Shishi
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 1,242
- 45
Wakuu nashukuru sana kwa maada hii nzuri kwani itawapa uandani wa wachumba wenu mlionao.
Kikubwa ni kwamba siku hizi hata maana halisia ya uchumba imebadilika utamkuta mtu anauhusiano wa kimapenzi tayari anamtangaza kwa dugu na jama kuwa ni mchumba of which siyo kweli.
Kingine kibaya hata sisi madada tumekuwa na tabia mbaya sana ya kununua weneyewe pete za uchumba ili tuvishwe kitu ambacho hakina maana yoyote na ndo maana asilimia kubwa huwa hawaoani kabisa.
Kingine kuna mazingira huwa tunavishana pete huwa siyo za heshima kabisa mfano mtu anavishwa pete baa au kwenye matamasha ya mzuki au club hivi kweli hata kama mna mapenzi motomoto kweli hapo kuna uhakika kuwa umechumbia au unataka kutumiwa kwa kisingizio hicho?
Kikubwa uchumba siyo kuvishana pete au hauanzi kwa kuvishana pete ila kuna mambo ambayo yanaonekana tu pamoja na pia kwa uzoefu wangu wanaoanza uhusiano kwa kuambiazana kuwa wataona mara nyingi huwa hawaoani ila mtu anafanya hivyo ili kukupata tu.
Niwape mfano mzuri tu kwa upande wangu mimi nilipompata mchumba wangu tufuata utaratibu ambao hata awe kiwembe asingeruka na kunitelekeza kwani ilikuwa hivi siku ya kwanza alitafuta washenga wakuja kujitambulisha kwetu kwa ajili ya kuleta barua ya uchumba na mambo mengine,siku hiyo kulifuatia na kupanga lini watakuja kutoa mahari wakakubaliana hivyo siku ile ya kutoa mahari ndo siku ya yule ndugu yangu kwa mara ya kwanza kujitokeza kwetu na siku hiyo mbele ya washenga wake na wazazi wangu ndipo tulipovishana pete.
sasa kweli hapo kuna mtu atakimbia kweli si atakuwa amebeba laana ya hali ya juu.
hivyo siku hizi kuvishwa pete ya uchumba imekuwa fashion unakuta mtu mumedo mara moja tu tayari anakuzinguwa kwa kusema anakuvisha pete ya uchumba kumbe wizi mtu halafu unakuta mashuhuda niwalewale wakware wenzie kiasi kwamba hata heshima yenyewe ya pete ya uchumba kwa kipindi hiki kimepitwa na wakati.
wakuu ni hayo tu.
kumbe na avatar yako hiyo kali u are a she???? mmmmnh haya we!!!