Uchunguzi: Chanzo cha matatizo katika sekta ya Umeme Tanzania na ujio wa IPTL

Mkuu Jb, hauko mbali sana na ukweli, hiyo miaka unayotaja labda wameichakachua kwenye record zao! Na kuna kitu kisicho cha kawaida kuhusu kadhia hii, wanajaribu sana kutomhusisha mzee mwinyi ktk dili hili na nadhani ndiyo sababu ya kusogeza kidogo miaka inayotajwa, wanasahau kuwa hawawezi kufuta rekodi za ziara za viongozi na maafisa wa serikali zilizozaa wizi huu! Kwa mtazamo wangu iptl ndiyo imehusika kwa % kubwa kuidhoofisha Tanesco, kwa karibu miaka ishirini inaikamua Tanesco tu bila tija yoyote. Tujaribu kupata kwa siku au mwezi tunailipa iptl kiasi gani mtachoka humu ndani.
Big up sana mkuu.

Nimedhamilua kuutafuata ukweli na kila kitu kitakuwa wazi, nitasafiri kwenda Vietnam na Malaysia kuutafuta ukweli huo!
 
Lete ukweli sioni mwendelezo wa scandal yenyewe au ndo wamekutisha mkuu?
 
Baada ya kuwa kwenye mgogoro wa umeme nchini Tanzani yapata miaka karibu 15 sasa, nimeamua kufuatilia hasa tatizo lilianzia wapi na nani waliohusika.

Nilianzia ndani ya Wizara ya nishati na madini kwa kufuatilia mikataba iliyoyaingiza nchini makapuni ya uzalishaji umeme,

Taarifa halisi na nyaraka zinabainisha kuwa tatizo hili lilianza baada ya mfanyabiashara maarufu bwana Rugemalia kuiingiza nchini kampuni ya IPTL kutoka Vietnam!

Mchakato unatajwa kuwa ndugu Rugemalila alikuwa akifanya biashara ya Mchele kutoka Vietnam mwaka 1995, katika harakati zake za kibiashara huko Vietnam aliweza kuunda urafiki na wanaotajwa kuwa wamiliki wa IPTL hii ya sasa.

Mwaka 1997 kulianza kutokea uhaba wa umeme tanzania ambapo ndani ya Wizara ya nishati na Madini kulipendekezwa itafutwe kampuni itakayozalisha umeme wa dharula wa haraka zaidi ili kunusuru taifa:

Kamishna wake alikuwa ni Ndugu Patrick Rutabanzibwa ambae katika uchunguzi umebaini ni ndugu na Rugemalila ambae ni mfanyabiashara na mmiliki wa Mabibo Heineken ya Ubongo,

Baada ya Rutabanzibwa kuona kuwa pale wizarani kuna mwanya wa kupiga hela aliweza kuongea na mdogo wake ambae katika nyaraka nyingi anatajwa zaidi kwajina moja tu la Rugemalila kuwa atafute kampuni ya kufanya kazi hiyo haraka sana!...


SILLY SEASON! YOU MUST BE IGNORANT OF FACTS. Watu kama nyinyi mnatia aibu kwenye JF kwa umbea. Huyo unaye sema ni mwizi anaidai serikali ya Tanzania Tsh120 Billion
 
"...Kama huu ndiyo ushirikiano wa nchi za kusini, bora ukoloni urudi.'
(‘If this is ‘South-South co-operation", then colonialism is preferable.')
--Julius K Nyerere commenting on IPTL.
 
Rejea na taarifa zinazojulikana kama 'the ugly malyasian' kuna huu uchunguzi wako, nadhani ni Cooksey 2011.

Kazi nzuri mkuu
 
Mkuu unatisha,coherent facts. Keep on informing us but be careful these guys are dangerous!!!

Lakini pia uwe makini.kwani.habari hii haitafurahisha wengine.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Aminia sana JB, ukimaliza hili tupe majina ya walioweka hela zetu huko duniani kwa siri. Hii habari ya muuza mchele na IPTL si ngeni akilini mwangu nilishaisikia. Thanks again JB. Jamani tuichangie JF iendelee kuwepo coz itatupa majina ya wezi wetu wote ili wakati wa kuichukua iwe rahisi na kunyonga mmoja baada ya mwingine. Big JB

Pokea tena like nyingine ya kianalogia..naiona nchi ya ahadi iiiile kwa mbali...Enhe Mola endelea kumpa ujasiri JB!
 
mkuu jb welcome back,tupe ukweli though inauma sana, Huyu baba riz hafai kabisa,yaani anatubebesha mzigo bila hata huruma.
 
jamani baba Ruiz tuonee huruma.unatukamua had I ngozi.
kumbe ndio maana na mzee maumvi nae akaleta Richmond!
ukoo Wa panya tuhurumieni jamani
 
Back
Top Bottom