UDA Scandal Files: Part I (Revealing) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDA Scandal Files: Part I (Revealing)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Aug 12, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Since the story of UDA became part of public discourse, there has been a lot of confusion as to the true facts of what happened. In the process, the truth became a victim of politics. This document you see here is part of an effort to put the facts out there for the public record ahead of political posturing. Hopefully, as a consequence, a rational, non-reactionary conversation about this issue can emerge...

  NOTE: This' just part I, follow the series...


  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  asante invisible kwa kazi nzuri nazipitia
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Sasa hapa Simon Group wanahudhuria kama nani wakati hawajakabidhiwa rasmi na inakuwaje wakati bado kuna utata kuhusu malipo maana hata baadhi ya doccument alizotumia Simon Group ni forged?
   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kuna mtu analindwa hapa na ngoma inazidi kuwa haluwa
   
 5. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Fantastic stuff! Shukrani Invi!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wanasema "every cloud has a silver lining".. sijui ndio msemo unaofanana na "kila marefu..."? Thanks!
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hebu tujikumbushe jinsi Meya wa jiji la Dar es Salaam alivyopatikana. Wagombea ubunge wa Dar es Salaam kupitia CCM walikua wakienda kuunga foleni na wagombea udiwani wao kusubiri laki tano bila aibu na sasa matokeo yake ndio haya na itafuatia sasa Coco Beach ambayo Masaburi atataka anayeendesha anyang'anywe apewe Manji.

  Tusisahau Yussuf Manji ni mmoja wa wafanyabiasharawaliokua wakitaka kuinunua UDA na hajakata tamaa hadi sasa na hata huyo Simon Group asidhani yuko salama kwa hili hata kidogo na tayari kuna dalili atakosa na Manji ataichukua UDA kiulaini.

  Yusuf Manji 'anunua' madiwani Dar

  • Amwaga 500,000/- kwa kila mgombea


  na Betty Kangonga Tanzania Daima jumatano, 22 septemba 2010


  MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuph Manji, anadaiwa kuwahonga fedha wagombea wa nafasi za udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuhakikisha wanamchagua mmoja wao kuwa meya wa Jiji la Dar es Salaam, kuziba nafasi ya Adam Kimbisa, aliyemaliza muda wake.

  Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya duru za CCM, vilidai kuwa mfanyabiashara huyo amekuwa akigawa sh 500,000 kwa kila mgombea udiwani wa CCM ili kuhakikisha mtu anayempigia chapuo, anashika nafasi hiyo nyeti jijini Dar es Salaam kwa masilahi yake binafsi.

  Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata zilisema kuwa mbali ya kutaka mtu wa karibu yake apate nafasi ya umeya wa jiji, pia anadaiwa kuwasaidia baadhi ya madiwani kushinda nafasi za umeya wa halmashauri za wilaya za jijini Dar es Salaam.

  Habari zinasema kuwa Manji amekuwa akiwapata wagombea hao wa udiwani kupitia baadhi ya wagombea ubunge wa majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakionekana katika ofisi za mfanyabiashara huyo mwenye asili ya Kiasia.

  "Huwezi amini ninachokisema, kama unataka fika ofisini kwa Manji, utashuhudia haya ninayozungumza. Kuna msafara wa foleni utafikiri kuna mkutano ndani ya ofisi hizo, kumbe watu wanachukua pesa," kilisema chanzo hicho na kuongeza kuwa ameahidi kuwapa zaidi awamu nyingine.

  Baadhi ya wagombea udiwani waliopata fedha hizo ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sasa, walilithibitishia Tanzania Daima Jumatano kupokea fedha hizo na kuongeza kuwa sambamba na fedha hizo, Manji amewapa majina ya watu wanaofaa kuwania umeya wa jiji na halmashauri za wilaya.

  Hata hivyo hatua hiyo imelalamikiwa na baadhi ya wana CCM kwamba si ya kiungwana na haipaswi kuvumiliwa kwa kuwa inavunja demokrasia nchini.

  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu, Manji kwanza alihoji chanzo chetu cha habari hizi. Hata hivyo mfanyabiashara huyo baadaye alikiri kutoa fedha hizo.

  Alisema amekuwa akitoa fedha hizo mbele ya baadhi ya wagombea ubunge wa CCM wa majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam na amekuwa akifanya hivyo kutokana na mapenzi yake kwa CCM.

  Alisema mara nyingi amekuwa mstari wa mbele kusaidia wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa CCM kwa ajili ya kuhakikisha wanashinda nafasi nyingi za uongozi na kuvibwaga vyama vya upinzani.

  Alifafanua kuwa katika ugawaji wa fedha hizo, wapo baadhi ya wagombea wa udiwani ambao hawakufika katika mgawo huo, lakini aliwaomba wasubiri mpaka atakaporudi kutoka katika safari yake anayotarajia kuondoka leo. Hata hivyo hakufafanua.

  "Sioni tatizo kutoa fedha kwa ajili ya chama changu ili kipate ushindi wa kishindo. Ni kweli nilitoa kiasi hicho cha fedha lakini sikuwa peke yangu, nilikuwa na wagombea wa nafasi ya ubunge ambao ndio walifika na madiwani na nikaahidi awamu ya pili nitawapa baada ya wiki mbili nikitoka safari," alisema Manji.

  Hata hivyo alikataa katakata kwamba wakati akiwapa fedha hizo hakutoa majina yoyote ya watu anaotaka wawe mameya, ingawa wapo baadhi yao waliomuomba awasaidie ili waweze kupata nafasi hizo.

  "Siwezi kukataa, ni kweli najua baadhi ya wagombea udiwani ambao wamekuja kwangu na kuomba niwasaidie fedha kwa ajili ya kupata umeya, lakini nitakuwa si mzalendo iwapo nitaamua kuingilia suala hilo, kwa kuwa hata hiyo nafasi ya udiwani wanaweza wasishinde, sasa itakuwaje wapite kwenye umeya?" alihoji Manji.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa (CCM), Yusuf Makamba, alisema taarifa hizo ndiyo kwanza anazisikia, lakini kamwe chama hakimkatazi mwanachama wake kukichangia, ili mradi afuate utaratibu uliowekwa.

  Hata hivyo Makamba aliwashangaa wagombea udiwani wanaohangaika kusaka viti vya umeya wakati hata Uchaguzi Mkuu haujafanyika.

  "Hii taarifa inatia aibu. Hawa wagombea wanachekesha sana, maana wanaamini vipi watashinda nafasi hizo wakati hata uchaguzi bado? Utaratibu wa kugombea umeya unafahamika, ukifika wakati wake watatangaziwa wachukue fomu," alisema Makamba.
   
 8. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 1,108
  Trophy Points: 280
  Na sinema yetu inaendelea
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Thanks invisible; usisahau kuhusu 3T pia we r still waiting!
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh! kweli bongo tambarare, kwa namna sakata hili lilivyokuwa linaendelea ilikuwa rahisi kufikiri haya mambo yalikuwa ni kati ya bodi ya wakurugenzi UDA na Dar City Council.

  Lakini ukisoma hiyo barua ya SGL kopi zilipelekwa kwa Waziri wa fedha na katibu mkuu wake, waziri wa uchukuzi na katibu mkuu wake. That means walikuwa wanajua na pengine walishakatiwa chao mapemaa otherwise hao vigogo muda wote huu wamefanya ufuatiliaji upi kuhusiana na hili sakata????

  Barua ni ya tarehe 16/06/11 na the deal has been on at least by115 days before that date. Hivyo basi kisingizio cha kutokufahamu ni kichekesho!!!!!
   
 11. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa hapa kuna ishu gani? Tayari tunafahamu kuwa hao Simon Group wamekuwa major shareholderz!
  Hizo ni minutes za mkutano wa shareholderz! Ungeleta mkataba or certificates ya hizo share ambapo kwenye hizo certificates kumeonyeshwa vitu vya muhimu kama price per share ndio ningeona umefanya cha maana!
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nimezisoma documents zote naweza kusema kitu kimoja kuna mtu behind Simon Groups aliyekuwa anasuka mpango wa kuchukua UDA jumla. Simon haikuwa na haki ya kuitwa mwanahisa kwani hadi Juni, 2011 haikuwa imelipa senti tano ya hisa walizokuwa alloted zilizokuwa na thamani ya zaidi ya Tshs 200 milioni. Sasa Simon ilikuwa kama nani katika mkutano huo batili wa extra ordinary meeting???

  Pia nakubaliana na mwanasheria Lyimo kuwa Dr Masaburi alitakiwa atoe kibali kilichomruhusu kuitisha mkutano huo kutoka kwa macouncilor wa jiji la Dar-es-Salaam. Dr Masaburi haongozi shirika lake binafsi ni Meya wa jiji na hivyo alitakiwa kupata kibali kutoka kwa councilor wa jiji kuitisha hicho kikao tunaomba atuambia hicho kikao aliitisha lini na kwa nani? Bila ya hivyo hakuwa na mandate ya kuitisha kikao cha wadau wa uda.

  Tatu kuiengua bodi kunatakiwa ruhusa ya majority shareholders or shareholders approval. Simon walikuwa hawana shares mpaka walipoitisha kikao chao na hivyo shareholders wa mwanzo bado ndio walikuwa wamiliki halali je ni kina nani na kwanini hawakushirikishwa. Na sheria ya Company law inasema ni muhimu minority shareholders washirikishwe katika maamuzi hayo je kwanini hawakushirikishwa?

  Kunaonekana kuna mchezo mchafu ulikuwa unataka kutokea wa kubandika na kubandua watu wameshaanua matanga na kuendelea na shughuli zao. Dr Masaburi hapa amechemka namuonea huruma kama hizi document ni authentic!!! Shukrani Invisible na bado tunasubiria zile Trilioni 3 sijui Trilioni 7 kwani kila mmoja mjini anazungumzia lake nakuaminia sana mkuu.
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huwezi kuwa mwanahisa au kuanzisha kampuni bila ya kuwa umelipa pesa yote ya initial capital au shares alloted rejea katika company act ya Tanzania mkuu. Simon walikuwa hawajalipia bado zile milioni 200 na ushee ya shares walizokuwa alloted na hivyo kisheria hawakuwa wanahisa UDA. Labda na wewe tuletee taarifa zinazoonyesha walikuwa wanahisa kamili kabla ya huo mkutano.
   
 14. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  Hiki ni kichekesho....uuzwaji wa shares unaonekana ulikuwa na walakini.
  Lingekuwa ni jambo la busara kama kuna mtu angetupatia Articles of Association kati ya Simon Group na Dar es salaam City council.
   
 15. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kweli nchi hii hatutakuja tupate maendeleo kamwe. Ndiyo maana mimi naamini kuwa tiba ya matatizo ya nchi hii ni kuiondoa ccm madarakani basi. Vinginevyo, chama hiki kimekuwa ni mtandao mpana wa wezi na majambazi yanayohujumu uchumi. Dawa yake ni kuuondoa mtandao huo.
   
 16. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kumbe huyu masaburi yeye ndio alikuwa anafikiria kwa (NENO LAKE). Wabunge wa Dar naona walikuwa sahihi. Kidogo anibadilishe nione kweli ameonewa na ni mpinga mafisadi
   
 17. n

  niweze JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli hii nchi kuna wapenda mali za wananchi kweli kweli. Kwanini Idd Simba na Robert Kisena wasijiunge na silicon valley huko US wakawa truelly entrepreneurials badala ya kujaribu kila njia kuwafilisi wananchi? kuna mwanaccm yeyote alie na mikono misafi? Wote ccm ni majambazi matupu

  Kulikuja intellectuals (wajinga wote) wakaanzisha na kufungua NGOs na miaka hii michache ccm wamegundua na ku-pattern vitu vipya vinaitwa 'consulting and investments' za kutumia raslimali za wananchi. Mifano mikubwa ni hii Saimon Group and Serengeti Advisers.

  Check their web links na jinsi gani wana-accumulate wealth katika nchi yetu, hawana fear wala shame. These are tools to grab land and resources in the name of creating private sectors Tanzania. These are the most fearful groups in Tanzania today. Idd Simba na Kisena wanakwenda oversea na wakiona Steve Jabs au Bill Gate wanafikiria moja kwa moja we can recreate the same innovation and twists in Tanzania na kujipa majina ya CEOs na Directors. They know how the constitution is working in Tanzania and the only call they need to make is ikulu or just show up at the ikulu gate.

  We thank all who work hard to make sure watanzania wanapata hizi docs. Huyu kijana wa Makamba alizungumzia transparency kwa kikwete, mbona achangii humu? Si anasema kikwete kaleta transparency Tanzania, what a shame this is...

  http://www.serengetiadvisers.com/category/insight-foresight

  http://allafrica.com/stories/201108070099.html
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  CCM inaangamia kwa kukosa maarifa.
  Kuna haja Chadema wafungue kituo cha TV na redoi ili huu uozo na mwingine mwingi ambao umekuwa ukifanywa na CCM na serikali yake utangazwe ili Watanzania wajue ni kwa jinsi gani wanahujumiwa. Sio kila mtu ana access na magazeti na jamii forums.
   
 19. 911

  911 Platinum Member

  #19
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Ngoja nizi_save,ntazisoma Jumatatu!Nisije nikaharibu weekend yangu.;-)
   
 20. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hakuna msemo kila marefu.......... labda 'hakuna marefu yasiyokuwa na ncha'
   
Loading...