza route.

3. Watu kusimama vituoni muda mrefu. Kwa mfano route ya kimara Morocco magari ni shida mtu unakaa kituoni nusu saa nzima kusubiri gari.

4. Misururu mirefu katika ukatishaji wa tiketi hili pia limekua jambo la kawaida sana.
5. Usumbufu kwa wenye kadi kwani kuna vituo havitoi kabisa huduma za kadi kama unataka kurecharge account yako mfano kituo cha mwanamboka na Urafiki. Pia wameamua kufuta kabisa mauzo ya kadi kwa wateja wapya kwasababu wanazojua wao.

NINI KIFANYIKE
1. Serikali ipitie upya mkataba huu wa usafirishaji na kuruhusu kampuni nyingine kujihusisha na usafirishaji huu hata ziwe kampuni tatu za usafirishaji kampuni zenye uwezo huo zipo. Monopoly kwa wakati mwingine inapelekea inefficiency na ndicho tunachokiona sasa. Na nadhani hili litawaamsha hawa jamaa.

2. Kuwe na ufuatiliaji wa huduma za huu usafiri na mawakala wa serikali sio kuja kufungua miradi na mbwembwe nyingi ili kupata sifa za kisiasa baada ya hapo ufanisi ni sifuri.

3. Watumiaji wa huduma hii tuendelee kulalamikia huduma mbovu zinazotolewa kwa kupaza sauti popote pale hadi tupate huduma tulizoahidiwa.

Mwisho huduma hii imekuwa kero sana kuliko ahadi ya mapinduzi ya usafiri tuliyohubiriwa na imekuwa ni kawaida viongozi kuhubiri huduma bora kwenye sekta mbalimbali kinyume na uhalisia.

TUJISAHIHISHE.
 
kituo cha dit kisutu kilifululiza siku tatu hawarecharge kadi

kwa sasa wanadai magari mabovu waongee na UDA wawakodishe magari
 
Yaani unasimama kituoni mpaka inasinzia hakuna hata pa kukaa watuwekee viti
 
yaani wakati ni hovyo kabisa.unakaa kituoni muda mrefu halafu ni asbh.magari mengine yanapita tu esp vituo vya kati ya kimara na ubungo ni shida sn.
 
yaani washindani kwenye vituo hivyo hivyo?
ukataji ticket?
mi naona mradi ungeongezewa mtaji ili walete mabasi mengi
 
Tatizo linaanzia Sumatra kwa kupanga Bei isiyo reflect gharama halisi za Magari hayo!

Tshs. 650 kutoka Kivukoni mpaka Mbezi Mwisho

UDART inabidi wafanye Uhuni mwingi ili kuweza ku maintain Profit margin Yao!

Kwenye Treni ya Ubungo na Pugu waliitsha Mkutano wa hadhara Watu wapange bei kwa Njia ya kidemokrasia sio kitaalam through cost analysis

Walalahoi wengi wakashinda kwa kishindo bei ikawa Tsh. 400 kwa safari ya Dsm steshen-Pugu station Mkoa wa Pwani!!!

Matokeo yake wakashindwa kujiendesha ikabidi bei ipandishwe kienyeji Ikawa Tsh 600 na bado Huduma zake mbaya

Viwango vya nauli vinapangwa kijamaa Halafu mnategemea kupata Huduma kwa Viwango vya kibepari
 
Yaani hii yamagari kupita watu kero moja kubwa sana gari lipo empty watu wamejazana vituoni lenyewe linatoka mjini kwenda kimara au kimara kwenda mjini kuanzisha ruti mpya
 
Juzi tarehe 30/10/2017 usiku route ya Kivukoni -Kimara hali ilikuwa mbaya sana.

Kulikuwa na mabasi machache, nayo pia yalikuwa yana tumia muda mrefu kugeuza yakifika Kivukoni, yakirudi yamejaza kiasi cha kuhatarisha kuvunjwa mlango.

Tatizo la kukosa huduma ya kuongeza salio ktk kadi limekuwa sugu hasa vituo vya Kibo, Ubungo Maji lango la kutokea Kimara, Posta ya Zamani lango la kutokea Azania Waterfront, na vituo vingine vingi hasa vya katikati.

Watu tunabanana mno, rahisi kuambukizana Herpetitis, TB, Uti wa mgongo na magonjwa mengine ya ngozi. Na joto la sasa watu mnapakazana jasho ambalo ni hatari tupu kwa afya.
 
Na waruhusu maxmalipo isaidie ukataji ticket mtu aende kituoni kupanda bus si kukata ticket na waweke machine za kukata ticket vituoni mbona zipo
 
Washa-monopolize route kwa hiyo wanafanya watakalo....
 
Huu mradi ulikuwa sawa Ila rushwa iliyowaingiza akina kisena from ginnery to mabasi udart ilinifanya nijue waafrica Hatuko serious
 
Yaani unasimama kituoni mpaka inasinzia hakuna hata pa kukaa watuwekee viti
😀😀😀 na katv tuwe tunaangalia taarifa ya habari....mtu unakaa kituoni mpk unasahau...wafanyakaz ni kujipitisha tu na vikaratas vyao .....wengine wanachati tu....sioni wanachofanya...na madereva wengine kuacha abiria vituon
 
Mradi huu uliharakishwa mno kuanzishwa bila kuufanyia utafiti wa kweli kuhusu uendeshaji wake,ndio tatizo wanasiasa wanapokuwa wanafukuzia matakwa yao yafikiwe they don't think about side effects zake.ujenzi wa mradi huu haukujengwa kwa kufuata taratibu,majiji mengi hapa Afrika yana miradi kama hii ila ukifananisha jinsi ilivyojengwa na uendeshaji wake wa kwetu ni vichekesho vitupu.ufumbuzi hapa tuanze upya na siasa iwekwe pembeni na wataalamu ndio washike hatamu za mradi huu.
 
Tulisema awali kabisa, UDART itakwama na itakuwa kuliko daladala za Mbagala kabla ya mradi kuanza. Hatukujiuliza wala kutafiti kwanini UDA na Ikarus zake ilikufa? Hatukuwa tayari kufanya utafiti wa changamoto, mahitaji na matumizi! Nilishangaa sana kituo cha maegesho na matengenezo kuwekwa pale Jangwani mahala ambapo mafuriko hayajadhibitiwa mpaka leo najiuliza waliwaza nini!? au ni mradi ndani ya mradi - mabasi yafe tupige hela za kuyatengeneza kama sio kununua mapya!!! Kwa hakika yapo matatizo katika mfumo mkuu ndio yanayosababisha miradi mingi kushindwa kama sio kushindikana. Hatujiulizi kwanini wenye viwanda wengi wanaajiri wahindi katika nafasi za kiutawala badala ya mawia wenzetu? Tunadharauliana na tunapeana kazi kindugu sio ki weledi. Hebu tutazame tuna kina Kimei wangapi? Je waliopo wengine wa kariba yake kwanini hawasikiki wamezingirwa na nini? Sijawahi kuona mradi ulioanzishwa na hii serikaCCM ukiendelea zaidi ya kunufaishana wao kwa wao.
Acheni tuendelee na mihemko, majungu na mipasho labda tutafika!
 
Tatizo linaanzia Sumatra kwa kupanga Bei isiyo reflect gharama halisi za Magari hayo!

Tshs. 650 kutoka Kivukoni mpaka Mbezi Mwisho

UDART inabidi wafanye Uhuni mwingi ili kuweza ku maintain Profit margin Yao!

Kwenye Treni ya Ubungo na Pugu waliitsha Mkutano wa hadhara Watu wapange bei kwa Njia ya kidemokrasia sio kitaalam through cost analysis

Walalahoi wengi wakashinda kwa kishindo bei ikawa Tsh. 400 kwa safari ya Dsm steshen-Pugu station Mkoa wa Pwani!!!

Matokeo yake wakashindwa kujiendesha ikabidi bei ipandishwe kienyeji Ikawa Tsh 600 na bado Huduma zake mbaya

Viwango vya nauli vinapangwa kijamaa Halafu mnategemea kupata Huduma kwa Viwango vya kibepari

WEWE hujielewi kabisa! basi la UDA kubwa linabeba hadi watu 200 kutoka kimara mpaka kvukon km 15
mafuta lita 2 tu hapo! sh elfu 4
watu 200 unapata 130,000


UDA hawajielewi waroho wakubwa! mungu atawalaani
 
aah mkoa wangu wa dalisalama, kuna mtu anasema selikali haina dila wakati watoto wetu wanasoma shule bule, in mkoromije's voice
 
Back
Top Bottom