OCC Doctors
Senior Member
- Jul 20, 2018
- 104
- 151
Maumivu ya uongo, uchungu wa Leba ya uongo (false labor, spurious labor). Leba ya uwongo inapatikana zaidi kwenye mimba ya kwanza kuliko kwa wanawake walio wahi kuzaa awali. Kawaida huonekana kabla ya kuanza kwa uchungu wa kweli wa leba, kwa wiki 1 au 2 kwa mimba ya kwanza na kwa siku chache kwa walio wahi kuzaa awali. Sababu ya maumivu haya ni kunyooka kwa mlango wa uzazi na sehemu ya chini ya mji wa uzazi.
Maumivu ya uzazi ya uwongo huwa ni dhaifu, huzuiliwa kwenye sehemu ya chini ya fumbatio na kinena, hayahusiani na ugumu wa mji wa uzazi, hayana sifa nyingine za uchungu wa kweli wa kuzaa na huondoka kwa dawa za maumivu.
............
Ifahamu leba ya ukweli:
Miezi 9 ya ujauzito huisha kwa kuzaliwa mtoto, tukio la leba hufanya wanawake wengi kuogopa kwa sababu mchakato unaweza kuwa na machungu makali.
Wanawake wengine huwa na wasiwasi juu ya uwezo wao wa kukabiliana na maumivu.
Maumivu ni makali na magumu, na yana mambo mengi ikiwemo kuathirika kisaikolojia. Maumivu kawaida huhusishwa na kuumia na uharibifu wa tishu za kizazi.
Kuongezeka kwa maumivu mwishoni mwa ujauzito mara nyingi ni ishara ya kwanza kwamba leba imeanza.
Wakati wa leba halisi, mikazo ya mji wa mimba huanza taratibu, inayofuata mtindo maalum na yenye nguvu. Mikazo hii huongezeka na haiwezi kupunguzwa kwa dawa za kutuliza maumivu. Ikiwa mwanamke atatumia dawa za kutuliza maumivu, dalili za uchungu zinaweza kutulia kidogo, lakini leba halisi bado huendelea.
Mara nyingi, leba hutokea wakati mtoto ameumbika kikamilifu, kufikia hatima ya wakati anaofaa kukaa mwilini mwa mama, yaani kati ya wiki 37-40 za ujauzito. Leba huashiria mwisho wa kipindi cha mtoto kukaa kwenye mji wa mimba na mwanzo wa maisha nje ya mwili wa mama.