Ukiangalia na kufatilia kiundani hii nchi kuna kikundi cha watu wachache sana wanayoitafuna barbara, kila deal zinazotokea majina ni yaleyale yanajirudia, Lakini kuna maswali machache ambayo Watanzania inatupasa kujiuliza
1) Kazi hasa Ya Usalama wa Taifa ni nini hasa? mimi nadhani hivi vitu vyote vinavyotokea wanavijua na wanavifanyia report, sasa ikitokea utekelezaji wa ripoti zao haufanywi wao kazi yao ni kukaa kimya na kuacha nchi iyumbe?
2) Hivi ni kweli Watanzania Hatuna Solution nyingine/Mbadala ya kusolve haya matatizo zaidi ya kuhabarishana kwenye mitandao na kilamtu anaondoka anasonya? Hiyo ndio hatua yetu ya mwisho kabisa
3) Kitu cha Muhimu kwa sasa kwaWatanzania sio kugombea uraisi bali ni kuitoa CCM madarakani kwa NJIA YOYOTE ILE, Tanzania inapaswa kuzaliwa upya, Chadema na watu wote wenye kuitakia mema hii nchi hebu unganeni kwenye hili la kuikomba Tanzania, Ukombozi wa Tanzania ni wamuhimu zaidi ya Siasa, Ukombozi unaanzishwa na Mtu mmoja, Watanzania tunasubiri kauli kama za Mh Lema zenye kutia HAmasa na uzalendo
SAA YA UKOMBOZI NI SASA