Uchumi kupitia miundombinu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumi kupitia miundombinu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by TingTing, Dec 30, 2009.

 1. TingTing

  TingTing Member

  #1
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Itakuwa ni jambo la busara sana kama zikitengenezwa Super Highway tatu tu Tanzania nzima ambazo ni two lanes pande zote kwenda na kurudi. Hii itapunguza idadi ya ajali kwa asilimia kadhaa na pia itasaidia kumovuzisha bidhaa 24/7hrs. Moja inayotembea kutoka mashariki kwenda magharibi, nyingine kutoka Kusini Magharibi kwenda Kaskazini Mashariki, nyingine kutoka Kaskazini Magharibi kwenda Kusini Mashariki

  Ingekuwa tumejaliwa uwezo basi ningetengeneza barabara mpya kabisa on a straight line if possible tofauti na zile ambazo tayari zipo. Barabara hizo kubwa nchini ni kama ifuatavyo;

  1. Dar/Bagamoyo/Kibaha - Kilosa - Dodoma - Manyoni - Tabora - Urambo - Kigoma

  2. Tunduma - Chunya - Rungwa - Manyoni - Mwadui - Musoma

  3. Kagera - Kahama - Tabora - Manyoni - Iringa - Ifakara - Liwale - Nachingwea - Mtwara

  Hapa naifanya Singida kuwa ndiyo center point badala ya Dodoma ili kupeleka maendeleo Singida pia. Baada ya hapo main highways zifuatazo zitaongezewa pia kuwawezesha watu hususan wafanyabiashara kusafirisha mizigo asubuhi na usiku 24/7hrs.

  1. Muleba - Biharamulo - Kigoma - Mpanda - Sumbawanga - Tunduma

  2. Lindi - Masasi - Tunduru - Songea - Njombe - Tunduru

  3. Horohoro - Bagamoyo - Kibaha - Liwale - Lindi

  Hapo matatizo mengi unakuwa umetatua kwa asilimia kama siyo 85 basi angalau 75% na ndipo uchumi wa nchi utakapoanza kunyanyuka kwani miundombinu hususani katika suala la barabara linakuwa limetatua matatizo> Hii pia itatuongezea biashara Bandarini toka mikoa jirani kwani mizigo itakuwa inamove bila vipingamizi vyovyote. Hii tena hadi kelele zipigwe jamaa waamulie kulivulia njuga hili suala!!!
   
Loading...