UDA ya Simon Group na Vipanya

Megawatt B

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
259
69
UDA ikiwa na mwekezaji mpya Simon Group, hivi karibuni imeingiza magari mapya 15 aina ya TATA na pembeni kuna nembo ya Marcopolo. sina tatizo na aina ya gari wala nembo, tatizo langu ni muundo wa magari yenyewe, hivi kweli kwa karne hii Town buses zinaagizwa za mlango mmoja kama vipanya? watu waendelee kusukumana wakati wa kuingia na kuteremka kwenye basi? nilidhani mwekezaji Simon group atakuja kisasa zaidi na kuwa na magari yenye hadhi ya Town au City Bus yenye milango miwili, yaani wakuingia na wakutokea. sijui wadau mna maoni gani juu ya hili na ikiwezekana yulijadili maana nilimsikia Kasena (MD wa Simon Group) anajigamba wataleta mabsi mengine 200 kufikia mwezi Machi 2013.
 
huyu simon group si alituhumiwa kwa rushwa huyu? Bado kapewa tenda ya kuendesha UDA mh! Mafisadi kiboko
 
Please jamani,naitwa robert kisena sio kasena,na kuhusu usafiri huu ni mwanzo na tutaboresha zaidi.asanteni
 
nlisoma habari leo ya jtatu iliyopita. UDA wanasema wataleta mabasi ya wanawake, ya watu wenye hela yatakayokua na starehe ndan yake na ya wanafunzi. ok. kiukwel haya mabasi ni mabaya kuanzia rangi hadi shape, kama wataleta hayo mengine inabidi wafikirie hilo.
 
Back
Top Bottom