Uchumi wa Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumi wa Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fundi Mchundo, Mar 26, 2008.

 1. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi kweli nchi yenye watu zaidi ya milioni moja( sawasawa na Mauritius) inaweza kujisifia kuongeza export kutoka dola milioni tatu kwa mwezi hadi milioni tisa na nusu? Na hii ikafanywa kichwa cha habari! Tutafika kweli?
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Zenj hawajajisifia, hiyo ni taarifa kwa wananchi na wadau wengine. Hata kama ongezeko lingekuwa ni la senti hamsini, lakini taarifa ikatolewa ni jambo la msingi na busara kuliko kukaa gizani kama Bara...
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Haujanielewa Mkuu!

  Ninachosema ni kuwa hatuwezi kutoka hapa tulipo, sisi wabara na nyie wazanzibari, kama tutaendelea kuona vitu kama hivi kuwa ni mafanikio. Takwimu kama hizi huwa zinatolewa sana hata na Bara ambako wakati mwingine ili kuzijazia jazia wanajumuisha za miaka kadhaa. Wenzetu walikuwa kila kukicha wakijipima na wenzao waliowapita na kupanga mikakati ya namna gani kuwafikia.

  Mapato ya export ya nchi ya watu milioni 35 hayajagusa $ bilioni moja kwa mwaka ambapo kanchi ka watu milioni moja kamauritius wanaexport mabilioni ya dola! na hawana mafuta.

  Ni lazima tuchukie umaskini wetu ndio tutaweza kujinasua. Si suala la Bara na Zanzibar. Ni letu wote.
   
 4. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Fundi uko pessimistic sana. Hapa umekurupuka tu kuuona umasikini wetu lakini hukufanya uchambuzi wa hiyo habari. Ukaangalia background information kuhusu exports revenues na imports za Zanzibar kwa angalau mwaka (miezi) iliyopita. Hiyo habari inaeleza hapo kuwa kumekuwepo na juhudi inayofanyika kukuza mapato na kupunguza matumizi na hivyo huko ndio kunakoitwa kukua kwa uchumi. Hasa kwa vile huko Zanzibar kwa muda mrefu kumekuwepo na trend iliyokuwa ikionyesha kuwa kinachotolewa kwa kununua kutoka nje (import) ni kikubwa kuliko kinachopatikana kutokana na mauzo (exports). Ukuaji kama huu ndio utakaotuwezesha siku moja nasi ku export kwa Mamilioni kama wafanyavyo wenzetu wa Mauritius. Hawakufanya kwa siku moja hao. Usiwavuje moyo Wazenj wacha tuombe kusikia katika habari ijayo kuwa wameuzxa vinavyofikia Milioni angalau 12 badala ya tisa za hivi sasa.
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ingawa sina kawaida ya kukurupuka lakini kila kitu kina mwanzo. Mimi siko pessimistic. Kwa nini kila siku tunapenda kujiweka chini? Mauritius wanaingiza zaidi ya $millioni 900 kutokana na utalii. Wamewekeza kwenye Information technology, financial services na huduma nyingine zitakazoendeleza uchumi wao. Hawa walikuwa masikini kama sisi wakitegemea miwa tu! Singapore ilipopata uhuru ilikuwa maskini kuliko nchi nyingi za kiafrika leo iko wapi? Hapana Mkuu, hii kuridhika na hali yetu ndiyo inayotuweka hapa. Tumebaki kutegemea windfalls kama mafuta na misaada kutoka kwa wenye kutuonea huruma badala ya kupanga mikakati ya namna gani tutawafikia.

  With all due respect, kwa mwendo huo unategemea lini serikali ya Zanziba itapata surplus?Hayo mapato hata yakiongezeka mara dufu hayatatutoa hapa tulipo, nchi ya nne masikini duniani. Hizo gains zimetokana na mabadiliko ya bei ya karafuu, zao la asilia. Kwingine kote the situation is dire. Consumer goods importation increase ni kwenye nguo na viatu, vitu ambavyo ni basic! Mapato jumla ni chini ya dola millioni mia moja! Utalii unaingiza chini ya dola milioni tano kwa mwezi ambapo wenetu wanaingiza on average milioni 80! Bado tusikasirike?

  Tunahitaji kufanya kazi ya ziada, Mkuu. Kama alivyosema Mwalimu R.I.P, inabidi tukimbie wakati wenzetu wanatembea. Tupongezane, ndio, lakini tukumbushane kuwa bado safari ni ndefu! Hakuna njia ya mkato.
   
 6. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  maneno ya wenzetu kule bara nimekusoma, ama kikwetu nimekuelewa vilivyo.

  tuombe mungu baada ya muafaka na kuja na serikali ya kitaifa iwe na lengo la makusudi kutafuta njia za kunyanyua kiwango cha uchumi wetu.

  uchumi wetu kuwa unadorora tusitafute mchawi hatujajituma bali tumeweka siasa mbele, kuna vitu tuone aibu jamani na tuukubali ukweli.

  kama tuko darasani tuna haki kuambiwa tunacheza hatutaki kusoma
   
 7. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sadakta Fundi. Nimekuelewa. Na kumradhi kwa kusema umekurupuka. Nakubabaliana na vision yako, hasa katika kuimarisha utalii, na kuacha kutumia fedha nyingi kununua nguo, viatu au mchele ambavyo vinaweza, tukiimarisha uzalishaji, kupatikana hapa hapa TZ. Tatizo la Zenj siasa na ubishani wa kugombania madaraka vimetawala sana, na ndiyo maana kuna kulegalega. Watu wote (hata wataalamu wetu wa kilimo na uchumi), kule, wanachapa siasa tu. Tunahitaji watu wenye mtizamo kama wako kuwasaidia wenzetu wa Zenj. Endelea kuwahamasisha, Fundi, kila upatapo nafasi.
   
 8. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mapato ya Zanzibar kwa mwezi hayazidi pesa anazolipa Rostam Aziz kwenye kodi!

  Aziz ameripoti kulipa zaidi ya USD 100 m, Zaznibar inacheza kwenye single digits!

  And then watu wanataka kuja na excuses.
   
 9. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2017
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Tutafika tu
   
Loading...