Uchunguzi : Mamlaka zavuruga biashara ya dawa za binadamu nchini Tanzania , Wenye vibali halali wakandamizwa wasionavyo wapeta

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,089
219,143
Nchini Tanzania iko sheria inayosimamia uendeshaji wa biashara ya dawa za binadamu , inaitwa Pharmacy Act , humu
imewekwa miongozo na utaratibu wa namna ya kufanya biashara hii. Nikiri kwamba mimi si mtaalam kabisa kwenye sekta hii lakini nilipata msukumo wa kuchunguza sekta hii baada ya kushuhudia maduka mengi makubwa ya dawa ( Pharmacy ) yakifungwa kutokana na kushindwa kujiendesha.

Niliyoyaona kwenye uchunguzi wa timu yangu yanatisha. Kumbe kila Pharmacy halali unayoiona mtaani kwako kabla ya kupewa leseni inapitia mchakato mrefu mno. Jengo litakalofanyiwa biashara hii ni lazima lithibitishwe na Mamlaka , kwa maana ya ubora wake pamoja na ukubwa wake. kwamba Retail shop ni lazima iwe na angalau ukubwa wa square meter 25, kwahiyo kumbe jengo lolote chini ya ukubwa huo halitapewa leseni ya kufanya biashara hiyo, taarifa zinaonyesha kwamba kwenye hili Mamlaka haina mswalie Mtume. Kingine ni kwamba jengo hilo ni lazima liwe na A/C ( Kipoza joto ) , ni lazima kuwe na Mfamasia ambaye mshahara wake kwa mwezi mmoja si chini ya Tsh mil 1. Kuwe na mtoa dawa wa ngazi ya cheti au diploma ambaye mshahara wake si chini ya tsh laki 5 na ni lazima awe anatambuliwa na Mamlaka na ni lazima kuwe na mkataba wa kazi kati ya mwenye duka na wafanyakazi wake uliosainiwa na mwanasheria .

Duka hilo ni lazima liwe na mashine ya EFD ambayo mwenye duka ananunua kwa pesa zake ambazo si chini ya tsh laki 8 na halipwi na yeyote. Lazima kuwe na leseni ya biashara ya manispaa, Temeke kwa mfano leseni hii baada ya kuja kwa DED mpya gharama yake ni Tsh Laki 4 , kabla ya DED wa sasa leseni ilikuwa Tsh laki 2. Kwenye duka hilo kunapaswa kuwe na certificate ya Fire na mtungi wake ambapo gharama yake ni tsh Laki 2. Kuna makampuni ya kuzoa taka ambayo bei ya kila mwezi inatofautiana kulingana na eneo.

Kwa ufupi hizi ni baadhi ya gharama anazokumbana nazo Mfanyabiashara halali wa dawa za binadamu nchini Tanzania. Pamoja na yote haya mfanyabiashara huyu amezungukwa na maduka uchwara na haramu yasiyo na vigezo vyoyote na yanayouza dawa za binadamu kama anazouza yeye bila kufuata utaratibu wowote wa kisheria wala wa kitaaluma, hayakaguliwi na yeyote na wala hayana leseni yoyote na wala hayalipi kodi yoyote, wala hakuna mashine ya EFD wala hata TIN. Mbaya zaidi hayana wataalam wa kutoa dawa kama mamlaka zinavyoagiza, ni maduka yaliyo hadharani na yanayoonekana bila kificho huku mamlaka zikifumba macho. Taarifa zaidi zinadokeza kwamba hata ukaguzi mdogo sana unaofanywa na Mamlaka bado waathirika ni wale wenye leseni halali wanaofahamika, ambako faini za kijinga hutozwa wakati mwingine kwa kumkuta mtoa dawa hakuvaa koti jeupe tu, mamlaka hazihangaiki kukagua maduka feki yaliyofunguliwa mitaani bila utaratibu wowote , yasiyozingatia taaluma , tena yaliyo kwenye majengo ambayo hayawezi kabisa kutunza ubora wa dawa zenyewe .

Ni ukweli kwamba Wananchi wanahitaji huduma ya maduka ya dawa mitaani, hili halina ubishi, lakini kuacha taaluma na kukubali kila mtu awe ana duka la dawa popote bila utaratibu wowote huku si kuwahurumia wananchi bali ni kuwamaliza. Pia ni kuwakatisha tamaa watu werevu walioamua kuuza dawa kihalali kwa ubora unaostahili na ni kuwakandamiza walipa kodi halali bila sababu yoyote ya msingi na ni uonevu wa hali ya juu kabisa, Mfanyabiashara halali anayelipa mishahara mikubwa na ambaye ni mlipa kodi halali hawezi kushindana na wasiolipa chochote, ni lazima atabwaga manyanga , ni wazi kwamba mamlaka zimeshindwa kuwalinda au hazijui zinachotaka kati ya Taaluma na ubora na huu uchafu wa mitaani .

Iko wapi mipango ya TFDA ya mwaka 1999 ya kuondoa maduka uchwara na kuyaboresha kwa kuyahamishia vijijini chini ya usimamizi wake?

..... ITAENDELEA BAADA YA KUKAMILIKA UCHUNGUZI TUNAOUFANYA HAPA TANDIKA MWEMBEYANGA .
 
pamoja na yote haya mfanyabiashara huyu amezungukwa na maduka uchwara na haramu yasiyo na vigezo vyoyote na yanayouza dawa za binadamu kama anazouza yeye bila kufuata utaratibu wowote wa kisheria wala wa kitaaluma , hayakaguliwi na yeyote na wala hayana leseni yoyote na wala hayalipi kodi yoyote


Hizi huwa ni part time sources of revenue za wakaguzi na wasimamizi kutoka Halmashauri, kuna rafiki yangu ana duka linaloendeshwa kwa mtindo huo, wakija anakata maisha yanakwenda
 
Hizi huwa ni part time sources of revenue za wakaguzi na wasimamizi kutoka Halmashauri, kuna rafiki yangu ana duka linaloendeshwa kwa mtindo huo, wakija anakata maisha yanakwenda
Aiseeee !!!!
 
Habar yako kiongoz?ktk sekta hii kumekuwa na changamoto nyingi ususani walio dhamilia kufanya kazi na kutoa huduma hii.mfano mwanza wameonewa sna walichukuliwa DAWA zao.kisa hawako maeneo sahihi lakini wazo likaja kuunda Chama cha watoa huduma ya kuuza dawa za binadamu,zoezi likafanikiwa uongoz hadi mwana sheria ikabidi kuanza hatua moja hadi mwisho Mh mkuu wa Mkoa zaidi ya Mara kadhaa,kwa waziri husika lakini mbio hazikuzaa matunda.ila mtoa hukumu ni mahakama sasa kesi ikaenda kwakuwa mungu siku zote huwa wawanyonge zaidi ile kesi wakashinda waliochukuliwa dawa.sasa hadi leo haki haijatendeka kitu kinacho umiza kwakuwa walishindwa kesi wanampa kibali mtu mpya atakae fungua eneo ambalo upo na wamezuia hilo eneo kisa wakukomoe na wameenda mbali zaidi hadi kuwarubuni washitaki wao baadhi kuwapa kibali cha mda mfupi,ili kuua nguvu ya wanachama husika.kifupi inaumiza sna mwenye dhamana kutangulia yye alafu sheria na taratibu kuziacha nyuma yake.kifupi tunaumizana sna na mungu anawaona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ummy Mwalimu kama unanisoma bado hujachelewa unaweza kurekebisha hali hii
 
Back
Top Bottom