UDART imeshindwa kutoa huduma bora

UDART imeshindwa kutoa huduma bora

yaani washindani kwenye vituo hivyo hivyo?
ukataji ticket?
mi naona mradi ungeongezewa mtaji ili walete mabasi mengi
Wapo wenye mitaji wapewe nafasi kama tatizo lao kubwa ni mtaji. Na nia ya ushindani ni mtumiaji huduma afaidike
 
Tatizo linaanzia Sumatra kwa kupanga Bei isiyo reflect gharama halisi za Magari hayo!

Tshs. 650 kutoka Kivukoni mpaka Mbezi Mwisho

UDART inabidi wafanye Uhuni mwingi ili kuweza ku maintain Profit margin Yao!

Kwenye Treni ya Ubungo na Pugu waliitsha Mkutano wa hadhara Watu wapange bei kwa Njia ya kidemokrasia sio kitaalam through cost analysis

Walalahoi wengi wakashinda kwa kishindo bei ikawa Tsh. 400 kwa safari ya Dsm steshen-Pugu station Mkoa wa Pwani!!!

Matokeo yake wakashindwa kujiendesha ikabidi bei ipandishwe kienyeji Ikawa Tsh 600 na bado Huduma zake mbaya

Viwango vya nauli vinapangwa kijamaa Halafu mnategemea kupata Huduma kwa Viwango vya kibepari
Naamini kwa uhitaji mkubwa wa hii huduma tender ikitangazwa kwa bei hiihii atapatikana mtoa huduma bora.
 
WEWE hujielewi kabisa! basi la UDA kubwa linabeba hadi watu 200 kutoka kimara mpaka kvukon km 15
mafuta lita 2 tu hapo! sh elfu 4
watu 200 unapata 130,000


UDA hawajielewi waroho wakubwa! mungu atawalaani

Ungekuwa umewahi kumiliki walau Bajaji ungejijua ulivyo Bwege !

Gharama za uendeshaji wa Magari ya Abiria ukimuuliza Mpumbavu yoyote atakutajia Fuel tu kwa kuwa ni Mpumbavu !

eti kutoka Kivukoni mpaka Kimara ni Lita mbili , Wewe utakuwa Msukuma Guta Mstaafu ndio sababu hujui hata CC za hayo Magari lakin umekurupuka tu!
 
Naamini kwa uhitaji mkubwa wa hii huduma tender ikitangazwa kwa bei hiihii atapatikana mtoa huduma bora.

Tender ilitangazwa akashinda Simon Group!
Sasa hivi Simon group sio tu mwendeshaji pia ni mwanahisa wa huo Mradi
 
Tulisema awali kabisa, UDART itakwama na itakuwa kuliko daladala za Mbagala kabla ya mradi kuanza. Hatukujiuliza wala kutafiti kwanini UDA na Ikarus zake ilikufa? Hatukuwa tayari kufanya utafiti wa changamoto, mahitaji na matumizi! Nilishangaa sana kituo cha maegesho na matengenezo kuwekwa pale Jangwani mahala ambapo mafuriko hayajadhibitiwa mpaka leo najiuliza waliwaza nini!? au ni mradi ndani ya mradi - mabasi yafe tupige hela za kuyatengeneza kama sio kununua mapya!!! Kwa hakika yapo matatizo katika mfumo mkuu ndio yanayosababisha miradi mingi kushindwa kama sio kushindikana. Hatujiulizi kwanini wenye viwanda wengi wanaajiri wahindi katika nafasi za kiutawala badala ya mawia wenzetu? Tunadharauliana na tunapeana kazi kindugu sio ki weledi. Hebu tutazame tuna kina Kimei wangapi? Je waliopo wengine wa kariba yake kwanini hawasikiki wamezingirwa na nini? Sijawahi kuona mradi ulioanzishwa na hii serikaCCM ukiendelea zaidi ya kunufaishana wao kwa wao.
Acheni tuendelee na mihemko, majungu na mipasho labda tutafika!

Hebu na sisi wananchi kama wadau tuumize kichwa kidogo kwa kujiuliza; je, mradi huu ukifa kutakuwa na faida gani? Ni nani ataumia? Je, ni kweli usafiri wa daladala uliokuwapo mwaka mmoja na nusu tu uliopita kati ya Mbezi/Kimara hadi Posta/Kivukoni/Kariakoo ulikuwa bora kuliko huu wa MWENDOKASI?

Watoto/wanafunzi wanauchukuliaje mradi huu wa MWENDOKASI? Wazazi tuliokuwa tukilalamikia unyanyaswaji wa watoto wetu uliokuwa ukifanywa na makondakta bado tunalalamika leo hii? Je, daladala zikirejea kwenye hizo 'monopolized' routes watoto wetu watapewa huduma kama wanayopewa leo hii?

Je, ni kweli kwamba miradi (ya huduma kwa umma) inayoendeshwa au iliyowahi kuendeshwa na wageni (Wahindi/Wazungu) ilifanikiwa? Na kwa kiwango gani? (NOTE: NET GROUP SOLUTION versus TANESCO and CITY WATER versus NUWA).

Kwa UDART/Mwendokasi; nini kifanyike? Wameshindwa kuongeza idadi ya mabasi au kuna urasimu fulani? Ni kweli ni wao ndio hawataki kuuza kadi za usafiri? Yaani hawapendi kuwapa huduma bora abiria wao ambao kwao ni wafalme? Nauli inayotozwa inakidhi uendeshaji wa mradi mkubwa na wa kisasa kama huu?

Tukipewa majibu ya maswali haya tunaweza kutoa 'uamuzi' kuwa UDART wameshindwa au la!

NI MTAZAMO TU!
 
5. Usumbufu kwa wenye kadi kwani kuna vituo havitoi kabisa huduma za kadi kama unataka kurecharge account yako mfano kituo cha mwanamboka na Urafiki. Pia wameamua kufuta kabisa mauzo ya kadi kwa wateja wapya kwasababu wanazojua wao.


Kuna vituo ambavyo huwa vina matatizo ya kusoma kadi kama kisutu muda mwingi mashine zinakuwa hazifanyi kazi na kuwafanya wanaotumia kadi kushindwa ku exit ili fedha yao isiendelee kulambwa
 
Ukiwa hauna mshindani lazima udumae akili..
 
Tatizo linaanzia Sumatra kwa kupanga Bei isiyo reflect gharama halisi za Magari hayo!

Tshs. 650 kutoka Kivukoni mpaka Mbezi Mwisho

UDART inabidi wafanye Uhuni mwingi ili kuweza ku maintain Profit margin Yao!

Kwenye Treni ya Ubungo na Pugu waliitsha Mkutano wa hadhara Watu wapange bei kwa Njia ya kidemokrasia sio kitaalam through cost analysis

Walalahoi wengi wakashinda kwa kishindo bei ikawa Tsh. 400 kwa safari ya Dsm steshen-Pugu station Mkoa wa Pwani!!!

Matokeo yake wakashindwa kujiendesha ikabidi bei ipandishwe kienyeji Ikawa Tsh 600 na bado Huduma zake mbaya

Viwango vya nauli vinapangwa kijamaa Halafu mnategemea kupata Huduma kwa Viwango vya kibepari

Sio kweli kwamba Kivukoni - Mbezi Mwisho ni Tshs. 650.
Kivukoni - Kimara Mwisho ni 650 sawa na Kimara Mwisho - Mbezi ni 400
 
abiria kuwa wengi gerezani huku basi zimepaki kusubiri muda wa route.
 
Hebu na sisi wananchi kama wadau tuumize kichwa kidogo kwa kujiuliza; je, mradi huu ukifa kutakuwa na faida gani? Ni nani ataumia? Je, ni kweli usafiri wa daladala uliokuwapo mwaka mmoja na nusu tu uliopita kati ya Mbezi/Kimara hadi Posta/Kivukoni/Kariakoo ulikuwa bora kuliko huu wa MWENDOKASI?

Watoto/wanafunzi wanauchukuliaje mradi huu wa MWENDOKASI? Wazazi tuliokuwa tukilalamikia unyanyaswaji wa watoto wetu uliokuwa ukifanywa na makondakta bado tunalalamika leo hii? Je, daladala zikirejea kwenye hizo 'monopolized' routes watoto wetu watapewa huduma kama wanayopewa leo hii?

Je, ni kweli kwamba miradi (ya huduma kwa umma) inayoendeshwa au iliyowahi kuendeshwa na wageni (Wahindi/Wazungu) ilifanikiwa? Na kwa kiwango gani? (NOTE: NET GROUP SOLUTION versus TANESCO and CITY WATER versus NUWA).

Kwa UDART/Mwendokasi; nini kifanyike? Wameshindwa kuongeza idadi ya mabasi au kuna urasimu fulani? Ni kweli ni wao ndio hawataki kuuza kadi za usafiri? Yaani hawapendi kuwapa huduma bora abiria wao ambao kwao ni wafalme? Nauli inayotozwa inakidhi uendeshaji wa mradi mkubwa na wa kisasa kama huu?

Tukipewa majibu ya maswali haya tunaweza kutoa 'uamuzi' kuwa UDART wameshindwa au la!

NI MTAZAMO TU!
Ukiukumbuka mwanzo wa RETCO utajua nilichomaanisha katika sekta ya usafiri. Alipoondoka yule mhindi aliyekuwa akisimamia uanzishwaji mradi ule nitajie ni RETCO ipi ilibaki zaidi ya ile ya Iringa? Ukiangalia makampuni ya watu binafsi utanielewa vema. Hatutaki kujifunza wala hatujifunzi kutokana na makosa ya awali. Tukiendelea kutanguliza mahaba na ushabiki hakika hatutavuka. Kwanini hatuangalii wanaofanikiwa tunapenda kuangalia na kuwakumbatia wanaofeli? Lugha ya tuwape muda... tujiulize ni kina nani tunawapa muda... mpaka lini?

Unaweza kutumia nguvu nyingi sana kutetea kitu ambacho utetezi pekee hautoshi naomba kukuuliza kitu kimoja tu;
Pale Newera pameendelezwa kwa mafanikio? Tukiona mafanikio yaliyofanyika hapo basi inamaanisha kwamba UDART nayo itaendelezwa vema.

Midhali walioua UDA wangalimo sioni jipya.
 
Kuna tatizo kubwa katika utoaji huduma kwa mabasi ya mwendokasi, ni dhahiri kwamba wahitaji wa huduma ni wengi na watoaji wa huduma wamezidiwa labda kwasababu ya monopoly power ya route wanayoenjoy na hivi hakuna competition wanafanya wanavyojitakia bila kuwa na ubunifu na kumbuka hii ni pre payment service. Kero kubwa kila Siku ni

1. Kupakia abiria kupita kiasi. Mabasi yanajaza na watu husimama hata sehemu iaiyoruhusiwa kusimamisha, hii ni hatari kwa usalama wa abiria.

2. Mabasi kupita hayana watu na kuacha watu wamesimama vituoni. Ni kihoja sana unapokuta gari linatoka jangwani kwenda kuanza route kimara au kivukoni ama gerezani kupita yanaacha watu kisa yanaenda kuanza route.

3. Watu kusimama vituoni muda mrefu. Kwa mfano route ya kimara Morocco magari ni shida mtu unakaa kituoni nusu saa nzima kusubiri gari.

4. Misururu mirefu katika ukatishaji wa tiketi hili pia limekua jambo la kawaida sana.
5. Usumbufu kwa wenye kadi kwani kuna vituo havitoi kabisa huduma za kadi kama unataka kurecharge account yako mfano kituo cha mwanamboka na Urafiki. Pia wameamua kufuta kabisa mauzo ya kadi kwa wateja wapya kwasababu wanazojua wao.

NINI KIFANYIKE
1. Serikali ipitie upya mkataba huu wa usafirishaji na kuruhusu kampuni nyingine kujihusisha na usafirishaji huu hata ziwe kampuni tatu za usafirishaji kampuni zenye uwezo huo zipo. Monopoly kwa wakati mwingine inapelekea inefficiency na ndicho tunachokiona sasa. Na nadhani hili litawaamsha hawa jamaa.

2. Kuwe na ufuatiliaji wa huduma za huu usafiri na mawakala wa serikali sio kuja kufungua miradi na mbwembwe nyingi ili kupata sifa za kisiasa baada ya hapo ufanisi ni sifuri.

3. Watumiaji wa huduma hii tuendelee kulalamikia huduma mbovu zinazotolewa kwa kupaza sauti popote pale hadi tupate huduma tulizoahidiwa.

Mwisho huduma hii imekuwa kero sana kuliko ahadi ya mapinduzi ya usafiri tuliyohubiriwa na imekuwa ni kawaida viongozi kuhubiri huduma bora kwenye sekta mbalimbali kinyume na uhalisia.

TUJISAHIHISHE.

Unaitoa wap nguv ya kuhoji mambo kama haya. Wachochez siwatak kwenye mkoa wangu. Nenden mkafanyie siasa hukoo mikoani kwenu. Wanasiasa mnachosahau ni kwamba zama zmebadilika sana utafanya siasa za muda mfupi baada ya hapo wananchi watakudharau. [emoji23]
 
Back
Top Bottom