Uchunguzi MwanaHalisi usivunje utawala bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchunguzi MwanaHalisi usivunje utawala bora

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 20, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,276
  Likes Received: 5,637
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi MwanaHalisi usivunje utawala bora


  TUMEPOKEA kwa masikitiko makubwa habari ya kuchunguzwa kwa ofisi za gazeti la kila wiki la MwanaHalisi na nyumbani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publisher, Bw. Saed Kubenea.

  Tunatahadharisha uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi usitumiwe vibaya na kuingilia uhuru wa wananchi kutoa na kupata habari ambao ni haki yao ya kidemokrasia.

  Tunasema hivyo kwakuwa kwa namna moja au nyingine kitendo hicho kinaweza kuwafunga mdomo Watanzania wenye nia njema na nchi yao kutoa taarifa za vitendo wanavyoona vinalengo baya kwa nchi yao.

  Vyombo vya habari ndio sehemu pekee ambayo Watanzania wanaweza kuitumia kutoa dukuduku lao kwa uwazi au kwa siri kwa nia ya kubadilisha mwelekeo wa nchi wanaodhani siyo sahihi.

  Kama taarifa zao za siri kwa wananchi wenzao zitakuwa zikipekuliwa na polisi kama walivyofanya, Watanzania wenye taarifa zinazoweza kuiokoa nchi isipotee, watakosa sehemu ya kukimbilia.

  Kama vyombo vya habari vitafungwa mdomo kutakuwa na doa kubwa sana katika demokrasia ya Tanzania na utawala bora ambao unasisitiza umuhimu wa uwazi wa Serikali kwa wananchi wanaoichagua na kuipa kodi.

  Wananchi ndio walioiweka Serikali madarakani na wanastahili kupata taarifa juu utendaji wake na hasa zama hizi ambazo hali ya maisha inazidi kuwa ngumu huku viongozi waliochaguliwa wakionekana kuneemeka.

  Aidha kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kitendo hicho kinaweza kumuharibia na kumfanya ashindwe kuhimiza utawala bora katika nchi nyingine.

  Tunatambua umuhimu wa usiri kwa kila mtu lakini pia tunatahadharisha umuhimu huo usitumike vibaya kuvifunga mdomo vyombo vya habari na kuigeuza nchi kichaka cha wahalifu.

  Pia wanahabari wenzetu tusitishwe na kilichofanyika kwa Bw. Kubenea bali iwe changamoto ya utendaji wetu wa kazi na tunatetea nchi yetu kwa kutumia nafasi tuliyonayo.
   
 2. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwanahalisi,

  Hii imekaa kama press release ya IKULU a.k.a CCM
  unaweza kutuambia nani kaitoa hiyo statement??????

  Je Tanzania kuna utawala Bora kweli??????????? Tanzania Kuna bora utawala hata kama ni kilaza. Huo uwazi unaozungumziwa hapa ni upi???? wa kuwaficha mafisadiiii?

  Haki ya mwanamchi mpiga kura anaezungumziwa hapa ni nani????

  Kama serikali inawasikiliza wapiga kura wake mbona
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nchi hii walishaiteka na tunatakiwa kukaza buti ili tuwanyang'anye hawa manyang'au. Tukiogopa vitisho kamwe hatutaikomboa na ole wetu wanetu na wajukuu zetu watatoa lawama kwetu. Maana twaanza kuwa watumwa katika nchi yetu wenyewe.
   
Loading...